Headlines News :
KARIBU CUF DIASPORA NETWORK - CUF HAKI SAWA KWA WOTE...TEGEMEA KILA JIPYA NA ZURI KUTOKA KWETU...LIKE PAGE YETU KWENYE FACEBOOK
Showing posts with label NEWS. Show all posts
Showing posts with label NEWS. Show all posts

CUF Wanawake wawapa 'take-care' Mutungi, Lipumba


Huku wakisubiri hukumu ya kesi zao zilizoko mahakamani dhidi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, na Profesa Ibrahim Lipumba, Jukwaa la Wanawake la CUF linamuonya Jaji Mutungi kuwa pakitokezea lolote baya kwenye nchi atahusika moja kwa moja


 

NDUNGAI NI NYOKA ANETAFUNA MKIANI

SERIAKLI YA CCM INAVYOJIKANYAGA LIPUMBA NA SAKAYA SIO WANCHAMA WA CUF ni mamluki walionunuliwa na CCM kuisambaratisha CUF kwa k usaidiwa na Msajili wa vyama , BRELA na Ofisi ya Speaker kutumika kuvuruga demokrrasia na kuzuia mabadiliko ndani ya nchi

Katibu Mkuu wa Chama cha CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema kwamba hatua ya Spika kuwavua ubunge , udiwani na kuteua wengine wapya inalenga kudhoofisha kambi ya wabunge wa CUF na Ukawa. Amesema Watanzania wanapaswa wajikumbushe kwamba hata kama hicho kinachoitwa ‘kuwafukuza uanachama’ wabunge halali wa CUF kingekuwa kiko sawa, hatua kama hiyo hufuata taratibu zote za kisheria na kikanuni za Bunge kujiridhisha kwanza. “ Spika Job Ndugai anadhani Watanzania ni vichaa wamuamini kuwa alishachukua hatua ya kujiridhisha kuwa wabunge wanane wa Chama cha Wananchi (CUF) wamefukuzwa uanachama kulingana na taratibu za chama hicho na hivyo wamekosa sifa za kuendelea na Ubunge. Ndani ya siku moja?” amehoji Maalim. Ameongeza kuwa Spika amejiridhisha vipi ikiwa hata hakuwasiliana na Katibu Mkuu wa Chama ambaye kwa mujibu wa Katiba ya CUF ndiye Mtendaji Mkuu wa shughuli za chama na pia kwa nafasi hiyo ndiye katibu wa vikao vya Mkutano Mkuu wa Taifa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama? Amesema yeye kama katibu, alimuandikia Spika Ndugai barua, Jumanne, Julai 25 akimueleza kwamba hilo lililoitwa Baraza Kuu la Uongozi la CUF halikuundwa na wajumbe halali wa Baraza Kuu. “Angekuwa na nia ya kweli ya kutaka kujiridhisha si hapo ndipo pangekuwa pa kuanzia kwa kuwepo kile wanasheria wanachokiita shaka inayoweza kuingia akilini yaani ‘reasonable doubt’?’’ amehoji. Hata hivyoa amesema Spika Ndugai aliyapuuza yote hayo kwa sababu ni kinyume na mkakati wa Dola wa kuihujumu CUF na kuua demokrasia Tanzania. Hapo ndipo Spika Job Ndugai alipolifikisha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

MAHAKAMA YAIPIGA NA CHINI HOJA ZA SERIKALI DHIDI YA KESI YA CUF

Mahakama yatupa hoja za serikali ya kesi ya CUF


MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imekubaliana na hoja za Wakili wa Wabunge wanane wa Chama cha Wananchi CUF ambao ubunge umetenguliwa baada ya kuvuliwa uanachama, na sasa pingamizi la muda litaanza kusikilizwa Jumatatu,


Awali serikali iliwasilisha mapingamizi matatu ambapo jana iliondoa moja na kubakia mawili likiwamo la kuiomba mahakama isiingilie mhimili wa Bunge kwa kuzuia wabunge hao wasiapishwe.
Mapingamizi mawili ya serikali nayo yalitupwa na mahakama huku serikali ikiambiwa kinachofanyika siyo kuingilia mhimili wa Bunge.
Kwa mujibu wa mahakama, shauri dogo namba 479 litaanza kusikilizwa jumatatu ambalo litakuwa na mambo makuu saba likiwamo hoja ya kuzuia wabunge wanane wa CUF kuapishwa.

Jaji Lugani Mwandambo amekubali hoja za Wakili wa wabunge hao, Peter Kibatala kwamba shauri hilo limefunguliwa kwa kifungu sahihi na kwamba litaendelea kusikilizwa.

Mahakama hiyo imezitupa hoja tatu za serikali, ikiwamo kutaka chombo hicho kutupilia mbali hoja za kuzuia kuapishwa wabunge hao.Mwandambo alisema kinachofanyika kwa sasa katika kesi hiyo siyo kuingilia mahakama kama hoja ya serikali ilivyowasilisha hoja hiyo.

Chanzo cha wabunge hao kuvuliwa ubunge kimetokana na Chama cha Wananchi (CUF), chini ya Profesa Ibrahim Lipumba kuwavua uanachama.*

MAAAMUZI YA BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA LA THE CIVIC UNITED FRONT (CUF - CHAMA CHA WANANCHI) KUHUSIANA NA HUJUMA ZA DOLA DHIDI YA CUF

Image may contain: 1 person
BARAZA Kuu la Uongozi la Taifa lilipokea, kujadili na kufanya maamuzi kuhusu ajenda moja tu iliyowasilishwa kwake na Kamati ya Utendaji ya Taifa ambayo ilikuwa ni: • Taarifa kuhusu kile kinachoitwa kuwavua uanachama Wabunge wanane (8) na Madiwani wawili (2) wa Viti Maalum kupitia CUF kilichotangazwa kufanywa na Ibrahim Lipumba na kikundi chake ikiwa ni mwendelezo wa hujuma za Dola dhidi ya Chama cha CUF. Baada ya mjadala wa kina, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa linapenda kutoa maazimio yafuatayo kuhusiana na tukio hilo na mwendelezo wa vitendo na matukio mengi ya hujuma yanayofanywa na Dola dhidi ya CUF:-

