SERA ZA CUF KUHUSIANA NA MADAWA YA KULEVYA

Tuwakumbushe hawa Manyumbu na hizi sera za chama makini .
Katika Ilani ya Uchaguzi ya CUF ya mwaka 2015 ambayo ni Dira ya Kuelekea Singapore ya Afrika Mashariki, suala la kupambana na uingizaji na utumiaji wa madawa ya kulevya lilielezwa kwa kina kama ifuatavyo:
Nchi yetu imeathirika sana na biashara ya madawa ya kulevya. Vijana wetu wengi wamejikuta wakiingizwa katika biashara hii pamoja na matumizi yake. Matokeo yake ni kuwepo kwa athari
kubwa ya kiafya, kijamii, kiuchumi na kimaendeleo kutoka katika ngazi ya familia hadi ya taifa. Tutakuwa tunafanya makosa makubwa ikiwa tutaendelea kulichukulia suala hili kama ni la maadili peke yake tu, bali ni suala la usalama mzima wa utaifa wetu na vizazi vyetu vijavyo. Ni wajibu wa
kila mmoja wetu kujtolea kuwasaidia vijana wetu na wale wote walioathirika na janga hili. Lakini pia ni wajibu wetu kuwakaribisha kwa jicho la wema na upendo wale waathirika wote walioweza kupona na wakawa tayari kurejea katika katika ujenzi wa taifa letu.
CUF inaamini kuwa suluhisho endelevu la janga hilo linawea likaja kwa kutumia misingi ya aina tatu:
kuwahudumia waathirika, kutoa elimu bora ya kinga na tiba kwa jamii, na kupambana kwa nguvu zote na wale wote wanaohusika na magendo,
uingizaji na uuzaji wa madawa haya ya kulevya hapa Zanzibar.
Serikali ya Umoja wa Kitaifa itakayoongozwa na CUF itachukua
hatua zifuatazo:
1. Itasimamia kurejeshwa kwa maadili mema ya Wazanzibari kwa kuhuisha mila, silka
na utamaduni wetu na kuwarejeshea Wazanzibari hadhi na fahari yao iliyotokana na mila, silka na utamaduni huo ambao unakataza tabia ovu kama ile ya utumiaji wa madawa ya kulevya.
2. Itapambana vikali na uingizaji na uuzaji wa madawa ya kulevya ambao umekuwa ukiongezeka kwa kasi visiwani Zanzibar kwa kuhakikisha kuwa sheria zinatekelezwa na kusimamiwa ipasavyo ili
kudhibiti marufuku ya uingizaji na uuzaji wa madawa hayo.
3. Itatoa msukumo mkubwa kwa kuanzisha, uviunga mkono na kuviendeleza vituo vya
kuwasaidia waathirika wa madawa hayo ya kulevya ambao wengi wao ni vijana ili
waache utumiaji huo.4. Itatoa elimu kwa jamii kuhusu athari 
za utumiaji wa madawa ya kulevya ili kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo. Itaangalia namna ya kuwasaidia waathirika wa madawa ya kulevya ikiwa ni pamoja na kuwapatia ajira na shughuli
nyengine za kufanya wale walioacha matumizi ya dawa za kulevya.
5. Itahakikisha inashirikiana na wananchi katika ngazi ya Shehia kuandaa mikakati
na mipango ya kupambana na madawa ya kulevya.
6. Itatizama upya mwenendo wa kesi za madawa ya kulevya ili kuona vikwazo vinavyokwamisha kesi hizo.
7. Itaanzisha “one stop center” katika viwanja vya ndege ili anapokamatwa mtuhumiwa wa madawa ya kulevya chunguzi na hukumu vimalizie hapo hapo.

No comments:

Post a Comment