The
Civic United Front (CUF- Chama cha Wananchi). CUF ni chama cha
uliberali wa kidemokrasia ambacho kauli mbiu yake ni Haki Sawa kwa Wote.
CUF inasimamia elimu bora, afya madhubuti, mfumo adilifu wa kodi,
Muungano wa haki, siasa kuwa utumishi ulioutukuka kwa umma na fursa sawa
katika kujiendeleza kiuchumi, kijamii na kisiasa.
HAKI SAWA KWA WOTE
Kaulimbiu
ya Haki Sawa kwa Wote inalenga visheni ya CUF ya jamii tuitakayo. Hiyo
ni jamii yenye wananchi wanaopendana, kuheshimiana, kuhurumiana, na
wanaochukia
Mwenyekiti wa muda wa CUF Julius Mtatiro.
uonevu, ukandamizaji na ubaguzi. Msingi Mkuu wa CUF ni haki za binaadamu na demokrasia na hivyo suala la usawa lina nafasi ya pekee katika kuijenga jamii inayokusudiwa na Chama chetu.
Mwenyekiti wa muda wa CUF Julius Mtatiro.
uonevu, ukandamizaji na ubaguzi. Msingi Mkuu wa CUF ni haki za binaadamu na demokrasia na hivyo suala la usawa lina nafasi ya pekee katika kuijenga jamii inayokusudiwa na Chama chetu.
Azma
ni kujenga jamii ambayo itahakikisha inapiga vita ubaguzi wa kila aina
na ambayo itahakikisha kila mwananchi anathaminiwa utu wake, na ana haki
na fursa sawa katika nyanja zote za maisha yake.
Lengo ni kujenga jamii ya demokrasia ya kweli na yenye kuongozwa na utawala wa sheria na Serikali nzuri (good governance), ambayo msingi wake ni kuwekwa madarakani na wananchi wenyewe.
Shabaha, Malengo na Madhumuni makuu ya CUF yameelezwa kwa urefu katika Katiba yake.
Lakini kwa ufupi Shabaha kuu ya CUF ni kuona kwamba nchi yetu na
wananchi wake wote wamepata uhuru wa kweli na kujigomboa na mapepe
yaliyobaki baada ya ukoloni mkongwe kuondoka na, pia, kujikinga na
athari za ukoloni mamboleo. CUF inakusudia kuhakikisha kwamba uwezo wa
kuiongoza nchi na wa kutoa maamuzi mazito ya mambo makubwa ya Taifa uko
mikononi mwa Watanzania wenyewe.
CUF
siku zote itaongoza juhudi za wananchi zenye kuelekezwa katika kuiletea
nchi yetu ukombozi wa kiuchumi. CUF itatilia maanani umuhimu wa
rasilmali za nchi yetu kuwanufaisha wananchi wenyewe. Katika kufikia
lengo hilo CUF itakuwa na uangalifu mkubwa katika kuwashirikisha wageni
wenye uwezo wa fedha na teknolojia. Wimbo wa Taifa wa CUF unasema hivi:
Ni haki sawa kwa watu wote, kuendeleza taifa letuUtajirisho itikadi yetu, tukatae kuonewa.Siasa itumikie, uchumi wa Nchi yetuNi mwiko huo uchumi, kutumikia siasa
Wimbo huu unabeba mantiki nzima ya itikadi, falsafa na sera za CUF.
ITIKADI YA ULIBERALI
Itikadi kuu ya Chama cha Wananchi (CUF) ni Uliberali ambayo
inalenga kuwazindua wananchi waweze kuitumia neema waliyopewa na
Mwenyezi Mungu kwa manufaa yao binafsi na Taifa kwa ujumla. CUF inaamini
kuwa Tanzania ni nchi tajiri kwa rasilimali na watu, lakini imefanywa
kuwa masikini kwa kukoseshwa uongozi wenye sera na mtazamo (dira) wa
kimaendeleo.
Inaposema
Tanzania ina neema, CUF inakusudia uwezo wa akili na nguvu pamoja na
utajiri wa asili tulinao. Nchi hii inao utajiri mkubwa wa ardhi ifaayo
kwa kuzalisha mazao ya aina mbalimbali na inao utajiri mkubwa wa maji ya
mito maziwa na bahari.