1. KUHUSU UHALALI WA BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA: Kutokana na mkanganyiko unaosababishwa na upotoshaji wa makusudi unaofanywa na Ibrahim Lipumba na kikundi chake wa kuitisha watu wa kuokota barabarani na kuwakusanya Buguruni huku akiwaita kuwa ndiyo Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF, tumeona kuna haja ya kuweka kumbukumbu sahihi ili kuepusha upotoshaji huo usiendelee. Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama huwa linaundwa kila baada ya miaka mitano kupitia Uchaguzi Mkuu wa Chama ndani ya Chama na hupata wajumbe wake kupitia uchaguzi unaofanywa na Mkutano Mkuu wa Taifa (wajumbe 25 kutoka Tanzania Bara na wajumbe 20 kutoka Zanzibar), wajumbe 14 wanaoteuliwa na Mwenyekiti kwa kushauriana na Makamu Mwenyekiti na kisha kuthibitishwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa, wajumbe wanaoingia kwa nafasi zao wakiwemo Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Chama, Wenyeviti na Makatibu wa Jumuiya za Chama na Viongozi wa Kambi za Wabunge na Wawakilishi wa Chama. Viongozi Wakuu wa kitaifa wa Chama pia ni wajumbe. Wafuatao ndiyo Wajumbe halali waliochaguliwa na Mkutano Mkuu wa Taifa uliomalizika Juni 27, 2014 hapo Ubungo Plaza, Dar es Salaam kuwa wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa (BKUT) watakaokaa madarakani kwa kipindi cha miaka mitano (2014 – 2019) hadi watakapochaguliwa wengine na Mkutano Mkuu wa Taifa kwa mujibu wa Katiba ya CUF ya mwaka 1992 (Toleo la 2014):- VIONGOZI WAKUU: 1. Mwenyekiti (alijiuzulu tarehe 5 Agosti, 2015 na kujiuzulu kwake kuthibitishwa na Mkutano Mkuu wa Taifa wa dharura tarehe 21 Agosti, 2016).

Mbunge wa Temeke akamatwa kihuni

Image result for ABDALL MTOLEA PICTURES

SITAKI KUMUONA LIPUMBA ASEMA MBUNGE WA TEMEKE

Mbunge wa Temeke kwa tiketi ya CUF, Abdallah Ally Mtolea amefunguka na kusema kwa sasa hana jambo la kumshauri Profesa Lipumba na kudai haitaji hata kumuona kwa sababu ameshapoteza ile heshima na thamani yake.

Mtolea amesema hayo leo alipokuwa akihojiwa na EATV na kusema yeye alikuwa ni miongoni mwa watu ambao walikuwa wanamuheshimu sana  Prof. Ibrahim Lipumba kiasi kwamba ilifika hatua hakutaka kua muongeaji sana juu ya mambo yake lakini kwa kuwa tayari ameshajivunjia heshima mwenyewe hivyo hana budi kusema.
"Mimi nilianza kuona nia mbaya ya Lipumba pale aliponikatalia kwenda kwenye ufunguzi wa kampeni zangu mwaka 2015 kwani nilimfuata lakini yeye alikataa kabisa, lakini niliposhinda ubunge nilimfuata pia na kumpa taarifa na kumuomba tuendelee kushirikiana nikiamini yeye ni mkongwe katika siasa kuna mambo mengi ya kunishauri na kuniongoza sikumtenga kabisa, ila aliposema anataka kurudi baada ya kujiuzulu mimi sikumuelewa ni nikamfuata nikimwambia mzee unataka kutuletea mgogoro" alisema Mtolea 
Mbali na hilo Mtolea anasema saizi Lipumba amefikia hatua ambayo haambiliki chochote na kusema hatamani hata kukutana naye 
Msikilize hapa akifunguka zaidi 

Kesi YA CUF DHIDI YA RITA KUUNGURUMA JULAI 10

 

Mashauri sita yaliyofunguliwa katika Mahakama Kuu na Bodi ya Wadhamini ya CUF yanatarajiwa kusikilizwa na baadhi yake kutajwa tarehe, Jumatatu ya Julai 10, 2017, baada ya leo kuahirishwa usikilizwaji wa kesi ya msingi ya wizi wa ruzuku ya chama hicho. Kufuatia mawakili upande wa mashitaka kutopewa nakala ya maombi ya pingamizi la Mwanasheria Mkuu wa Serikali. 
Wakati akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, Wakili wa CUF, Juma Nassoro amesema leo mahakama hiyo imewapatia nakala za pingamizi hilo.
Na kwamba, Jaji Wilfred Dyansobela anayesimamia mashauri hayo amesema Jumatatu ijayo mashauri yote yatasikilizwa na kutajwa tarehe ikiwemo la kupinga maamuzi ya RITA ya kusajili wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa .
Shauri lingine litakalosikilizwa siku hiyo ni la kuzuia fedha za ruzuku ya chama hicho kupewa Profesa Lipumba na wenzake.
Aidha, upande wa Lipumba kupitia Abdul Kambaya haikuridhishwa na maamuzi hayo ya mahakama ya kuahirisha usikilizwaji wa kesi hiyo ya msingi kwa madai kuwa yanachelewesha muda.
“Sisi tulikuja kwa agizo la mahakama, badala yake jaji hakutokea tukasikia juu kwa juu kuwa kesi imeahirishwa. Wanachokifanya ni kuchelewesha muda jumatatu watazikwa,” amesema.  

TAMKO LA MADIWANI WA THE CIVIC UNITED FRONT (CUF-CHAMA CHA WANANCHI) WA MKOA WA DAR ES SALAAM JUU YA KUUNGA MKONO HOTUBA NA MSIMAMO WA CHAMA ULIOTOLEWA NA KATIBU MKUU MAALIM SEIF SHARIF HAMAD TAREHE 28 JUNE 2017 KATIKA HOTEL YA PEACOCK:

