CUF WACHAGUA BARAZA KUU
BARAZA KUU LA UONGOZI TAIFA LA CUF, LAKUTANA NA KUJAZA NAFASI WAZI ZA WAJUMBE WA BODI YA WADHAMINI; THE CIVIC UNITED FRONT (CUF-CHAMA CHA WANANCHI) TAARIFA KWA UMMA TAREHE 19 FEBRUARY, 2019 TAARIFA KWA UMMA WAJUMBE WA BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA LA THE CIVIC UNITED FRONT [CUF-CHAMA CHA WANANCHI] wamekutana leo Tarehe 19/2/2019 katika kikao chake kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya CUF, Magomeni-Dar es Salaam. Kikao hicho kilichohudhuriwa na Mheshimiwa Bonifance Jacob (Afisa kutoka Mamlaka ya Serikali-Government Authority, kwa mujibu wa matakwa ya Sheria ya The Trustees incorporation Act. CAP 318 RE: 2002 Section 17(1)] na pia kikao hicho kilimualika Mheshimiwa James Francis Mbatia (Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania-TCD). Kikao kilikuwa na Ajenda Moja pekee ambayo ni KUJAZA NAFASI WAZI ZA WAJUMBE WA BODI YA WADHAMINI YA CUF. Wajumbe 37 walihudhuria kati ya wajumbe wote 63 kama wangekuwepo kama walivyochaguliwa na Mkutano Mkuu wa Taifa mwaka 2014. Na hivyo kufanya kupatikana (koramu) ya zaidi ya nusu ya wajumbe halali waliopaswa kuhudhuria kikao hicho. Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kwa mujibu wa Katiba ya CUF 1992[Toleo 2014] Ibara ya 98(1) na (2) imewateua wanachama wa CUF wafuatao
KUJAZA NAFASI NA KUWA WAJUMBE WA BODI YA WADHAMINI YA THE CIVIC UNITED FRONT [CUF-CHAMA CHA WANANCHI]. WALIOTEULIWA NI;
1. ABDALLAH SAID KHATAU-(ME)
2. ALI MBARAKA SULEIMAN-(ME)
3. YOHANA MBELWA-(ME)
4. MOHAMED NASSOR MOHAMED-(ME)
5. DR. JUMA AMEIR MUCHI-(ME)
6. ZUMBA SHOMARI KIPANDUKA-(ME)
7. MWANAWETU SAID ZARAFI-(KE)
8. MWANA MASOUD ALI-(KE)
9. BLANDINA OBAS MWASABWITE-(KE)
HAKI SAWA KWA WOTE SALIM BIMANI MKURUGENZI HABARI. +255 777414112 +255 655314112
No comments:
Post a Comment