CUF KUENDELEA KUIGOMEA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR.

Na Mwandishi wetu Boston

Maalim Seif awsili Boston kwaajili ya mkutano wa hadhara
Makamo wa Kwanza Mstaafu wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, walipowasili uwanja wa ndege wa Logan uliopo Mjini Boston

Maalim Seif Sharif Hamadi akipata picha ya pamoja na wenyeji wa mji huo

Katibu Mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad, akipata picha ya pamoja na Wazanzibar waishio jijini hapa, ili kujianda na  mkutano wa hadhara uliofanyika leo July 30, MAHALI: 42 Charles St Boston
MA 02122. 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad, amesisitiza kuwa Chama chake kitaendelea kuigomea Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Dkt Ali Mohammed Shein.

Maalim Seif Sharif Hamad 

Maalim Seif alitoa sisitizo hilo hapo jana alipokuwa akizungumza na Wazanzibari waishio nchini Marekani kwenye mkutano uliofanyika katika jiji la Boston.

"Tutaendelea kuigomea Serikali, na wala hatushirikiani nayo kwa jambo lolote", alisema Maalim Seif na kuongeza kuwa hatua hiyo tayari imeanza kuiathiri Serikali ya Zanzibar.

Maalim Seif aliwasili jijini Boston jana akitokea jijini Philadelphia ambako alihudhuria Mkutano Mkuu wa Chama Cha Democrats, uliomalizika Alkhamis iliyopita kwa kumpitisha rasmi Bi Hillary Clinton kuwa Mgombea Urais wa Marekani kwa tiketi ya Chama hicho. Uchaguzi Mkuu wa Marekani unatarajiwa kufanyika mapema mwezi Novemba mwaka huu.

Alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege, Maalim Seif anayefuatana na Msaidizi wake Bwana Issa Kheri Hussein, alilakiwa na halaiki ya Wazanzibari wakiongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazanzibari Bwana Sharif Idris pamoja na wanaharakati mbalimbali wa Demokrasia.


Akiwa Philladelphia, Mwanasiasa huyo mkongwe alipata nafasi ya kuhudhuria kwenye Kongamano la Kimataifa juu ya Uongozi Bora ambapo alipata nafasi ya kuonana na viongozi kutoka sehemu mbali mbali duniani wakiwemo Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Bwana Raila Odinga, Rais Mstaafu wa Zambia Bwana Rupia Banda, Waziri Mkuu wa zamani wa Guinea Bwana Cellou Dalein Diallo, Waziri Mkuu wa Denmark Bwana Lars Løkke Rasmussen na wengineo.

Maalim Seif na ujumbe anaofuatana nao, anaondoka leo nchini Marekani kuelekea London baada ya ziara iliyochukua muda wa wiki moja.

No comments:

Post a Comment