4
Image may contain: 4 people, people sitting, table and indoor
THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF-CHAMA CHA WANANCHI)
TAMKO LA MADIWANI WA THE CIVIC UNITED FRONT (CUF-CHAMA CHA WANANCHI) WA MKOA WA DAR ES SALAAM JUU YA KUUNGA MKONO HOTUBA NA MSIMAMO WA CHAMA ULIOTOLEWA NA KATIBU MKUU MAALIM SEIF SHARIF HAMAD TAREHE 28 JUNE 2017 KATIKA HOTEL YA PEACOCK:
Tarehe 5 JULY, 2017
NDUGU WAANDISHI WA HABARI,
WAHESHIMIWA VIONGOZI WA CUF,
WAHESHIMIWA WANACHAMA WA CUF,
WAHESHIMIWA WANANCHI, MABIBI NA MABWANA,
NAOMBA NIANZE KWA KUWASALIMU KWA SALAMU ZA CHAMA CHETU HAKI SAWA KWA WOTE,
1. Awali ya yote, tuanze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kutujaalia uhai na uzima na kutuwezesha kukutana hapa asubuhi hii, kwa lengo la kutoa Tamko na msimamo wetu Rasmi juu ya sintofahamu inayoendelea ndani ya Chama chetu, na kuunga mkono Hotuba na msimamo wa Chama uliotolewa na Katibu Mkuu wetu, Maalim Seif Sharif Hamad. Tukiwa ni Madiwani wa CUF, kutoka Manispaa za Mkoa wa Dar es Salaam na kupitia kwenu ujumbe wetu uweze kuwafikia wana-CUF wenzetu, Wapenda Mabadiliko wote nchini, na Watanzania kwa Ujumla.
2. Tunapenda kuchukua fursa hii kuwashukuru nyinyi Waandishi wa Habari kwa kuhudhuria kwenu na mara zote kutukimbilia kila tunapokualikeni mbali na Changamoto mnazokabiliana nazo juu ya uhuru wa Habari na aina ya uongozi wa Serikali ya awamu ya Tano jinsi unavyoikandamiza demokrasia nchini na kutopenda kukosolewa.

BASHANGE AWATULIZA WANA CUF

ZANZIBAR STONE TOWN MEMBER OF PARLIAMENT STAND WITH GIRLS

I STAND FOR THE GIRLS ... PLEASE JOIN ME
Image result for ALLY SALEH PICTURES
By Ally Saleh
Many people have come to the defence of young girls who get into wrong side and become pregnant while still at school be it at primary level or secondary one and thus cut off from following their educational programs.
Thus means not only dreams but also hopes are dashed and buried in a grave that most of them would not be able even to trace as they grow old and lament only. But then lamenting will not be enough because their lack of education might be an obstacle to their development and end up in the poverty cycle.
Most people believe that pregnancy in young girls is never wanted but these young females are caught at a time when they are not only naïve but also at an age where foolishness is only thing they do. And on top of it both young men and those of old age with good cash flow pry on these innocent souls and and trap them.
Some feel it is cruel to blame a girl of 13 or even 16 and 17 to have willingly made a choice of entering sex life and hence with no education to protect herself from becoming pregnant but even from being passed with HIV AIDS or any other sexual transmitted diseases.
A month ago a debate ensued at the Parliament about change of the 1971 Law of Marriage Act in order to change marriage age in Tanzania and a big shout was recorded with two opposing sides arguing their cases with no results. Those who refuse lean on morality and those who want it be raised to be 18 lean of reality.
There not even consensus with the Cabinet Members as the then newly appointed Minister for Constitutional and Legal Affairs Professor Palmagamba Kabudi took a cautious approach saying the government was still synthesizing the issue while Minister for Women and Health Ummy Mwallimu skipping out of official Budget presentation notes indicated that things were moving on to effect changes.
But while the debate is still raging in the public domain with consensus being sought with activists charging time was up for the changes, the traditionalist especially those with religious inclinations have been saying this was only going to happen over their dead bodies.
The latter’s argument is that if a girl was pregnant and returned to classes after delivery will poison the others on their habits, which tends to assume that the only bad thing is to become pregnant ignoring the very act of having sex which is not committed only by the girl who becomes pregnant but many and most others around her.

MAALIM SEIF AWAPANDISHA RITA MAHAKAMANI

RITA) MAELEZO YA JUMLA YA KATIBU MKUU WA CUF, SEIF SHARIF HAMAD, KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA WA WATANZANIA JUU YA MUENDELEZO WA HUJUMA ZINAZOFANYWA NA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI JAJI FRANCIS MUTUNGI DHIDI YA CUF KWA KUTUMIA WAKALA WA USAJILI, UFILISI NA UDHAMINI (

PEACOCK HOTEL, DAR ES SALAAM, TAREHE 28 JUNE, 2017

Ndugu zangu wahariri na waandishi wa habari,

Awali ya yote nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kutujaalia uhai na uzima na kutuwezesha kukutana leo hapa. Nitumie fursa hii pia kuwapa mkono wa Eid Mubarak Waislamu wa hapa nchini pamoja na Waislamu wengine duniani wanaoendelea na maadhimisho ya sikukuu ya Eid-el-Fitr kufuatia kukamilika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Pili, nawashukuru na nyinyi Wahariri na waandishi wa habari kwa kupokea mwaliko wetu na kuhudhuria mkutano huu. Siku zote mmetupa mashirikiano makubwa katika shughuli zetu na kuufikisha ujumbe wetu kwa umma wa Watanzania na ulimwengu kwa ujumla. Ahsanteni sana.

Ndugu Wahariri na waandishi wa habari, mtakumbuka vyema tarehe 9 Aprili, 2017 katika ukumbi wa Hotel ya Ramada Encore Dar City Centre jijini Dar es Salaam, nilitoa maelezo ya kutosha kuhusu mbinu chafu iliyopangwa kufanywa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kwa maelekezo ya Dola kupitia Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kwa lengo la kumnusuru kibaraka wao Ibrahim Haruna Lipumba kwa kuhakikisha kwamba Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini feki waliopelekwa na kibaraka Lipumba wanasajiliwa baada ya kuona Bodi halali ya CUF - Chama Cha Wananchi ni kikwazo katika kufanikisha mipango yao haramu ya kufungua akaunti mpya ya benki ili kuwezesha wizi wa ruzuku ya Chama.

Katika mkutano huo, nilifafanua pia na kueleza kwa kina hujuma zinazofanywa na dola dhidi ya CUF - Chama Cha Wananchi hasa baada ya mafanikio makubwa na ushindi wa kutosha uliopatikana Zanzibar katika uchaguzi wa Oktoba, 2015. Sitoyarejea tena hapa niliyoyaeleza siku ile.

RITA YAKUBALI KUTUMIWA KATIKA MPANGO HARAMU

Niseme tu kwamba yale tuliyoyaeleza tarehe 9 Aprili yamethibitika wiki iliopita kwa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kutekeleza alichoagizwa kufanywa ambacho ni kusajili wajumbe feki wa Bodi ya Wadhamini ya CUF. Mtaona utekelezaji umechukua muda kwa sababu inaonekana baada ya kuzieleza njama zile hadharani na nyinyi vyombo vya habari kuziandika, RITA walishtuka na kudai bado wanayafanyia kazi maombi yaliyowasilishwa na wanahitaji kujiridhisha juu ya uhalali wa vyombo vilivyofamya mabadiliko yaliyowasilishwa kwao.

