Jumuiya ya vijana CUF (JUVICUF) wilaya ya Kaskazini A Unguja leo tarehe 22/10/2016, imefanya Kongamano lao katika Viwanja vya hoteli ya Silver sand,Pwani mchangani Wilaya ya Kaskazini A Unguja.



Jumuiya ya vijana CUF (JUVICUF) wilaya ya Kaskazini A Unguja leo tarehe 22/10/2016, imefanya Kongamano lao katika Viwanja vya hoteli ya  Silver sand,Pwani mchangani  Wilaya ya Kaskazini A Unguja.

Kongamano hilo limelenga katika kujitathmin Zanzibar tulipotoka tulipo na tunapoelekea pamoja na mustakbali wa jumuiya za vijana na jinsi ya kufanya kazi kisayansi.

Katika kongamano hilo lililokutanisha wajumbe wa kamati tendaji za Wilaya za kisiwani Unguja za jumuiya ya vijana wa CUF (JUVICUF),pia viongozi waandamizi wa chama cha wananchi CUF na jumuiya walihudhuria katika kongamano hilo miongoni mwa viongozi hao ni;

Mh.Nassor Ahmed Mazrui (Naibu katibu mkuu CUF Zanzibar),
Mh.Juma Duni Haji (Makamo M/kiti mstaafu CUF),
Mh Salim Biman (mkurugenzi wa habari na uenezi CUF),
Mh. Khalifa ( Mbunge wa jimbo la Mtambwe na M/kiti wa chama wilaya ya Wete),
Mh.Faki Suleiman (Makamo M/kiti JUVICUF Taifa),
Mh.Mahmoud Ali Mahinda (Katibu Mtendaji JUVICUF Taifa),
Mh.Issa Kheir Hussein ( katibu wa Katibu mkuu),
Wajumbe wa baraza kuu chama cha wananchi CUF,
Wawakilishi, wabunge wa chama na
Wajumbe wa kamati tendaji JUVICUF taifa.

Pamoja na mengi katika kongamano hilo Mh. Mazrui amesisitiza kuwaambia vijana kwamba "vijana ondoeni hofu  maana tuliwaahidi kama ikitokea tutashindwa kuipata haki ya Wazanzibar tutawaambia vijana muitafute wenyewe ila musijali bado hatujashindwa na wala hakuna dalili za kushindwa katika hili, haki yenu itapatikana muda sio mrefu"

pia akawasihi vijana kwa kusema " vijana chama kinawategemea hivyo hamupaswi kutetereka kwamaana kama mutatetereka na chama kitatetereka hivyo munapaswa kuwa imara muda wote".

Kuhusu suala la mgogoro iliotengenezwa na *wahafidhina* Mh Mazrui alisema " CUF nichama imara na kitaendea kuwa imara na CUF ndio iliokuza jina la Lipumba na ifahamike ikiwa Lipumba amekianzisha yeye chama cha CUF basi ataweza kukivuruga lakin kama CUF ndio imemtengeneza yeye basi yeye ndio atakae vurugika"

Na mwisho kabisa akawaambia yakwamba  ikiwa CCM wanasema Maalim ni Simba mzee basi niajabu kuona Simba mzee kumpita Paka jike kwa kura zaidi ya elfu ishirini na tano (25,000)".

Nae mh Juma Duni Haji amesema kwa mzalendo yoyote hawez kukubali kununulika " mzalendo hawezi kurud nyuma wala kukubali kutiwa bei,mimi hapa nimeteswa na kufungwa lakin bado naamin katika ukombozi kwasababu *I HAVE  A MISSION* na siwezi kukubali kurudi nyuma mpaka malengo ya ukombozi yakamilike."

Mwisho nae babu Duni amewaambia vijana ya kwamba " Vijana musijali,kuhusu haki yenu ya 25,october kwamaana kijungu kipo jikoni kinapwaga na sio kijungu cha mawe bali nicha maboga,hivyo vijana muwe tayari kuyapokea mamlaka yenu kamili"

Naye Katibu mtendaji wa JUVICUF taifa Mh Mahinda amesema " Hakuna wakumzuia Maalim Seif kuzungumza na Wazanzibari,na waumin wenzake akiwa msikitini, na siku watakapo jaribu kumkamata au kumdhalilisha kiongozi huyo basi katu Vijana wa CUF na Wanzanzibar wazalendo hatutokubali nandio itakua mwanzo wa fujo katika nchi hii" alimalizia kwa kusema "tumechoka na hatuwezi kukubali tena kuwa maridhia"

Mwisho Mh.Salim Biman alifunga kwa nasaha nyingi kwa vijana pamoja nakuwataka vijana kuwatayar kuyapokea mamlaka kamili baada ya kazi kubwa walioifanya.
Pia aliwapongeza zaidi vijana wa JUVICUF wilaya ya Kaskazini A kwakuonesha mfano kwa kufanya jambo kubwa la kuwakutanisha vijana kwalengo la kujenga

Abeid Kh Bakar
N/M/Habari na Uenezi
JUVICUF - Taifa

No comments:

Post a Comment