HOTUBA YA KIONGOZI WA UPINZANI BUNGENI (KUB) MHESHIMIWA FREEMAN AIKAELI MBOWE (MB) AKIWASILISHA BUNGENI MAONI YA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KATIKA OFISI YA WAZIRI MKUU KWA MWAKA WA FEDHA 2016/17

.

Mr Freeman Mbowe speaks to journalists in

Inatolewa chini ya Kanuni ya 99(9) ya Kanuni za Kudumu za Bunge,
Toleo la Januari, 2016
_________________________________


1. SHERIA YA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA MAWAZIRI (MINISTERS – DISCHARGE OF MINISTERIAL FUNCTIONS – ACT, 1980.
Mheshimiwa Spika, kifungu cha 5(1) kinaweka masharti kwa Rais kutengeneza mwongozo wa muundo na utekelezaji wa majukumu ya Serikali yake.
Inasomeka ifuatavyo: Nanukuu “the President shall from time to time by notice published in the Gazette, specify the departments, business and other matters and responsibility for which he has retained for himself or he has assigned under his direction to any minister and may in that notice specify the effective date of the assumption of that responsibility…….” mwisho wa kunukuu.
Mheshimiwa Spika, mpaka sasa Serikali inafanya kazi bila kuwa na mwongozo wa utendaji wake na kazi kwa wizara mbalimbali. Hii ina maana kwamba Serikali inafanya kazi kwa kauli za Rais na Mawaziri bila kufuata mwongozo wowote wenye msingi na uhalali wa kisheria.
Mheshimiwa Spika, mpaka sasa mwongozo wa utendaji wa Serikali kwa kila Wizara (Instrument) unaotumika ni ule uliochapishwa kwenye gazeti la Serikali namba 494A la tarehe 17/12/2010. Kwa mujibu wa Instrument hiyo, majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu ni:

Coordination of Government Business
Leader of Government Business in the National Assembly
Link between Political Parties and Government.
National Festivals and Celebration of Management of Civic Contingencies (relief).
Facilitation and Implementation of Plans for the Development of Dodoma as Capital of Tanzania.
Coordination and Supervision of Transfer of the Government to Dodoma.
Government Press Services.
Investment, Economic Empowerment, Public-Private-Partnership (PPP), Poverty alleviation Policies and their Implementation.
Facilitation of the Development of Informal Sector.
Performance Improvement and Development of Human Resources under this Office
Extra – Ministerial Department, Parastatal Organisations, Agencies, Programmes and Projects under this Office.

REGIONAL ADMINISTRATION AND LOCAL GOVERNMENT:
Decentralization by Devolution (D by D), Rural Development, Urban Development Policies and their Implementation.
Regional Administration.
Primary and Secondary Education Administration
Dar Rapid Transit – DART.
Performance Improvement and Development of Human Resources under this Office.
Extra-Ministerial Departments, Parastatal Organisations, Agencies, Programmes and Projects under this Office.
Mheshimiwa Spika, kitendo cha Serikali hii kuendesha kazi zake kwa Mwongozo wa 2010 ina maanisha kwamba majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu bado ni yale yale yaliyochapishwa mwaka 2010, kwa sababu gazeti hilo la Serikali halijafutwa.

2. UVUNJWAJI WA KATIBA NA SHERIA ZA NCHI KUHUSIANA NA BAJETI UNAOFANYWA NA SERIKALI
Mheshimiwa Spika, hili ni Bunge la Bajeti ambalo kwa mujibu wa ibara ya 63(3)(b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limepewa mamlaka ya kujadili  utekelezaji wa kila Wizara wakati wa Mkutano wa Bunge wa kila mwaaka wa Bajeti kwa madhumuni ya kujadili na kuidhinisha Bajeti ya Serikali.

Mheshimiwa Spika,  Ikiwa fedha zilizoidhinishwa na Bunge hazikutosha kutekeleza majukumu ya Serikali , kifungu cha 41(1) cha  Sheria ya Bajeti ya Mwaka 2015  kinaelekeza kwamba: “ Serikali itawasilisha Bungeni kwa idhini, bajeti ya nyongeza ya fedha zilizotumika ambazo zimezidi kiwango kilichoidhinishwa na Bunge au kwa madhumuni ya kugharamia mahitaji ambayo hayakupangwa”.

