Muhimili wa mwisho wa Dola uliowasaliti WATANZANIA

KUTOTIIWA KWA AMRI YA MAHAKAMA KUU KULIKOFANYWA NA LIPUMBA NA GENGE LAKE, NINI KIFANYIKE:

THE CIVIC UNITED FRONT
[CUF-CHAMA CHA WANANCHI]

TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI:

TAREHE 4/12/2018 MAHAKAMA KUU KANDA YA DAR ES SALAAM MBELE ya Mheshimiwa Jaji DKT BENHAJJ MASOUD imetoa AMRI YA KUHIFADHI HALI ILIYOKUWEPO WAKATI HUO [Maintenance of Status Quo] KWA KUZUIA KUFANYIKA KWA MKUTANO MKUU ‘FEKI’ ULIOPANGWA KUITISHWA NA LIPUMBA NA GENGE LAKE. Katika shauri dogo Namba 40/2018 lililotokana na shauri la Msingi Namba 23/2016 linalotarajiwa kutolewa HUKUMU kesho Jumatatu Tarehe 18/3/2019.

Mheshimiwa Jaji Benhajj alisema “…anasitisha utoaji wa uamuzi wa maombi ya shauri hilo Namba 40/2018 isipokuwa hali iliyopo sasa ibaki hivyo hivyo (KUSIFANYIKE MKUTANO MKUU)  *to maintain status quo* kwa sababu mashauri haya yanaingiliana na kuhitajika kutolewa Uamuzi kwa pamoja…” Court Records zinasomeka hivyo na maamuzi haya yalitolewa mbele ya Wakili wa Lipumba Mashaka Ngole.

ILIKUWAJE:

Karani ameliita Shauri Civil Application No. 40/2018 Mawakili wote wakajitambulisha. Jaji akasema *“sitotoa UAMUZI leo. Mashauri haya yanayohusu CUF ikiwemo lile dhidi ya Msajili na lile linalohusu RITA yanaingiliana.* akaendelea kusema *Ni vyema yakaamuliwa pamoja.*

Jaji akauliza; *Mkutano Mkuu si haujafanyika?*
Mashaka Ngole akajibu,

*Ndio Mheshimiwa Jaji haujafanyika*

Jaji akamalizia kwa kusema : *“I Order to Maintain Status Quo”.*
Baada ya maneno hayo ya Mhe Jaji Mawakili wakainuka wakasema “…Much obliged” kisha karani akaliita Shauri lingine kuhusu RITA, ushahidi ukaanza kusikilizwa.

“Status Quo: law and legal definition: Status Quo generally refers to the existing state of affairs or circumstances. a Status Quo order may be issued by a Judge to prevent ANY OF THE PARTIES INVOLVED IN DISPUTE FROM TAKING ANY ACTION UNTIL THE MATTER CAN BE RESOLVED. it seeks to prevent harm or preserve the existing conditions, so that a party's position isn't prejudiced in the meantime until a resolution is reached.

"In Statu Quo" – Which itself is a shortening of the original phrase In Statu Quo Res Erant Ante Bellum, meaning "in the state in which things were before the war". TO MAINTAIN THE STATUS QUO IS TO KEEP THE THINGS THE WAY THEY PRESENTLY ARE.

Mkutano Mkuu haujafanyika HALI ibaki hivyo mpaka kesi aya msingi itakapo kwisha ndio maana ya Amri/Order iliyotolewa na Mahakama Kuu.

Hii ni AMRI ya kwanza kutolewa mbali na ile ya Pili iliyotolewa na Jaji Stephen Magoiga tarehe 28/2/2019

Lipumba na genge lake wamevunja AMRI ZOTE HIZO MBILI.

KESI NI YA MAHAKAMA KUU DHIDI YA LIPUMBA NA GENGE LAKE. Tunachopaswa kufanya ni “to move the court, to switch on the issue before the court”.

KESHO JUMATATU TAREHE 18/03/2019 MAHAKAMA KUU KANDA YA DARE ES SALAAM MBELE YA MHESHIMIWA JAJI DKT. BENHAJJ MASOUD, Inatarajia kutoa JUDGMENT katika shauri Namba 23/2016 UHALALI WA LIPUMBA NDANI YA CUF.

UAMUZI HUO UNAWEZA KUTOA MUELEKEO NA HATMA YA LIPUMBA NDANI YA CUF NA KUFUTA NA KUBATILISHA (NULLIFY) MAMBO YOTE YALIYOFANYWA NA LIPUMBA NA GENGE LAKE TANGU WAKATI HUO MPAKA HIVI SASA.

Kukimbilia kufanya Mkutano Mkuu na kuchagua viongozi na yote yaliyofanyika ni kama mathalani “muumini kaoga josho la Janaba, akachukua udhu, akaingia msalani akajisaidia haja kubwa na ndogo, akatoka na kwenda kuswali salatul Dhuhri. Je swala hiyo inajuzu kwa mujibu wa shurti za swala?” jibu swala ni batili kwa kuwa hajatawadha alipotoka Chooni.

KAMWE HARAMU HAIZAI HALALI. MKUTANO HARAMU, UCHAGUZI HARAMU, MATOKEO HARAMU, VIONGOZI HARAMU, UONGOZI HARAMU, UTENDAJI HARAMU, MAAMUZI HARAMU.

TUKUTANE KESHO SAA 3 ASUBUHI MAHAKAMA KUU.

HAKI SAWA KWA WOTE

Imetolewa LEO Tarehe 17/2/2019 na Kurugenzi ya Habari;

MBARALA MAHARAGANDE
K/NAIBU MKURUGENZI HABARI, UENEZI NA MAHUSIANO NA UMMA CUF TAIFA.

maharagande@gmail.com

+255 715 062 577
+255 767 062 577

No comments:

Post a Comment