CUF yamvaa Gavana Ndulu kuhusu hali ya uchumi TZ

Chama cha Wananchi CUF kimeeleza kushangazwa na kauli ya iliyotolewa hivi karibuni na Gavana wa Benki Kuu, Prof Benno Ndulu kuhusu hali ya uchumi nchini, kikieleza kuwa kauli ile haina uhalisia.
Taarifa iliyotolewa leo na chama hicho kwa vyombo vya habari, imeelza kuwa hali ya uchumi haiwezi kuwa nzuri kama watanzania hawana fedha za kutumia huku wakilia kuwa fedha haipatikani.
Taarifa hiyo imedai kuwa uchumi kuwa mzuri maana yake ni watu kuwa na uwezo wa kufanya kazi kwa bidii na kupata fedha za kuhudumia mahitaji ya kila siku na kwamba haiwezekani kwamba watanzania wote walikuwa wakipata pesa kwa njia zisizo halali.
Chama hicho kimepinga hoja ya Gavana Ndulu kuwa wanalalamika kutopata pesa walikuwa wakizipata kwa njia zisizo halali na kwamba ndiyo maana fedha haipatikani kwa vile serikali imebadili mfumo wa ukusanyaji.
Kupitia tamko hilo CUF imemtaka Gavana wa benki kuu Bendo Ndulu kuwa mkweli kwa madai kuwa wananchi wanahitaji fedha za kuendesha maisha.
"Haiwezekani serikali iseme fedha ipo halafu wananchi walalamike fedha haipo. Ni Prof. Benno Ndulu huyuhuyu ndiye mwaka 2008 aliliambia taifa kuwa Tanzania haitaguswa na mtikisiko wa uchumi duniani, miezi michache baadaye taifa likatenga bajeti ya dharura ya takribani TZS Trilioni 2 ili kupambana na mtikisiko mkubwa wa uchumi uliotukumba". Imesema sehemu ya taarifa hiyo
Chama hicho kimeitaka serikali ieleze itafanya nini kuhakikisha kilio cha wanachi cha fedha kukosekana mtaani kinaondoka

No comments:

Post a Comment