Mheshimiwa Spika utaratibu huu unatiliwa nguvu na Sheria ya Fedha za Umma  wa mwaka 2001( Public Finacne Act, 2001)ambapo kifungu cha 18 (3) na (4) kinaitaka Serikali kuleta Bungeni bajeti ya nyongeza ( mini-budget) kwa ajili ya kupata idhini ya Bunge ikiwa fedha zilizoidhinishwa awali hazikutosha.


Mheshimiwa Spika, utaratibu huo wa kisheria  umekuwa ukivunjwa na Serikali kwa  kufanya matumizi ya fedha ambazo hazikuidhinishwa na Bunge jambo ambalo linaua dhana ya madaraka ya Bunge ya kuisimamia na kuishauri Serikali.

Mheshimiwa Spika, ili kuthibitisha jambo hilo, kwa mfano bajeti ya maendeleo iliyokuwa imeidhinishwa na Bunge kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha 2015/16  ilikuwa ni shilingi bilioni 883.8 ambapo kati ya fedha hizo,  fedha za ndani zilikuwa ni shilingi bilioni 191.6

Mheshimiwa Spika, Jambo la kushangaza ni kwamba hadi kufikia mwezi Machi 2016 Wizara ilikuwa imeshapokea kutoka hazina shilingi  bilioni  607.4 ikiwa ni fedha za ndani.

Mheshimiwa Spika, ukitazama takwimu hizo utaona kuwa kuna ongezeko la fedha zilizotolewa na hazina hadi kufikia mwezi Machi 2016 ukilinganisha na fedha zilizoidhinishwa na Bunge. Tangu kuidhinishwa kwa bajeti ya Wizara ya Ujenzi, hakuna bajeti ya nyongeza iliyoletwa Bungeni na Serikali kwa ajili ya kupata idhini  kutokana na matakwa ya Sheria ya Bajeti ya 2015 au sheria ya Fedha ya 2015.

Mheshimiwa Spika, kitendo cha Serikali kuamua kufanya re-allocation ya bajeti bila kupata idhini ya Bunge ni dharau kwa bunge lakini mbaya zaidi ni uvunjaji wa Katiba na Sheria.

3. UHURU NA MADARAKA YA MHIMILI WA BUNGE
Mheshimiwa Spika, Ibara ya 63 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inalitaja Bunge kuwa ndicho chombo kikuu katika Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake. Katika hali isiyo ya kawaida, kifungu hiki cha Katiba kimevunjwa na badala yake Serikali imelipoka bunge madaraka yake na Bunge kwa maana ya uongozi wake wanaonekana kushiriki na kukubali kupokwa huku kwa madaraka na uhuru wake.
 Mheshimiwa Spika, Bunge ni chombo cha uwakilishi wa wananchi, na wananchi wana haki ya kujua Bunge lao linavyofanya kazi ili wawe na uwezo wa kuwawajibisha wawakilishi wao iwapo hawafanyi kazi inavyostahili.  Katika hali isiyo ya kawaida, Serikali na uongozi wa Bunge, imewapoka wananchi haki yao ya kupata habari za Bunge kwa kuzuia mijadala Bungeni kurushwa moja kwa moja na televisheni ya Taifa na vyombo vingine vya habari vya kujitegemea.
Mheshimiwa Spika, Jambo hili pia ni uvunjwaji wa ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo inasema kwamba kila mtu anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake; anayo haki ya kutafuta, kupokea na kutoa habari bila ya kujali mipaka ya nchi; anao uhuru wa kufanya mawasiliano na haki ya kutoingiliwa katika mawasiliano yake na anayo haki ya kupewa taarifa wakati wowote kuhusu matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia kuhusu masuala muhimu kwa jamii,
Mheshimiwa Spika, katika Mazingira kama hayo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni haiko tayari kuendelea kushiriki uvunjaji wa Katiba Sheria na haki za msingi za wananchi.
Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani haitakuwa tayari kuwasilisha hotuba yake katika mazingira haya na inaushauri uongozi wa Bunge kupata ufumbuzi wa haraka wa kadhia hii ili kurejesha heshima ya Bunge na haki za msingi za wananchi. Hivyo basi Kambi bado inatafakari kwa kina na makini hatua za kufuata.
 Mheshimiwa Spika,  naomba kuwasilisha.

Freeman Aikaeli Mbowe (Mb)
KIONGOZI WA UPINZANI BUNGENI NA
MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI
KATIKA OFISI YA WAZIRI MKUU
22 Aprili, 2016.

No comments:

Post a Comment