Nilieleza siku ile kwamba tokea kuanza kwa njama ovu na mbinu chafu hizi, moja ya vinavyoonekana vikwazo vikubwa vinavyokwamisha kufanikiwa malengo ya wanaomtumia kibaraka Ibrahim Lipumba imekuwa ni Bodi ya Wadhamini ya THE CIVIC UNITED FRONT (CUF - Chama Cha Wananchi) ambayo imechukua hatua madhubuti za kukilinda Chama na; hususan, rasilimali zake kupitia Mahakama na taratibu nyingine za kiutawala na kisheria. Hatua hizo zilizochukuliwa na Bodi ya CUF ni kwa mujibu wa Katiba ya Chama ya mwaka 1992(Toleo la 2014) kifungu cha 98(4) ambayo nanukuu:

"98(4) - Bodi inaweza kushtaki au kushitakiwa kwa niaba ya Chama"

Aidha mamlaka hayo yamebainishwa katika Sheria ya Wadhamini (The Trustees' Incorporation Act Cap.318), kifungu cha 8(1)(b), nanukuu:

"8(1) Upon the grant of a certificate under subsection (1) of section (5), the trustee or trustees shall become a body corporate by the name described in the certificate, and shall have;-

(b) power to sue and be sued in such corporate name"

Tunazo taarifa zisizo na shaka kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA amepata shinikizo kubwa kusajili wajumbe feki wa Bodi ya Wadhamini ya CUF kwa kutumia majina yaliyowasilishwa na kibaraka Lipumba ili kuhujumu majina halali yaliyopitishwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kupitia kikao chake kilichofanyika Makao Makuu ya Chama Zanzibar, tarehe 19 Machi, 2017. Afisa Mtendaji Mkuu huyo wa RITA amenukuliwa na vyombo vya habari kukiri hivyo alipohojiwa akiwa Dodoma kama ilivyonukuliwa na gazeti la Mwananchi toleo Na.6176 la tarehe 25 Juni, 2017. Aidha katika barua aliyomwandikia Kaimu Katibu Mkuu (cheo ambacho hakipo kwenye Katiba ya CUF), amebainisha wazi wazi kuwa usajili huo wa wajumbe feki wa Bodi ya CUF umezingatia barua mbili alizoandikiwa na Msajili wa Vyama vya Siasa zenye Kumb. Na. CHA.322/362/14/23 ya tarehe 4/4/2017 na Kumb. Na. CHA.322/362/14/30 ya tarehe 11/5/2017. Wakati akihojiwa na gazeti la Mwananchi, Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Mama Emmy Hudson, amejitetea na kuweka wazi kuwa mtu mahsusi wa kutoa majibu ya kwa nini yamesajiliwa majina feki ya Bodi ya CUF ni Msajili wa Vyama vya Siasa.

Pamoja na kwamba utetezi huo haumwondoi Mama Hudson kutiwa hatiani kwa kosa la matumizi mabaya ya madaraka kutokana na kwamba anayesajili Bodi sio Msajili ya Vyama vya Siasa bali ni yeye (RITA) na sheria inamtaka kujiridhisha na nyaraka zinazowasilishwa kwake na waombaji. Suala hilo limefafanuliwa vizuri na yeye mwenyewe kupitia taarifa yake kwa umma ya tarehe 29 Machi, 2017. Katika ibara ya (3) ya taarifa hiyo Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu na Kaimu Kabidhi Wasii Mkuu wa RITA, Mama Emmy K. Hudson anasema (nanukuu):

"Tarehe 27 Machi, 2017 Wakala ulipokea maombi ya Usajili wa Bodi mpya ya Wadhamini ya CUF. Kwa mujibu wa utaratibu, maombi hayo yakipokelewa hupitia katika hatua ya uchambuzi wa taarifa zilizowasilishwa ili kujiridhisha sababu za mabadiliko hayo, na kuangalia iwapo taratibu zilifuatwa katika upatikanaji wa wadhamini hao kwa kuzingatia maamuzi ya mkutano uliohusika kupitisha mabadiliko hayo, hii ni kwa mujibu wa kifungu 17(a). Hatua hii bado haijakamilika."

Maelezo hayo yamenukuliwa kutoka kwenye Sheria ya Wadhamini (The Trustees' Incorporation Act Cap. 318), kifungu cha 17(a) kinachotamka ifuatavyo:

"17 - No changes of the names of a person who is or who were trustee or trustees of a body corporate  or organization incorporated under this Act shall be authorised by the Registrar-General unless he is satisfied that-

a) There were held a lawful meeting of the body corporate or organization for the purpose of electing a person or persons as trustees of such a body corpotate or organization."

Ndugu Wahariri na waandishi wa habari, kwa sababu ya kutaka uelewa fasaha wa hujuma iliyofanywa na RITA akishirikiana na Msajili wa Vyama vya Siasa na kibaraka wake Lipumba kuhusiana na Bodi ya Wadhamini ya The Civic United Front (CUF - Chama Cha Wananchi), naomba kutoa maelezo ufafanuzi.

Bodi ya Wadhamini ya CUF ilisajiliwa mwaka 1993 kwa kufuata taratibu zote za kisheria (Sheria ya Vyama vya Siasa, Sura 258 na The Trustees' Incorporation Act Cap. 318) na kupatiwa hati ya usajili Na. ADG/T.1/1127. Sheria ya Wadhamini (The Trustees' Incorporation Act Cap. 318) kifungu cha 8(1a) kinasema Bodi iliyosajiliwa ni endelevu isipokuwa kama imefutwa. Hapa nanukuu:

"8(1). Upon the grant of a certificate under subsection (1) of section (5) the trustee or trustees shall become a body corporate by the name described in the certificate, and shall have;-

(a) perpetual succession and common seal"

CUF - Chama Cha Wananchi kimeendelea kuheshimu na kutekeleza  matakwa ya sheria hiyo kwa kuweka sawa kumbukumbu za Bodi yake na kufanya mabadiliko kila ilipobidi kwa mujibu wa Katiba ya Chama kifungu 98(1) na kuwalipia wadhamini ada ya kila mwaka (return of trustees) ambayo kwa sasa ni Tshs. 50,000/=. Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya CUF walifanyiwa mabadiliko madogo mara ya mwisho mwaka 2012 na imeendelea kulipiwa ada ya wadhamini ya kila mwaka hadi tarehe 24 Mei, 2017 kwa mujibu wa kumbukumbu ya stakabadhi ya malipo iliyotolewa na RITA tarehe 24 Mei, 2016 yenye Na.105888047. Kwa mantiki hiyo mabadiliko mengine ya wajumbe wa Bodi yalipaswa kufanya mwaka huu wa 2017.

