Headlines News :
KARIBU CUF DIASPORA NETWORK - CUF HAKI SAWA KWA WOTE...TEGEMEA KILA JIPYA NA ZURI KUTOKA KWETU...LIKE PAGE YETU KWENYE FACEBOOK
Home » , » CHAMA CHA Wananchi CUF kimesikitishwa kwa kudai kuwa kitendo cha Jeshi la Polisi kuwateka viongozi wa chama hicho takribani 20 mkoani Pwani.

CHAMA CHA Wananchi CUF kimesikitishwa kwa kudai kuwa kitendo cha Jeshi la Polisi kuwateka viongozi wa chama hicho takribani 20 mkoani Pwani.



Naibu Katibu Mkuu Uenezi Jumuiya ya Vijana Chama cha Wananchi CUF Mohamed Mahmoud Mahinda amedai hayo leo kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Facebook kuwa viongozi wa CUF katika maeneo ya Kibiti, Ikiwiri na Rufiji wametekwa na jeshi hilo na kupelekwa mahala pasipo julikana.

Kibiti, ikwiriri na rufiji itazamwe kwa jicho pana na la huruma!! #jeshi la polisi linawateka na kuwatesa viongozi wa cuf kwa faida ya nani??” Amehoji.
Kiongozi huyo amesema kuwa chama hicho kimekuwa mstari wa mbele kuhimiza, kuhamasisha na kulinda amani ya nchi, na kuiunga serikali vitendo vya kihalifu vya aina yoyote ile ni haramu katika chama cha cuf.
“Tunaposema jeshi la polisi na vyombo vyengine vya dola, vitumie uweledi katika kuwasaka na kuwakamata "wahalifu" tuna maanisha yoyote alie mhalifu achukuliwe hatua za kisheria kama zinavyopaswa kuchukuliwa bila ya kujali itikadi wala muelekeo wa KISIASA, DINI WALA KABILA, Maana UOVU hauna kabila, Dini wala itikadi ya kisiasa” Amefafanua.

Hali kadhalika amesema kitendo hicho cha Jeshi la Polisi kimewasikitisha juu ya yanayoendelea kufanywa Kibiti dhidi ya viongozi wa CUF kwani vimeanza kutoa ishara mbaya na kuonesha kuwa Jeshi la Polisi, kukosa uwezo wa kutosha katika kuwabaini waovu.

“ Jeshi la polii na vyombo vya dola wamekubali kuweka pembeni taaluma zao na kukubali kutumika kwa kuwaridhisha viongozi wa chama tawala. nasema haya nikimaanisha kwamba, haiyumkiniki uwateke viongozi wa cuf zaidi ya 20, uwapeleke kusikojulikana, (kinyume na sheria) uwatese "kinyama" uwadhalilishe utu wao kisha uwaachie warudi makwao wakiwa wahoi bin taaban!! kutokana na mateso walioyapata kutoka kwenye vyombo vinavyotegemewa kusimamia sheria za nchi yetu, kulinda raia na mali zao (bila ya ubaguzi wa aina yoyote). ni aibu na fedheha kubwa, unapoona jeshi la polisi na vyombo vya dola, vinawaaminisha raia kuwa vinapambana na uhalifu, huku wao wakiongoza, au wakifanya zaidi ya uhalifu (MATESO YA KINYAMA) dhidi ya Raia wasio na "HATIA"” Amebainisha Mahinda.
Kwa upande wa Kamanda mkuu wa Mkoa wa Pwani mara alipopigiwa simu leo na muandishi wa habari hizi majira ya saa kumi na moja jioni amesema hayupo tayari kuongelea suala hilo na hana taarifa kwani uongozi wa Jeshi la Polisi haujampa taarifa yoyote.

Kamanda huyo aliyeonekana hayupo tayari kuzungumza lolote, na kusema anafuatilia tuuhuma hizo licha ya kudai kuwa waandishi wengi wa habari leo wamempigia kutaka kujua ukweli wa tuhuma hizo.
Share this article :

No comments:

Post a Comment

 
Support : ZENJIBARZA
Copyright © 2011. ACT WAZALENDO DIASPORA NETWORK - All Rights Reserved