Chama cha Wananchi CUF Chaahidi Uchimbaji Mafuta Ndani ya Siku 100

Mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama cha wananchi-CUF- Maalim Seif Sharrif Hamad amesisitiza kuwa  anahitaji siku 100 tu kwa Zanzibar kuwa na mamlaka yake kuhusu sera  na uchimbaji wa mafuta  kisiwani humo.
Maalim ametoa msimao huo wakti akiwahutubia  wanachama,wapenzi na wananchi waliohudhuria  katika mkutano wa kampeni za urais zinazoendelea visiwani Zanzibar uliofanyika Sebleni nyumba za wazee  mjini unguja  ambapo  amesmea CUF haijachupia agenda ya mafuta  na  sera hiyo bado iko mikononi  mwa uopande wa pili wa muungano.

Mgombea huyo wa urais wa Zanzibar ambaye pia ni katibu mkuu wa CUF na makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar aliwahakishia umati huo na wananchi kwa ujumla kuwa serikali ya CUF itakuwa na mfumo mzuri wa kuhakikisha haina shida ya soko la ajira na kusema seriklai yake itapigania kubadilisha hali ya maisha ya wananchi.

Katika mkutano huo Maalim Seif alitumia fursa ya kuwanadi wagombea ubunge,uwakilishi na udiwani wa chama hicho kwa majimbo ya magomeni na amani katika hatua nyengine pamoja na kuwepo wagombea 14 wa urais bado vyama vya CCM na CUF ndivyo vianvyonekana kuwa na mikutano mingi ya kampeni huku badhi ya vyama vyemngine havijannza kampeni zao za urais.

No comments:

Post a Comment