Itikadi
ya Utajirisho inamhamasisha mwananchi ili aweze kuutumia ipasavyo
utajiri wetu wa ardhi, bahari na madini ya thamani kama dhahabu, almasi,
gesi, na tanzanite.
Kuhusu siasa, CUF
kinasimama kama chama halisi na makini cha kisiasa kinachotumia siasa
kwa maana yake halisi kufanya siasa kufikia malengo na dhamira yake kwa
njia za kisiasa. CUF inasisitiza kuwa siasa si mchezo mchafu, ingawa
inafahamu kwamba CCM imezifanya siasa zionekane hivyo kutokana na
viongozi wake kuiharibu siasa kutokana na ulaghai wao kwa Watanzania.
Kwa hivyo, mwelekeo wa siasa ya Chama Cha Wananchi ni kuwaelimisha na
kuwaandaa wana-CUF na Watanzania wote katika kutoa utumishi wa
kuridhisha kwa wananchi ili kurudisha hadhi na heshima ya siasa kama
utumishi uliotukuka kwa umma.
Kuhusu mamlaka ya dola, CUF
inaamini kwamba Serikali ndiyo dola na kwamba mamlaka yake yanapatikana
kutokana na ridhaa ya wananchi kwa kufanyika uchaguzi ulio halali na
huru na Serikali hiyo lazima iweajibike huko huko kwa wananchi. Kwa
mujibu wa Itikadi hii, Serikali itakayoundwa na CUF lazima iwajibike kwa
wananchi. Ndani ya Serikali ya CUF, kwa hivyo, hakutokuwa na nafasi ya
walaghai wachache kuendesha mambo kwa ujanja, ufisadi na utapeli kama
ambao umekuwa ukitekelezwa na viongozi wa serikali za CCM.
Kwenye uchumi na maendeleo, CUF
inakusudia kujenga uchumi ulio imara kwa kuanzisha taratibu za kiuchumi
zainazowashawishi kwa kadiri ya uwezo wao na kuchangia Taifa kwa ziada
wapatayo. Mtazamo wa CUF kijumla ni wa kiliberali, kwa hivyo uhuru wa
mtu binafsi kujiendeleza na kutumia fursa zilizopo kujinufaisha na
kulinufaisha Taifa.
Kuhusu ardhi, CUF
inachukulia kuwa ni mali ya watu wote, hivyo Serikali ya CUF itasimamia
matumizi yake kwa uangalifu mkubwa. Ardhi itamilikiwa na wananchi
wenyewe au Serikali yao. Kwa hivyo, ingawa CUF inakaribisha uwekezaji
rasilimali kutoka nje, lakini Serikali yake haitomilikisha ardhi kwa
wageni. Iwapo mwekezaji anahitaji ardhi kwa ujenzi wa kiwanda, kuendesha
shughuli za kilimo au kuendeshea shughuli nyinginezo, mwekezaji huyo
atawajibika kuingia ubia na mwananchi ambaye ndie atakayemilikishwa
ardhi inayohitajika.
Kuhusu elimu,
CUF imekusudia kutoa elimu ya darasa la kwanza hadi la kumi na mbili
bure katika mashule yenye vifaa na walimu wenye sifa ya kufanya kazi
hiyo wala sio katika hali ya sasa ambapo shule zilizopo hazina vifaa vya
kutosha wala walimu wenye sifa hasa za kuwa walimu. CUF inaamini kwa
elimu ndio msingi wa ujenzi wa taifa na kwamba taifa lisilo na watu
walioelimika haliwezi kwenda mbele. Kusoma na kuelimika ni haki ya kila
mwananchi na CUF inakusudia kuilinda na kuigawa haki hiyo kwa wenyewe,
wananchi.
Kama ilivyo elimu, CUF inaamini kuwa afya nayo
ni haki ya msingi ya kibinaadamu. Kwa hivyo, inakusudia kuboresha
huduma za kinga pamoja na zile za tiba. Katika kulifanikisha hili, CUF
itahakikisha kuwa mahospitali yaliyopo yanapatiwa vifaa bora pamoja na
kuzingatia mafunzo kwa wafanyakazi.
