TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU ZIARA YA KATIBU MKUU WA THE CIVIC UNITED FRONT (CUF-Chama Cha Wananchi) KATIKA WILAYA ZA KISIWA CHA UNGUJA ILIOANZA TAREHE 1

Image may contain: 2 people, hat and outdoor

April, 1 2017 Katibu Mkuu wa The Civic United Front (CUF-Chama Cha Wananchi), Maalim Seif Sharif Hamad, ataanza ziara ya kichama ya siku tisa katika Wilaya saba za Mikoa mitatu ya kisiwa cha Unguja.
Ziara hiyo itaanza Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja ambapo Maalim Seif Sharif Hamad atafanya ziara maalum ya kutwa nzima katika kisiwa cha Tumbatu na baadae, siku zinazofuata, kuendelea na ratiba ya ziara yake katika maeneo mengine ya kisiwa cha Unguja.
Katika ziara ya kisiwa cha Tumbatu Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad amepanga kutembelea maeneo mbali mbali ya kisiwa hicho hasa yale yaliyoathiriwa kwa kuchomwa moto na makundi ya vijana maharamia wanaojulikana kama mazombi.
Kama ilivyo kawaida yake katika ziara za aina hii, Maalim Seif Sharif Hamad, amepanga pia kuwatembelea na kuwafariji wananchi wa kisiwa hicho waliopata athari kutokana na kadhia za matukio ya uvunjwaji wa haki za binadamu hasa wale waliopata athari kufuatia kuvamiwa, kupigwa na kujeruhiwa na makundi hayo. Kwa upande mwengine Maalim Seif Sharif Hamad atawajulia hali na kutoa pole kwa wagonjwa na kuwafariji wafiwa.
Sambamba na ratiba yake hiyo, Maalim Seif Sharif Hamad atafanya shughuli mbali mbali za uimarishaji Chama katika kisiwa cha Tumbatu kwa kuweka mawe ya msingi, kufungua matawi na majengo mapya ya Chama, kuzindua waratibu wa Chama na kukabidhi kadi kwa wanachama wapya wa chama katika maeneo mbali mbali ya kisiwa hicho.

Baada ya kukamilika kwa ziara katika kisiwa cha Tumbatu, Maalim Seif Sharif Hamad ataendelea na ziara yake katika Mikoa na Wilaya nyengine za Unguja kwa ratiba ifuatayo:
Siku ya Jumapili, tarehe 2 Aprili, 2017 Katibu Mkuu atafanya ziara Wilaya ya Kaskazini ‘A’
Siku ya Jumatatu, tarehe 3 Aprili, 2017 ziara itafanyika Wilaya ya Kaskazini ‘B’
Siku ya Jumanne, tarehe 4 Aprili, 2017 Katibu Mkuu atafanya ziara Wilaya ya Kusini Unguja.
Siku ya Jumatano, tarehe 5 Aprili, 2017, Maalim Seif Sharif Hamad atafanya ziara katika Wilaya ya kati. Kuanza ziara yake kwa siku hiyo, Maalim Seif Sharif Hamad atafanya ziara maalum katika kisiwa cha Uzi na Jumamosi tarehe 8 Aprili, 2017 ataendelea na ziara yake katika maeneo mengine ya Wilaya hiyo.
Jumapili tarehe 9 Aprili, 2017, Katibu Mkuu ataendelea na ziara yake katika Wilaya ya Mjini, na Jumatatu tarehe 10 Aprili, 2017 ziara itafanyika Wilaya ya Magharibi ‘B’ kabla ya kuhitimisha ziara yake kwa kutembelea Wilaya ya Magharibi ‘A’ siku ya Jumanne tarehe 11 Aprili, 2017.
Imetolewa na:
Hisham Abdukadir
Afisa Habari na Mawasiliano
The Civic United Front
CUF-Chama Cha Wananchi
Makao Makuu-Zanzibar

No comments:

Post a Comment