CUF kupitia Baraza Kuu la Uongozi la Taifa lililochaguliwa kihalali kupitia Mkutano Mkuu wa Taifa wa mwezi Juni mwaka 2014 na kwa kufuata masharti mapya ya Katiba ya 1992 (Toleo la 2014) ilifanya mabadiliko machache ya wajumbe wa Bodi ya Wadhamini tarehe 19 Machi, 2017 na kuyawasilisha kupitia barua ya Katibu Mkuu Kumb. Na. CUF/HQ/AKM/003/RT/001 ya tarehe 24 Machi, 2017 kwa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA). Aidha pamoja na barua hiyo Fomu T.I.4 (Notification) na T.I.5 (Return of Trustees) na malipo ya Tshs. 100,000/= yalifanywa na kupatiwa stakabadhi mbili; Na.14995169 (Notification) na Na.14995170 (Return of Trustees) zote za tarehe 27 Machi, 2017.

Kuthibitisha kupokelewa kwa mabadiliko hayo, Msimamizi wa Wadhamini RITA alikiri kwa barua Kumb. Na.ADG/T.1/1127/29 ya tarehe 31 Machi, 2017 aliyomwandikia Katibu Mkuu wa CUF - Chama Cha Wananchi. Katika barua hiyo, Msimamizi wa Wadhamini alimjulisha Katibu Mkuu kuwa pindi taratibu zitakapokamilika atamtaarifu. Mpaka ninapozungumza nanyi hapa, Katibu Mkuu hajataarifiwa chochote, jambo ambalo linakinyima Chama chetu hata haki ya kukata rufaa kwa Waziri kwa mujibu wa sheria ya Wadhamini (The Trustees'  Incorporation Act Cap. 318), kifungu cha (27) kama kilivyonukuliwa hapa:

"27. Appeals
Any person aggrieved by the refusal of the Administrator-General to grant a certificate of incorporation or to approve a change of name, or by any conditions or directions inserted in any certificate of incorporation, or by the revocation of the incorporation of any body corporate may within twenty-one days after the notification of such refusal, conditions or directions or revocation, as the case may be, appeal to the Minister responsible for legal affairs and the Minister may make such order as the circumstances may require and except as aforesaid no appeal shall lie against any such refusal, conditions or directions or revocation."

Hata hivyo, mara baada ya kuwasilisha mabadiliko hayo, kibaraka Ibrahim Lipumba naye akatakiwa na Msajili haraka aandae majina yake na kuyafikisha RITA na kwamba Ofisi ya Msajili itatoa maelekezo kwa RITA nini wafanye. Ni dhahiri barua mbili za Msajili wa Vyama vya Siasa za tarehe 4/4/2017 yenye Kumb. Na. CHA.322/362/14/23 na tarehe 11/5/2017 yenye Kumb. Na. CHA.322/362/14/30 zilizonukuliwa na RITA katika barua ya kuitambua Bodi feki ya kibaraka Lipumba zinahusika na maelekezo hayo.

Lakini pamoja na maelekezo kutoka kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, RITA si kwamba amefanya kitu ambacho hakifahamu.  Mwezi Novemba, 2016 baada ya Bodi kumfungulia kesi Msajili wa Vyama vya Siasa (Shauri Na. 23/2016 ambalo liko Mahakama ya Rufaa), Msajili wa Vyama vya Siasa katika hatua za kutaka kujinusuru na mkono wa sheria aliwasiliana na RITA kupitia barua Kumb. Na. HA.322/362/14/30 ya tarehe 14 Novemba, 2016 akiomba kusaidiwa kughushi kumbukumbu za Bodi ya CUF ili ionekane Bodi imepita muda wake na hailipii ada zake tangu mwaka 2010.

Msajili wa Vyama vya Siasa akiwa Jaji wa Mahakama Kuu alifanya hivyo akijua fika kuwa anachomshawishi RITA kufanya ni kosa la jinai na ikizingatiwa kuwa mwezi Oktoba, 2016 alikamilisha uhakiki wa utekelezaji wa masharti ya usajili kwa vyama vya siasa vyote nchini, ambapo alivifuta vyama kadhaa visivyokidhi masharti hayo na CUF - Chama Cha Wananchi hakikuwa miongoni mwa vyama visivyokidhi masharti. Barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa Kumb. Na. HA.322/362/01/21 ya tarehe 24 Oktoba, 2016 kwa makatibu wakuu wa vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu ni ushahidi wa zoezi hilo la uhakiki.

Baada ya kupata taarifa hizo za muendelezo wa hujuma za Msajili wa Vyama vya Siasa kupitia RITA, Katibu Mkuu wa CUF aliandika barua Kumb. Na.  CUF/HQ/BRT/005/016/12 ya tarehe 10 Oktoba, 2016 kuitahadharisha RITA juu ya mipango hiyo iliyokuwa ikiratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa. Barua hiyo ya Katibu Mkuu iliambatanishwa na nyaraka za kughushi za Msajili wa Vyama vya Siasa na mfuasi wa kibaraka Lipumba anayeitwa Thomas Malima akijitambulisha kama Katibu wa Bodi zilizopelekwa Bank ya NMB Ilala katika harakati za kutaka kuiba fedha za ruzuku ya Chama.

Jambo la ajabu RITA licha ya kuwa na jopo kubwa la wanasheria, ilikubali ombi la Msajili wa Vyama vya Siasa na kwa barua Kumb. Na. ADG/T.1/1127/16 ya tarehe 15 Novemba, 2016 iliyosainiwa na Afisa wake anayeitwa Gilbert P. Bubelwa iliwasilisha nyaraka za kughushi zilizoambatanishwa kwenye hati ya kiapo ya Mwanasheria Mkuu wa serikali kupinga kufunguliwa kwa shauri dhidi ya Msajili wa Vyama vya Siasa. Jambo la kushangaza wameghushi mpaka sahihi ya kibaraka Lipumba licha ya kwamba ni mshirika wao.

