MAMILIONI ya shilingi ndani ya ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa yaliyotengwa kwa ajili ya kuwajengea uwezo wanawake ndani ya vyama vya siasa nchini, hayakujulikana yalipo.
“Ama mamilioni hayo yamekwapuliwa au yametumika isibvyopasa”,.
Taarifa kutoka ndani ya Msajili wa Vyama vya Siasa zinasema, mamilioni hayo ya shilingi yaliingizwa katika akaunti ya Msajili katika benki lakini sasa hayajulikani yalipo au yalivyotumika.
Mmoja ya maofisa waandamizi ndani ya ofisi ya waziri mkuu ameliambia gazeti hili kuwa tayari uchunguzi umeanza ili kufahamu jinsi fedha hizo zilivyotumika.Mtoa taarifa huyo anasema, “kuyeyuka” kwa fedha hizo kuligunduliwa na mkaguzi wa ndani wa ofisi hiyo.
Amesema, “ofisi ya msajili ilipokea Sh. 600 milioni ili zitumikekujengea uwezo wanawake ndani ya vyama vya siasa; lakini kazi hiyo haijafanyika”.
Amesema, “…..baada ya kubaini kutokuwepo fedha hizo au ushahidi wa matumizi yake, ndipo ikaagizwa ufanyike ukaguzi maalum ili upatike uhakika wa kile kilichoonwa na mkaguzi wa ndani”.
mwanaHALISI lilipomuuliza Jaji Francis Mutungi juu ya madai ya kupotea kwa mamilioni hayo ya shilingi, alikiri kuwepo ukaguzi katika ofisi yake kuhusiana na upotevu wa fedha hizo.
“N kweli ukaguzi unafanyika…… Ni kweli pia kwamba kuna ukaguzi maalum unaofanyika nab ado unaendelea,” alisema.
Alipoulizwa ukaguzi unafanywa na nani, Jaji Mutungi alijibu haraka, “…unafanywa na mkaguzi wa ndani”.Alipoelezwa kuwa gazeti hili linazo taarifa kuwa ukaguzi huo unafanywa na ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) na unafanyika baada ya makguzi wa ndani kugundua kuwepo kwa upotevu wa mamilioni hayo ya shilingi, Jali Mutungi alisema, “kwa kuwa jambo lenyewe lipo katika uchunguzi, nakuomba msubiri likamilike”.Alisema “siwezi kuzungumza kwa wakati huu. Jambo hili bado liko katika uchunguzi. Nakuomba subiri taarifa ya uchunguzi; naamini mtapata ukweli uliokamilika kiliko kuanza kutafuta jambo hili hivi sasa”.
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ndio pia husimamia malipo ya ruzuku kwa vyama vya siasa nchini.
Hivi karibuni kumekuwa na mvutano miongoni mwa ofisi ya Msajili, Chama cha Wananchi CUF upande unaomkubali Katibu Mkuu Maalim Seif na upande unaomkubali Prof. Ibrahim Lipumba anaedai kuwa mwenyekiti wa chama hicho.
Mvutano unatokana na madai kuwa Jaji Mutungi amemchotea Prof. Lipumba zaidi ya Sh. 369 milioni kutoks ruzuku ya CUF.
Inadaiwa mamilioni hayo ya shilingi kutoka kwa Msajili yaliingizwa katika akaunti Na. 2072300456 iliyoko benki ya National Microfinance Bank (NMB), tawi la Temeke.
Akaunti hii siyo ya CUF bali imeonyesha kuwa inamilikiwa na wanaojiita wanachama wa CUF kutoka wilaya ya Temeke.
Tayari katibu mkuu wa CUF, Maalim seif Shariff Hamad, amenukuliwa akisema, akaunti iliyotumika kupitishiwa fedha hizo, siyo mali ya baraza la wadhamini.
Prof.Lipumba ambaye alijiuzulu uenyekiti kwa hiari kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa oktobar 2015, alifukuzwa uwanachama wa chama hicho, Septemba mwaka jana na Baraza kuu la Uongozi la Taifa, lililokuta mjini Zanzibar.
Alituhumiwa kwa usaliti, ugombanishi, kukichonganisha CUF na vyama vingine vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), kwa lengo la kuvuruga na kukubali kutumiwa na wabaya wa chama hicho.
Amerejeshiwa uwenyekiti wake na Jaji Mutungi, kinyume cha sheria inayounda Baraza la Wadhamini ndani ya vyama vya siasa na katiba ya CUF.
Wengine waliovuliwa uwanachama na Lipumba kwa makosa hayohayo, ni pamoja na Magnalena Sakaya, aliyekuwa naibu katibu mkuu Bara na mbunge wa Kaliua, mkoani Tabora.