Kuhusu umeme na maji, CUF inasisitiza kuwa kulingana na umuhimu wa huduma hizi kwa uhai na uchumi, Serikali yake itahakikisha kuwa wananchi wanapatiwa maji pale walipo na kunakuwepo umeme wa uhakika katika sehemu zote zilizokubalika kupata huduma hiyo.Kwenye nyanja ya wafanyakazi, Serikali ya CUF inakusudia kupanga pato la mfanyakazi kwa saa wala sio kwa mwezi. Utaratibu huu ni wenye manufaa kwa pande zote mbili, wakati mfanyakazi anajitahidi kufanyakazi kwa masaa mengi ili ajipatie donge nono, mwajiri ananufaika kwa kulipa kulingana na kazi iliyofanywa.
Kwenye ushuru, Serikali
ya CUF itahakikisha kwamba baadhi ya ushuru unaokusanywa na Serikali
Kuu unahamishiwa Serikali za Mitaa na Serikali hizi zinakuwa bunifu.
Juu ya mabenki na huduma za fedha,
Serikali ya CUF inakusudia kurekebisha mfumo wa uendeshaji wa Mabenki
hapa nchini. Katika mabadiliko hayo, mabenki na taasisi nyingine za
kifedha zitajiendesha kibiashara huku zikizingatia kutoa fursa ya
kuwahudumia wananchi wote kwa kuondoa masharti yanayokwamisha wananchi
wa kawaida kunufaika na huduma hiyo.
Kilimo kitapewa
umuhimu mkubwa na wakulima wananchi watasaidiwa kuboresha njia zao za
ukulima. Kwa sababu ardhi ndio rasilmali kuu ya nchi yetu basi ni wajibu
wetu kuhakikisha kwamba ardhi yetu inatumika vyema.
Hivyo
watumiaji wote wa ardhi watashawishiwa na kuelimishwa juu ya matumizi
bora ya ardhi ili ardhi itoe mazao bora na mengi na wakati huo huo
kuwahakikishia wakulima bei nzuri za mazao yao ili zilingane na juhudi
zao na ubora wa mazao yao. Nia ni kuwafanya wananchi wawe na maisha
mazuri kutokama na rasilmali ya nchi na juhudi zao.
Sekta za viwanda na madini zitapewa
mwelekeo mpya ambao utakidhi hali halisi na ambao utatawaliwa na
matumizi sahihi ya sayansi na teknolojia na sekta hizi zitaongozwa na
wataalamu waliofunzwa na kufunzika, zitapata usimamizi wa makini na
zitafanywa ziweze kuzalisha bidhaa zinazokidhi mahitaji ya masoko ya
kimataifa ili bidhaa hizo ziweze kuuzika kwa urahisi.
Na kwenye suala la muhimu kwa uhai wa Taifa hili kama taifa, yaani Muungano,
CUF inatambua umuhimu wa Muungano uliopo baina ya Tanganyika na
Zanzibar bali inataka pawepo na Muungano wa ukweli unaozingatia maslahi
ya wananchi wote.
Kwa mfano, kwa mujibu wa Makubaliano ya Muungano (Articles of Union),
Rais wa Zanzibar anakuwa mmoja wa Makamo wawili wa Rais, na hivyo CUF
inayachukulia Mabadiliko ya 11 ya Katiba ya Muungano kama ukiukwaji
mkubwa wa Mkataba wa Muungano, na ambao unavunja misingi ya Muungano
wenyewe. Sera ya CUF kuelekea Muundo wa Muungano ni Serikali Tatu, yaani
ile ya Zanzibar, ya Tanganyika na nyengine ndogo ya Muungano.
Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Diaspora Ismail Jussa Ladhu
Dira
hii ya CUF inaweza kufanywa kuwa hai ikiwa kila Mtanzania ataungana na
CUF kuihuisha. Jiunge sasa na ukombozi, saa ndiyo hii.
HAKI SAWA KWA WOTE
No comments:
Post a Comment