Ndugu wahariri na waandishi wa habari, baada ya kugundua kuwa Chama kinazo nakala halisi na stakabadhi za malipo hadi mwaka 2016 na kwa hivyo nyaraka zao za kughushi haziwezi kuwasaidia, ndipo wakaja na njama hii ya pili ya kusajili Bodi feki kwa malengo makuu manne yafuatayo:-

1) Kufuta kesi zote zilizofunguliwa na ambazo zinawaelemea licha ya kutumia nguvu kubwa ya dola.

2) Kufungua akaunti mpya ya benki ili kumwezesha kibaraka Lipumba kupata ruzuku.

3) Bodi hiyo kuwezesha udhibiti wa Ofisi za Makao Makuu, Zanzibar.

4) Kumwondoa madarakani Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad na hivyo kufanikisha njama za kuwapokonya haki yao Wazanzibari kwa maamuzi yao ya tarehe 25 Oktoba, 2015.

Baada ya kupata taarifa za uhakika juu ya njama hizo ovu, na kupata stakabadhi ya malipo ya kibaraka Lipumba ya mabadiliko ya wajumbe wa Bodi yenye Na. 14995179 ya tarehe 27 Machi, 2017 iliyotolewa na RITA, Katibu Mkuu wa CUF alimwandikia tena barua RITA yenye Kumb. Na. CUF/HQ/AKM/003/017/01 ya tarehe 28 Machi, 2017 kumtahadharisha juu ya njama hizo kama alivyokuwa amefanya awali mwezo Novemba, 2016.

Aidha, Katibu wa Bodi halali ya Wadhamini, Mhe. Joran Bashange alikwenda RITA na kukutana na wanasheria Gilbert P. Bubelwa na Mwakatobe na kuwaeleza juu ya njama hizo ovu lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kuikabili hali hiyo. Jambo hilo linadhihirisha wazi kuwa njama, hujuma na mipango yote ya kuihujumu CUF ni ya dola. Kwa hali ilivyo ya utawala wa serikali ya awamu ya tano haingii akilini kama mtumishi yeyote wa umma anaweza kuwa na ujasiri wa kufanya makosa makubwa ya kijinai wazi wazi namna hii. Watawala wanafanya hivyo kwa kujidanganya kuwa wataweza kuidhibiti CUF na hivyo khofu yao ya madai ya Wazanzibari juu ya haki yao ya ushindi ulioporwa katika uchaguzi wa tarehe 25 Oktoba, 2015 itakuwa imetoweka. Aidha wanadhani kuwa Watanzania wanaoiamini CUF kama taasisi imara ya kuwaletea mabadiliko ya kweli watasambaratika.

Ndugu wahariri na waandishi wa habari, taarifa za kusajiliwa Bodi feki ya kibaraka Lipumba kwa shinikizo la dola kupitia Msajili wa vyama vya Siasa na RITA zilipatikana tarehe 20 Juni, 2017 ambapo mawakili wa Chama walitaarifiwa kwa njia ya simu na karani wa Mahakama kuwa Shauri Na. 21/2017 mbele ya Jaji Wilfred Dyansobera, dhidi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali lililokuwa limepangwa tarehe 3 Agosti, 2017 ghafla limerudishwa nyuma hadi Jumatano ya tarehe 21 Juni, 2017 (hakuna summons zilizotolewa). Aidha Jumanne, tarehe 20 Juni, 2017 wafuasi wa kibaraka Lipumba walianza kuandika kupitia mitandao ya kijamii wakihamasishana kukusanyika Ofisi Kuu Buguruni tarehe 21/6/2017 wakitangaza kwamba mambo yote yamekwisha. Baadaye CUF - Chama Cha Wananchi kikapata taarifa za uhakika kuwa RITA imesajili Bodi feki ya Lipumba, na kwamba tayari imekwishamtaarifu Jumamosi ya tarehe 17 Juni, 2017 na kwamba wanakwenda kufuta kesi zote ili pia Msajili aweze kuanza kuwapatia ruzuku.

Jumatano, tarehe 21 Juni, 2017 siku ambayo kesi ilipangwa kusikilizwa Afisa mwandamizi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Bw. Sisty L. Nyahoza alifika Mahakama Kuu ya Tanzania Dar es salaam na kufanya mazungumzo ya siri na uongozi wa Mahakama. Wakati mazungumzo hayo yanaendelea ilikuwa ikitangazwa kuwa mashauri yote mbele ya jaji Wilfred Dyansobera, yataanza kusikilizwa saa 4.00 asubuhi hivyo wenye mashauri waendelee kusubiri.

Jumatano hiyo ya tarehe 21 Juni, 2017 saa 3.20 za asubuhi (muda mfupi kabla ya shauri kuitwa) ndipo mawakili wetu  walipopatiwa barua mbili zilizosainiwa na mfuasi wa kibaraka Lipumba anayeitwa Thomas Malima akijitambulisha kuwa eti ni Katibu wa Bodi. Barua aliandikiwa Msajili wa Mahakama Kuu na kunakiliwa kwa Jaji Wilfred Dyansobera.

Ø Ya kwanza ikimtaarifu kuondolewa kwa mawakili wetu wasomi Juma Nassor, Daimu Halfani na Hashim Mziray na eti kumuajiri wakili msomi Makubi Kunju Makubi.

Ø Ya pili ikiomba kufutwa kwa Shauri Na. 21/2017 linalomkabili Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi la wizi wa fedha ya ruzuku ya Chama takriban Tshs.369 milioni. (Thomas Malima ambaye aliomba ajumuishwe kama mlalamikiwa "RESPONDENT" kwenye shauri hilo ghafla amejigeuza kuwa mlalamikaji na anawasilisha barua mahakamani kufuta kesi).

Kupitia muhtasari wa kugushi wa kilichoitwa kikao cha Bodi feki ya kibaraka Lipumba, kilichoketi Jumamosi tarehe 17 Juni, 2017 na kuhudhuriwa na wajumbe Jumatano tarehe 21 Juni, 2017 lakini barua kupelekwa kwa Msajili wa Mahakama Jumatatu tarehe 19 Juni, 2017, azimio la Bodi feki ni kufuta kesi zote zilizofunguliwa dhidi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, kibaraka Lipumba na wafuasi wake. Ni wazi nyaraka hizo zote ni za kughushi.