Mamilioni ya shilingi ya CUF yalitoroshwa kwa msaada wa Jaji Mutungi,Alhamisi ya 5 januari 2017, “bila idhini ya katibu mkuu wa chama hicho wala bodi ya Wadhamini.”
Kwa mujibu wa sheria na. 5 ya vyama vya siasa, baraza la wadhamini ndio msimamizi mkuu wa fedha na mali za vyama vya siasa.
Baraza kuu la uongozi la CUF, taarifa zinasema, halijawahi kupitisha maamuzi yoyote juu ya fedha hizo tangu Jaji Mutungi akiarifu juu ya uamuzi wake wa kuzuiya ruzuku yake.
Katika barua yake kwa Prof. Lipumba na Maalim Seif, Jaji Mutungi amesema, ameamua kusimamisha ruzuku ya chama hicho kwa kuhofia usimamizi wa matumizi yake wakati huu ambako anadai “chama hicho kinakabiliwa na mgogoro”.
Tuhuma za kuchotwa kinyemela kwa fedha za ruzuku ya CUF zinamuangukia moja kwa moja Jaji Mutungi.
Jaji Mutungi hakuweza kujibu madai mengine juu ya hatua yake ya kumkabidhi Prof. Lipumba kama inaendana na utawala bora na mambo mengine kadhaa yanayohusu ofisi yake nay eye binafsi.
Mwandishi wa gazeti hili alifika ofisini mwa msajili, wiki mbili zilizopita na kuwasilisha maswali yake. Baadhi ya maswali hayo, yalijibiwa na mengine alitaka mwandishi kumpa nafasi ya kuandalia majibu. Alimuahidi mwandishi kufika ofisini kwake Ijumaa – tarehe 13 January 2017.
Mwandishi alifika ofisini kwa msajili kama alivyoahidiwa. Lakini mwandishi hakuweza kupata majibu aliyoahidiwa. Alimtaka kufika tena Jumanne iliyopita ili kumpa majibu.
Mwandishi alifika tena Jumanne kama ambavyo masajili ameelekeza. Lakini kinume na makubaliano hayo, Jaji Mutungi alijibu baadhi ya maswali .
MwanaHALISI linaendelea kufuatilia baadhi ya majibu ya maswali ambayo Jaji Mutungi amegoma kujibu.
Awali Jaji Mutungi alitetea uamuzi wake wa kutoa fedha za ruzuku kwa Prof. Lipumba akidai kuwa hakuna mahali ambako utaratibu utaratibu umekiukwa.
“Fedha hizi zimetolewa kwa kufuata taratibu zote za kisheria. Wala hakuna ambako taratibu zimekiukwa,” ameeleza.
Hajaeleza ni lini alitengua barua yake ya kusitihsa ruzuku. Ametoa fedha hizo bila kueleza kwa uwazi ni lini alikutana na makundi anayodai yanayosigana ndani ya chama hicho, kama alivyodai katika maelezo yake alitoa wakati anatanga kuzuia ruzuku.
Kwa mujibu wa kifungu cha 21 (1) cha sheria ya vyama vya siasa, kila chama chenye usajili wa kudumu kinatakiwa kuteuliwa bodi ya wadhamini, itakayosimamia na kumiliki mali zote za chama, biashara pamoja na vitega uchumi.
Aidha, kifungu cha 21 (2) kinataka kila chama kilichopata usajili wa kudumu, kupeleka ndani ya siku 60, majina na anuani za wajumbe wa bodi na cheti cha usajili wa wajumbe kwa msajili wa nyama vya siasa.
Vilevile, kifungu cha 21 (A) kinamtaka msajili wa vyama, ndani ya kipindi cha miezi mitatu, baada ya kupokea majina, anuani na kivuli cha cheti cha usajili wa bodi ya wadhamini kutoka Kabidhi Wasihi Mkuu wa Serikali (Administrator General), ofisi yake kuitambua bodi hiyo.
Bodi ya Wadhamini CUF inatajwa kwenye kifungu cha 98 (1) cha katiba ya chama hicho, toleo la mwaka 2014.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
- TAMKO LA UMOJA WA KLABU ZA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA JUU YA KUTEKWA KWA MWANDISHI WA HABARI WA SAUTI YA UJERUMANI ( DW ) SALMA SAID.
- CUF wamuandikia barua Mwenyekiti wa ZEC
- Sera ya kunena na Kutenda ya Wana CUF
- (no title)
- Ufungaji wa Kampeni ya uchaguzi mdogo wa Dimani.
- Salam kwa Mkururinza wa Zanzibar
No comments:
Post a Comment