TAARIFA KWA UMMA
IMETOLEWA LEO 02/02/2016
BAKWATA MKOA DAR HAINA MAMLAKA YA KUITAKA CUF KUINGIA KWENYE UCHAGUZI
ALHAD MUSSA ANASHUGHULISHWA ZAIDI NA DUNIA KULIKO KUSIMAMIA HAKI
NI VYEMA AKAJIFUNZA KWA VIONGOZI WA KIKRISTO KUHUSU ZANZIBAR
CUF - Chama cha Wananchi, tunasikisitishwa na kushangazwa na kauli ilitolewa leo na Alhad Mussa, kuunga Mkono ukiukwaji wa Demokrasia uliofanywa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) sio tu Kuna onyesha sura halisi ya Kiongozi huyo wa Kiroho Lakini pia kinamuonyesha jinsi asivyokua na khofu ya Kukabiliana na Mola wake kwa Matendo atendayo hapa Duniani au kwa kauli atowazo kama Kiongozi wa Dini. Cuf tumezoea kumsikia mara kadhaa akiwashauli Viongozi wa Kisiasa na Viongozi wenziwe wa Kiroho kwamba wasichanganye Dini na Siasa, Lakini leo ajabu kwetu kumuona Alhad Mussa sio tu akichanganya Lakini akichupa Mipaka na kuitaka Cuf ishiriki kwenye Uchaguzi. Bila Shaka Alhad Mussa ni Mwanachama wa CCM kama ambavyo aliwahi kujitambulisha kwenye moja ya Shughuli za Kiserikali zilizopambwa na kunogeshwa na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi. Kwakua umeshindwa kusimamia Maendeleo ya Jamii unayoiongoza, tunahakika Huku unapokuja Sasa hutapaweza. Hali ya Zanzibar kwa Sasa ni tete na si suala jepesi kama Vile kwenda Ofisi za Bakwata pale Kinondoni. CUF tunaipuza kauli yako kama tunavyopuuza Uchafu wowote ule utakao kwenye Majumba yetu. CUF inawapongeza Viongozi wa Dini ya Kikristo ambao wameshatoa kauli ya Kupinga Ubakwaji wa Demokrasia na Maamuzi ya Wazanzibar. Tuna mtaka Alhad Mussa ajifunze kupitia kwa Viongozi Hao wa Dini ya Kikristo ambao wameonyesha uadilifu Mkubwa kwa kukemea ubabaishaji unaofanywa na ZEC. Kama Hana cha kujifunza kutoka kwa Viongozi wenziwe wa Kiroho kama alivyo yeye, basi ajifunze kwa Makada wa CCM ambao wanaijua vizuri CCM zaidi yake, ambao ni Benard Membe, Joseph Butiku na Dr Salim Ahmed Salim. Hata hivyo katika ile dhana au ile nia ya Kushughulishwa zaidi na Dunia kuliko kazi ya kulingania Waumini wake kutenda Mema na kuhimiza Maendeleo yao, Kielimu, Kiafya na Kiuchumi, Bila Shaka atakua amefikia Lengo la kuwafurahisha Maswahiba zake. CUF - Chama cha Wananchi hakiingii kwenye Uchaguzi hata iweje.
Huo ndio Msimamo wa Baraza Kuu la Uongozi Taifa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
- TAMKO LA UMOJA WA KLABU ZA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA JUU YA KUTEKWA KWA MWANDISHI WA HABARI WA SAUTI YA UJERUMANI ( DW ) SALMA SAID.
- CUF wamuandikia barua Mwenyekiti wa ZEC
- Sera ya kunena na Kutenda ya Wana CUF
- (no title)
- Ufungaji wa Kampeni ya uchaguzi mdogo wa Dimani.
- Salam kwa Mkururinza wa Zanzibar
No comments:
Post a Comment