KUTOKA MAHAKAMANI LEO.

KUTOKA MAHAKAMA KUU LEO TAREHE 31/10/2017;

LIPUMBA NA WAJUMBE WAKE WA ‘BODI FEKI YA WADHAMINI’ WAINGIA WOGA JUU YA MAAMUZI YA MAHAKAMA KUU JUU YA UHALALI WAO:

THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF-CHAMA CHA WANANCHI)

TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI
Tarehe 15/10/2017 tulieleza kuwa “MASHAURI YA CUF YANAELEKEA MWISHO MAHAKAMANI: LIPUMBA NA WASHIRIKA WAKE ACHENI VISINGIZIO MAHAKAMA KUU IAMUE” hii inatokana na utaratibu mzuri ambao Mahakama Kuu imejiwekea kumaliza mashauri yalipo Mahakamani Hapo ndani ya wakati muafaka.
Leo Tarehe 31/10/2017 Mheshimiwa Jaji Ndyansobera alipanga kusikilizwa na kutolewa maamuzi baadhi ya mashauri yaliyopo mbele yake na mengine kupangia utaratibu wa kuanza kusikilizwa ili mashauri/kesi hizo zimalizike. Mashauri hayo ni [1] Shauri No. 21/2017, [2]. Shauri No. 80/2017, [3]. Shauri No. 68/2017, [4]. Shauri No. 13/2017, [5]. Shauri No. 28/2017, [6]. Shauri No. 50/2017, [7]. Shauri No. 51/2017. Miongoni mwayo yanahusu Fedha za Ruzuku ya Chama, Bodi ya Wadhamini iliyosajiliwa na RITA, Jinai ya Kugushi Nyaraka nk,

Mashauri hayo yamelazimika Leo kuahirishwa kutokana na barua mbili zilizowasilishwa Mahakamani hapo na Lipumba na Genge lake likidai kupinga Jaji Wilfred Dyansobera kuendelea kusikiliza mashauri hayo na kumtaka AJITOE. Kutokana na hali hiyo,Mheshimiwa Jaji Wilfred Dyansobera amezingatia maelekezo ya Mahakama ya Rufaa katika kushughulikia masuala mfano wa hilo na kuamua wahusika waliosaini barua za malalamiko wapewe fursa ya kusikilizwa kesho Tarehe 1/11/2017, ili Mahakama ipime hoja zao na kuyatolea uamuzi. Hata hivyo wakili wa Lipumba Mashaka Ngole aliomba kusogeza mbele ili waweze kwenda kujipanga vizuri na wateja wake na kuwaleta Mahakamani kusikilizwa. Mahakama imepanga kuwasikiliza Tarehe 13/11/2017.

Katika hatua nyingine ya usikilizaji wa mashauri hayo Wakili wa Lipumba na Genge lake Mashaka  Ngole na Hosea Chamba walijenga zisizo na mashiko ya kisheria walipotaka Mahakama iondoe majibizano ya kimaandishi (Written Submissions) zilizowasilishwa na Wakili Msomi Mheshimiwa Mpale Kabe Mpoki kwa niaba ya Mhe Ally Salehe kwa madai ya kosa la kimaandishi katika namba za shauri hilo. Suala ambalo linarekebishika kwa mwasilishaji kuiomba Mahakama chini ya kifungu cha 97 cha sheria ya mwenendo wa Makosa ya Jinai. Mwanasheria Mkuu wa Serikali Wakili Msomi Mheshimiwa Gabriel Malata alitoa ufafanuzi wa kisheria uliosapotiwa kisheria na Mawakili Wasomi wa CUF-Chama cha Wananchi Mheshimiwa Juma Nassor,  Mheshimiwa Daimu Halfani, Mheshimiwa Hashim Mziray na Mheshimiwa Lovenes Denis,  Mahakama ikazingatia ufafanuzi huo na kuridhia marekebisho ili kuweka kumbukumbu za Mahakama vizuri.  Aidha, Shauri No.  51/2017 lilishapangwa tangu awali kutajwa Tarehe 7/11/2017 na Mashauri mengine yote yatatajwa tena Tarehe 24/11/2017 siku ambayo pia Mheshimiwa Jaji Atafanyia maamuzi juu ya Hoja za waliowasilisha barua za kumtaka ajitoe.

WAKILI WA LIPUMBA NA AFISA WA OFISI YA MSAJILI SISTY NYAHOZA WACHANGANYIKIWA:

Kutokana na maamuzi hayo Wakili Mashaka Ngole na Sisty Nyahoza wameondoka mahakamani hapo wakiwa hoi vichwa vimevurugika kutokana na mambo kutokwenda kama walivyotarajia huku Ruzuku ya Chama ikiendelea kuzuiliwa kwa AMRI YA MAHAKAMA. Suala la Kugushi Nyaraka na mengi mengineyo yamewaweka katika mazingira ya khofu kubwa na hatimaye kuibuka na hoja za Kumtaka Jaji Ndyansobera Ajitoe na kuomba Jaji Mstaafu Kihiyo ikiwezekana arejeshwe.

Huku ni kupoteza muda na kutaka kuchelewesha maamuzi ya MAHAKAMA KUU. Sisty Nyahoza alionekana amewahi kufika Mahakamani hapo mapema sana asubuhi na kuvinjari katika ofisi mbalimbali za Mahakama bila mafanikio ya alichokitarajia. wanaCUF waliohudhuria Mahakamani hapo wamekuwa wakihoji Ofisi ya Msajili inanufaika nini na kupata maslahi yepi kwa namna ya Juhudi hizi wanazozifanya kutaka kupindisha HAKI YA TAASISI YA CUF.

MAPAMBANO YA KISHERIA YAMEFIKIA HATUA NZURI YA MWISHO NA hatuna budi kuwapongeza Wasomi Mawakili wetu (The Learned Advocates) wote kwa jitihada kubwa wanazozichukua kuhakikisha kuwa Mashauri haya yanasikilizwa na kumalizwa ndani ya wakati muafaka na HAKI KUREJESHWA KWA TAASISI YA CUF. Tunatoa wito kwa wanachama na watanzania wote wapenda Mabadiliko kuendelea kuwa na subira, WASALITI na VIBARAKA wote watarejea kwa wanaomtumikia na kuiacha CUF ikiwa SALAMA na NGANGARI zaidi.

CUF NI TAASISI IMARA, YENYE VIONGOZI MAKINI.
HAKI SAWA KWA WOTE

Imetolewa leo Tarehe 31/10/2017
Na. Kurugenzi ya Habari, Uenezi Na Mahusiano Na Umma-CUF Taifa

SALIM BIMANI
MKURUGENZI
Zantel +255 777 414112 / Tigo +255 655 314112

MBARALA MAHARAGANDE
NAIBU MKURUGENZI
Phone No. 062577 Tigo Code-+255 715 / Zantel Code - +255 773 / Voda Code- +255 767
maharagande@gmail.com

No comments:

Post a Comment