Ndugu Wahariri na waandishi wa habari, Chama chetu kimepatwa na mshtuko mkubwa sana, kuona taasisi kubwa na nyeti yenye dhamana kubwa katika nchi inaweza kufanya vitendo vya ovyo vya kughushi nyaraka kama hivyo. RITA ni taasisi inayobeba maisha ya watu ya kila siku. Licha ya kusajili Bodi za Wadhamini, inasajili vizazi na vifo, ndoa, talaka na inatunza WOSIA kwa ajili ya mirathi. Katika mazingira ya kujihusisha na vitendo vya ovyo, vilivyokosa maadili ya utumishi wa umma na vya kijinai kama hivi, itaaminikaje kwa wananchi na taasisi nyingine? RITA wameacha kuongozwa na weledi katika kutekeleza majukumu yao badala yake wamesukumwa na utashi binafsi wa kifisadi na hujuma dhidi ya taasisi ya CUF. Ukiipitia barua ya RITA kwa kibaraka Lipumba unajiuliza maswali kama imetoka kweli kwenye taasisi hiyo iliyosheheni wasomi na wanasheria waliobobea. RITA imedhihirisha kuwa sio chombo cha kutenda haki na kusimamia misingi yake. Yumkini ndiyo sababu Jaji Wilfred Dyansobera ameamua Mtendaji wa RITA afike mahakamani kutoa ushahidi.

Ni aibu kubwa maana pamoja na kupokea majina feki ya kibaraka Lipumba tuliamini angetimiza ahadi aliyokuwa ameitoa kwenye taarifa yake mwenyewe kwa umma kwamba atafanya uchambuzi na kujiridhisha kama yalivyo matakwa ya sheria na si kushirikiana na mhalifu Francis Mutungi ambaye RITA wanafahamu wazi kuwa ni mlalamikiwa kwenye kesi na amekwisha waingiza kwenye mgogoro na Mahakama kufuatia nyaraka za kughushi alozoambatanisha pamoja na hati ya kiapo kwenye shauri Na. 23/2016.

Katibu Mkuu ameandika barua tatu kati ya 31 Machi na 6 Juni, 2017 akiomba kukutana na Kabidhi Wasii Mkuu wa RITA, bila ya mafanikio yoyote. Katibu Mkuu ndiye mtunza kumbukumbu zote za wajumbe wa vikao vyote vya kitaifa na jinsi wanavyopatikana. Kitendo cha RITA kukataa kumpa nafasi Katibu Mkuu kukutana naye wakati akifanya hivyo kwa kibaraka Lipumba kunadhihirisha kuwa alichokifanya hakikuwa cha bahati mbaya bali alidhamiria. Ni dhahiri RITA wamejiunga na Jaji Francis Mutungi sio tu kuivuruga CUF bali kuzizamisha ndoto za Wazanzibari juu ya haki yao ya maamuzi waliyoyafanya Oktoba 25, 2015 kwa lengo la kuididimiza demokrasia nchini.

HATUA TUTAKAZOCHUKUA:

Baada ya kupata taarifa hizi kupitia Mahakama Kuu tarehe 21 Juni, 2017, Kamati ya Utendaji ya Taifa ilikutana mjini Zanzibar tarehe 22 Juni, 2017 na kuazimia yafuatayo:

1. Kufungua kesi dhidi ya RITA kwa kukiuka taratibu za Sheria ya Wadhamini (The Trustees' Incorporation Act Cap. 318) kama nilivyonukuu vifungu mbali mbali hapo juu, kwa kutojiridhisha juu ya uhalali wa majina ya Bodi ya Wadhamini ya CUF yaliyofikishwa kwake na iwapo yamefanywa na kikao halali cha Chama chenye mamlaka hayo kwa mujibu wa Katiba ya Chama.

2. Kuwasilisha maombi mbele ya Mahakama Kuu kuitaka isimamishe kesi nyengine zote tulizozifungua kuhusiana na kadhia hii hadi hapo shauri linalohusu uhalali wa maamuzi ya RITA litakapoamuliwa.

Ni imani yangu na imani ya CUF kikiwa ni chama chenye wanachama wapatao milioni mbili na mamilioni ya wafuasi hapa nchini kwamba Mahakama Kuu zitaona umuhimu wa kulitendea haki suala hili ili kuiepusha nchi yetu na mgogoro usio na sababu zaidi ya malengo ya muda mfupi ya baadhi ya watu wanaodhani kwamba kwa kuihujumu CUF watafanikiwa.

Asanteni sana kwa kunisikiliza.

HAKI SAWA KWA WOTE

Seif Sharif Hamad,
Katibu Mkuuu,
Chama Cha Wananchi (CUF),
28 Juni 2017, Dar Es Salaam


BODI FEKI YA LIPUMBA YA GONGA MWAMBA

UPDATES KUTOKA MAHAKAMA KUU LEO TAREHE 29/6/2017



MAHAKAMA YAPANGA KUSIKILIZA PINGAMIZI LA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI:

Leo mbele ya Mheshimiwa Jaji Wilfred Dyansobera amefanya maamuzi ya kuahirisha Shauri la Msingi Miscellaneous Civil Cause No. 21/2017 kuhusu wizi wa shilingi milioni 369 fedha za Ruzuku za Chama cha CUF uliofanywa na Lipumba na genge lake wakishirikiana na Msajili wa Vyama vya siasa nchini Jaji Franscis Mutungi mpaka Tarehe 6 July, 2017. Maamuzi hayo yameelezwa mbele ya Mahakama ya wazi (Open Court) iliyofurika wana NGANGARI wakiongozwa na Wabunge 40 wa CUF na kikosi makini cha ulinzi wa Chama Blue Guards. Hatua hiyo imefikiwa baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (Senior State Attorney) Wakili Msomi SILVESTER MWAKITALE – kuiomba Mahakama kuhairisha shauri hilo ili waweze kuwapatia nakala za Pingamizi (Copy of Preliminary Objection to be saved to Applicant-(THE REGISTERED TRSTEES OF THE CIVIC UNITED FRONT (CUF-CHAMA CHA WANANCHI). Upande wa Mawakili wasomi wa CUF ukiongozwa na JUMA NASSOR, HALFANI DAIMU NA HASHIMU MZIRAY ulikuwa hauna Pingamizi na Maombi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya kuweka pingamizi hilo na kukubaliana na kuagizwa na Mahakama kuwa kesho Tarehe 30/6/2017 nakala hizo wapatiwe Mawakili wa CUF na pingamizi hilo litasikilizwa Tarehe 6 July, 2017.

