Bunge la 11 la Tanzania lakiri kwamba Serikali ya Zanzibar ni kharamu.

"Hansard" ni neno la kingereza ambalo maana yake ni kumbukumbu za mijadala inayofanywa na wabunge wakati wabunge wakiwa katika vikao vya bunge, neno hili "Hansard" ni jina la mwandishi na mpiga chapa maarufu nchini uingereza ambaye alikuwa akiitwa "Thomas Curson Hansard" neno hili lilianza kutumika baada ya bwana "Hansard" alipokuwa akiandika na kuchapisha kumbukumbu za bunge la Uingereza kwa wakati huo.

Kwa mujibu wa "Hansard" za bunge la 11 kikao cha 3 serikali ya Mapinduzi ya zanzibar uliyopo Madarakani kuanzia Anaeitwa Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein, mawaziri wake hadi wanaojiita wawakilishi waliopatikana baada ya kinachoitwa uchaguzi wa Marudio wa Machi 20 mwaka huu basi serikali hiyo yote ni kharamu na haifai kwa wananchi wapenda haki kushirikiana nayo.

Nadiriki kusema hivyo na nikiomba wasomaji wanielewe kwamba haya si maneno yangu, bali ni maneno ambayo yamekubalika na bunge zima la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambalo linaendelea na vikao vyake katika mji mkuu wa kisiasa tanzania.

Pamoja na juhudi za Serikali ya Rais dkt. John Pombe Magufuli kupitia kwa Waziri wake wa Habari Mheshimiwa Nape Nauye kujaribu kuwaziba midomo watetezi wa wanyonge Wakitanzania kwa kujaribu kufanya sauti zao zisipae kusikika hewani na kuwafika wananchi ambao wanaliendesha bunge hilo na nchi nzima kwa majasho yao kupitia mzigo mzito wa kodi waliobebeshwa juu ya vichwa vyao hadi mabegani, lakini tunawashukuru, tunawapongeza na tunapenda kuwaambia kwamba bado tunawapenda na kuwaamini wabunge wetu hawa kwa juhudi wanazofanya za kuturikodia angalau kwa simu zao pale muda wa wanapotoa utetezi wao katika bunge hilo na baadae kutusambazia.

Katika vikao vya bunge la 11 la Tanzania vinavyoendelea huko mjini Dodoma alisikika Muheshimiwa Khatibu Said Haji ambaye ni Mbunge wa Konde Pemba akitamka bayana katika bunge hilo kwa kuwaambia wananchi wa Konde na Zanzibar kwa ujumla ndani ya Bunge hilo kwamba wasitoe ushirikiano kwa viongozi madhalimu waliopo madarakazi Zanzibar hivi sasa.

Muheshimiwa Haji alikwenda mbali zaidi aliposema kwamba, "Dini zote duniani zimekataza kushirikiana na madhalim, kwa hivyo nawaomba wananchi wangu wa Konde wasishirikiane na madhalim muda wote wa uhai wa maisha yao".

"Na mimi niwaonyeshe mfano nimeanza, mwakilishi kharamu aliyechaguliwa Machi 20, alinipigia simu nikamwambia ukome, kama ulivyoma kuzaliwa mara ya pili kutoka katika tumbo la mamako, na nikamwambia kuwa asinisogelee..." alimalizia Mh. Haji.

Kumbukumbu za bunge letu linatuonyesha kuwa, endapo bungeni kutatokezea jambo lolote ambalo aidha mbunge, Spika ama naibu spika analielezea na jambo lile si sahihi au halikuupendeza upande mmoja wapo wa wabunge, kama tujuavyo bunge letu ni la pande mbili, upande mmoja ni wa walio wengi ambao ni wa Chama cha Mapinduzi - CCM na upande mwengine ni wa vyama vya upinzani, hivyo ikitokea hali hiyo ya kutoridhishwa na kinachoelezewa basi upande usioridhika au kutounga mkono kauli hiyo basi huzua vurugu, vurugu hiyo inaonyesha kutounga mkono au kutokubaliana na jambo hilo, muda mwengine hupelekea spika wa bunge/naibu spika kuakhirisha kikao ili kutafuta muafaka kupitia kamati maalum au hata wakati mwengine hulazimika wabunge wasiokubaliana na hoja kutoka nje ili kujiweka mbali na hoja hiyo na hata muda mwengine spika hutumia rungu lake kwa kuwatoa wale wasiokubaliana na hoja iliyopo mezani.

Lakini kwa hili la Mh. Khatibu Said Haji ambalo alikuwa akijaribu kulitambulisha bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania linaloendelea pamoja na ulimwengu kwa ujumla juu ya ukharamu wa Serikali ya Zanzibar iliyopo madarakani  ambayo inaongozwa na Dkt. Shein, wabunge wa pande zote mbili kuanzia  ule upande wa upinzani ambao una wabunge wachache kulinganisha na wingi wa wabunge wa chama tawala cha CCM, lakini pia na huo upande wa wabunge wa chama tawala cha CCM ambao ndio wenye wajumbe wengi bungeni humo, mbali ya wingi wao, ndani ya bunge hilo pia muna mwanasheria mkuu wa Serikali ya Tanzania ambaye ni mwana CCM, muna mawaziri wa Serikali ya Tanzania wote ni kutoka CCM, Mh. Spika ndugu Job Ndugai ni mbunge wa CCM pamoja na Naibu spika pia ni Mbunge CCM wote hawa walibakia kimya bila malalamiko yeyote yakuonyesha kutokuridhishwa na maelezo ya Mh. Haji, bali kwa mbali zilikuwa zikisikilikana kofi za kuunga makono kauli yake.

Hivyo vitendo vyote hivyo ni kuashiria na kuonyesha kwamba, kumbe bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaelewa vyema ukharamu na umutlaki wa Dkt. Shein na serikali yake aliyoiunda kupitia unaoitwa uchaguzi kharamu wa marudio wa Machi 20 mwaka huu, lakini wameamua kusalia madarakani kwa nguvu za kijeshi zilizoletwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli ambapo amerithi hatua hiyo kutoka kwa mtangulizi wake Dkt. Jakaya Kikwete aliyeleta jeshi Zanzibar awali kupindua maamuzi ya wananchi wa Zanzibar waliyoyafanya Oktoba 25 mwaka jana kupitia Jecha Salum Jecha alipoamua kufuta uchaguzi halali, ambapo ulimwengu mzima unajua kitendo hicho cha kuufuta uchaguzi ule ni kinyume na taratibu za kisheria.

Pamoja na yanayofanywa na Dkt. shein na serikali yake kharamu na vikosi vya ulinzi na usalama vya Zanzibar na lile jeshi la Tanzania linalotii amri zote za Dkt. Pombe Magufuli akiwa ndiye Amiri jeshi wake mkuu, sisi watu wa Zanzibar tunalipongeza kwa dhati bunge hilo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuonyesha utukufu wake kwa kukubali kwamba serikali ya Dkt. Shein yote ni kharamu na pia tunafurahi kuona kitendo hicho kimehifadhiwa katika "Hansard" za bunge la 11 katika kikao chake cha tatu.


No comments:

Post a Comment