BODI MPYA YA WADHAMINI YA CUF YASAJILIWA RASMI RITA
THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF–Chama Cha Wananchi)
THE DIRECTORATE OF INFORMATION, PUBLICITY AND PUBLIC RELATION
P.O.BOX 3537 ZANZIBAR
TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI
Imetolewa leo Tarehe 27/3/2017
Na. Kurugenzi ya Habari, Uenezi Na Mahusiano Na Umma-CUF Taifa
BODI MPYA YA WADHAMINI YA CUF YASAJILIWA RASMI NA WAKALA WA USAJILI, UFILISI NA UDHAMINI (REGISTRATION INSOLVENCY AND TRUSTEESHIP AGENCY -RITA):
BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA LA THE CIVIC UNITED FRONT (CUF-CHAMA CHA WANANCHI) lililofanyika MAKAO MAKUU YA CHAMA MJINI UNGUJA, ZANZIBAR TAREHE 19/3/2017 Katika agenda yake namba 4(A) lilipokea Mapendekezo ya uteuzi wa wajumbe wapya wa Bodi ya Wadhamini wa CUF ili kukidhi matakwa ya Katiba Mpya ya CUF Toleo la mwaka 2014 Ibara ya 98(1), (2), (3), (4), (5), na (6). Baraza Kuu baada ya mjadala wa kina liliwapitisha wafuatao kuwa WAJUMBE WA BODI YA WADHAMINI WA CUF;
1. ABDALLAH SAID KHATAU- KUTOKA MASASI, MTWARA.
2. ALI MBARAK SULEIMAN – KUTOKA UNGUJA, ZANZIBAR.
3. MOHAMED NASSOR MOHAMED- KUTOKA UNGUJA, ZANZIBAR.
4. DR. JUMA AMEIR MUCHI- KUTOKA UNGUJA, ZANZIBAR.
5. MWANAWETU SAID ZARAFI- KUTOKA KILWA, LINDI
6. BRANDINA OBASSY MWASABWITE, KUTOKA KINDONDONI , DAR ES SALAAM.
7. YOHANA MBELWA- KUTOKA HANDENI TANGA.
8. MWANA MASOUD- KUTOKA PEMBA
9. ZUMBA SHOMARI KIPANDUKA – KUTOKA MIKUMI, KILOSA.
Tayari Bodi hii mpya imesajiliwa rasmi Leo tarehe 27/3/2017 kwa WAKALA WA USAJILI, UFILISI NA UDHAMINI (REGISTRATION INSOLVENCY AND TRUSTEESHIP AGENCY -RITA), baada ya kukamilisha kujazwa fomu za Usajili na Marekebisho kwa stakabadhi za malipo (Receipt Number) Return of Trustees No. 14995170 na Notification for Change No. 14995169. Hatua hii muhimu kwa Chama imefanyika leo baada ya kukamilisha hatua zote za Kikatiba-CUF, Sheria za nchi, na Mikakati ya kuimarisha Chama ili kukabiliana na wenye nia ovu dhidi ya Taasisi ya CUF.
kikao hicho cha Baraza Kuu cha kawaida kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ndogo ya Makao Makuu ya Chama iliyopo Vuga, Mjini Unguja-Zanzibar, kilihudhriwa na Wajumbe halali 43 kati ya wajumbe wote Halali 53 na Wajumbe watano (5) kati ya hao hawakuweza kuhudhuria kwa kutoa udhuru kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuwa nje ya nchi. Wajumbe hao ni Ismail Jussa(Marekani/Uingereza), Ahmed Marshed(India), Juma Mkumbi(Marekani), Hashimu Mziray(msiba) na Mama Kimey ambae ni mgonjwa wa muda mrefu (Mwenyezi Mungu Amponye kwa Baraka zake). Wajumbe wote 43 walipitisha Majina haya ya Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya CUF. Uteuzi huu wa Bodi mpya Haubatilishi maamuzi yote halali yaliyochukuliwa na Bodi hapo awali. Usajili huu umesimamiwa kikamilifu na Katibu Mkuu wa Chama Maalim Seif Sharif Hamad, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Mheshimiwa Nassor Mazrui na Mkurugenzi wa fedha na Uchumi ambae pia ni Kaimu Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara Mheshimiwa Joran Lwehabura Bashange.
CUF NI TAASISI IMARA, YENYE VIONGOZI MAKINI.
HAKI SAWA KWA WOTE
----------------------------------------------
SALIM BIMAN
MKURUGENZI WA HABARI, UENEZI
NA MAHUSIANO NA UMMA- CUF TAIFA
MAWASILIANO: 077414112/ 0752 325227
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
- CUF wamuandikia barua Mwenyekiti wa ZEC
- TAMKO LA UMOJA WA KLABU ZA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA JUU YA KUTEKWA KWA MWANDISHI WA HABARI WA SAUTI YA UJERUMANI ( DW ) SALMA SAID.
- Sera ya kunena na Kutenda ya Wana CUF
- (no title)
- Toleo la Annur June 23
- Ufungaji wa Kampeni ya uchaguzi mdogo wa Dimani.
- Salam kwa Mkururinza wa Zanzibar
No comments:
Post a Comment