Headlines News :
KARIBU CUF DIASPORA NETWORK - CUF HAKI SAWA KWA WOTE...TEGEMEA KILA JIPYA NA ZURI KUTOKA KWETU...LIKE PAGE YETU KWENYE FACEBOOK
Home » , , , , » Kesi YA CUF DHIDI YA RITA KUUNGURUMA JULAI 10

Kesi YA CUF DHIDI YA RITA KUUNGURUMA JULAI 10

 

Mashauri sita yaliyofunguliwa katika Mahakama Kuu na Bodi ya Wadhamini ya CUF yanatarajiwa kusikilizwa na baadhi yake kutajwa tarehe, Jumatatu ya Julai 10, 2017, baada ya leo kuahirishwa usikilizwaji wa kesi ya msingi ya wizi wa ruzuku ya chama hicho. Kufuatia mawakili upande wa mashitaka kutopewa nakala ya maombi ya pingamizi la Mwanasheria Mkuu wa Serikali. 
Wakati akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, Wakili wa CUF, Juma Nassoro amesema leo mahakama hiyo imewapatia nakala za pingamizi hilo.
Na kwamba, Jaji Wilfred Dyansobela anayesimamia mashauri hayo amesema Jumatatu ijayo mashauri yote yatasikilizwa na kutajwa tarehe ikiwemo la kupinga maamuzi ya RITA ya kusajili wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa .
Shauri lingine litakalosikilizwa siku hiyo ni la kuzuia fedha za ruzuku ya chama hicho kupewa Profesa Lipumba na wenzake.
Aidha, upande wa Lipumba kupitia Abdul Kambaya haikuridhishwa na maamuzi hayo ya mahakama ya kuahirisha usikilizwaji wa kesi hiyo ya msingi kwa madai kuwa yanachelewesha muda.
“Sisi tulikuja kwa agizo la mahakama, badala yake jaji hakutokea tukasikia juu kwa juu kuwa kesi imeahirishwa. Wanachokifanya ni kuchelewesha muda jumatatu watazikwa,” amesema.  

Share this article :

No comments:

Post a Comment

 
Support : ZENJIBARZA
Copyright © 2011. ACT WAZALENDO DIASPORA NETWORK - All Rights Reserved