Katika hatua nyingine Mahakama Kuu haikuweza kufanyia kazi Maamuzi yake iliyoyatoa awali Shauri lilipoitwa mbele ya Jaji Tarehe 21/6/2017 juu ya kuwataka kufika Mahakamani Afisa wa RITA na Thomas Malima aliyejitambulisha kama Katibu wa Bodi ya Wadhamini aliyewasilisha barua ya kutaka Kufuta kesi zote zilizopo Mahakamani hapo kuleta ushahidi na kuthibitisha nyaraka zilizowasilishwa Mahakamani za kuteuliwa kwa ‘Bodi FEKI’ ya Wadhamini na pia kutaka kuwaondoa mawakili wanaoiwakilisha Bodi Halali ya Wadhamini ya CUF pamoja na kutaka kumuingiza Wakili Mpya atakaye iwakilisha ‘Bodi FEKI’ ya Lipumba na genge lake Mhe. Makubi Makubi. Kutosikilizwa kwa suala la maombi ya kufuta kesi limetokana na uwepo wa pingamizi la Mwanasheria Mkuu wa Serikali na hivyo kuamuriwa kuwa masuala hayo yatajadiliwa baada ya pingamizi hilo kusikilizwa na kutolewa maamuzi ndipo itaangaliwa kama kuna haja ya kuendelea na maombi hayo ya kufuta kesi hizo.

Mahakama Kuu imeendelea kuwatambua Mawakili wa Bodi Halali ya Wadhamini wa CUF inayoongozwa na Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad na kuiweka pembeni barua ya ‘Bodi FEKI’ ya Genge la Lipumba kutaka kubadilisha mawakili hao kwa kumuingiza wakili wao. Leo mawakili wa Lipumba na genge lake hawakuruhusiwa kushiriki katika kesi hiyo kwa kuwa si sehemu ya walalamikiwa (Respondents). Kesi hii inawahusu Bodi ya Wadhamini-CUF dhidi ya Mutungi na Mwanasheria Mkuu wa serikali.

Wakati huohuo CUF IKIWA NI TAASISI IMARA, YENYE VIONGOZI MAKINI tayari imeshachukua hatua za kutekeleza Maazimio ya Kikao Cha Kamati ya Utendaji Taifa kilichofanyika tarehe 23/6/2017 na kuongozwa na Mwenyekiti wake Maalim Seif Sharif Hamad katika Ofisi ndogo ya Makao Makuu Vuga, Zanzibar kushughulikia kisheria kuipinga Bodi FEKI ya lipumba kwa mujibu wa Sheria ya REGISTRATION INSOLVENCY AND TRUSTEESHIP AGENCY (RITA) THE TRUSTEES INCORPORATION ACT [CAP 318-R.E 2002] AN ACT TO PROVIDE FOR THE INCORPORATION OF CERTAIN TRUSTEES.

Article 26. “Application to decide question whether a person is a member of a corporate body or as to property When any question arises as to whether a person is a member of a body corporate or as to the vesting or divesting of any property under the provisions of this Act, any person interested in such question may apply to the High Court for its opinion on such question and notice of hearing shall be given to such persons and in such manner as the court shall think fit, and any opinion given by the court on an application under this section shall be deemed to have the force of a declaratory decree.” [s. 18]

Sheria hii inaeleza wazi kuwa “…kama kuna mtu yeyote ambaye hakuridhika na maamuzi ya RITA kuteua wajumbe wa Bodi ya Wadhamini sheria inampa haki ya kufungua mashtaka Mahakama Kuu na kupinga maamuzi ya RITA. Maamuzi ya Mahakama Kuu ndiyo yatakayo zingatiwa na kufuatwa kwa kuwa na nguvu ya kisheria.”

Pamoja na hilo wahusika wote walioshiriki kufoji nyaraka watapaswa kuitwa mbele ya Mahakama Kuu na kujibu kwanini wasitiwe hatiani na Kufungwa Jela kwa makosa hayo.

HAKI SAWA KWA WOTE

SALIM BIMAN
MKURUGENZI WA HABARI, UENEZI NA MAHUSIANO NA UMMA CUF-TAIFA
ZANTEL-0777414112
VODA-0752325227

MBARALA MAHARAGANDE
NAIBU MKURUGENZI WA HABARI, UENEZI NA MAHUSIANO NA UMMA CUF-TAIFA
maharagande@gmail.com
TIGO-0715 062577
VODA-0767 062577

CHAMA CHA Wananchi CUF kimesikitishwa kwa kudai kuwa kitendo cha Jeshi la Polisi kuwateka viongozi wa chama hicho takribani 20 mkoani Pwani.



Naibu Katibu Mkuu Uenezi Jumuiya ya Vijana Chama cha Wananchi CUF Mohamed Mahmoud Mahinda amedai hayo leo kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Facebook kuwa viongozi wa CUF katika maeneo ya Kibiti, Ikiwiri na Rufiji wametekwa na jeshi hilo na kupelekwa mahala pasipo julikana.

Kibiti, ikwiriri na rufiji itazamwe kwa jicho pana na la huruma!! #jeshi la polisi linawateka na kuwatesa viongozi wa cuf kwa faida ya nani??” Amehoji.
Kiongozi huyo amesema kuwa chama hicho kimekuwa mstari wa mbele kuhimiza, kuhamasisha na kulinda amani ya nchi, na kuiunga serikali vitendo vya kihalifu vya aina yoyote ile ni haramu katika chama cha cuf.
“Tunaposema jeshi la polisi na vyombo vyengine vya dola, vitumie uweledi katika kuwasaka na kuwakamata "wahalifu" tuna maanisha yoyote alie mhalifu achukuliwe hatua za kisheria kama zinavyopaswa kuchukuliwa bila ya kujali itikadi wala muelekeo wa KISIASA, DINI WALA KABILA, Maana UOVU hauna kabila, Dini wala itikadi ya kisiasa” Amefafanua.

Hali kadhalika amesema kitendo hicho cha Jeshi la Polisi kimewasikitisha juu ya yanayoendelea kufanywa Kibiti dhidi ya viongozi wa CUF kwani vimeanza kutoa ishara mbaya na kuonesha kuwa Jeshi la Polisi, kukosa uwezo wa kutosha katika kuwabaini waovu.

“ Jeshi la polii na vyombo vya dola wamekubali kuweka pembeni taaluma zao na kukubali kutumika kwa kuwaridhisha viongozi wa chama tawala. nasema haya nikimaanisha kwamba, haiyumkiniki uwateke viongozi wa cuf zaidi ya 20, uwapeleke kusikojulikana, (kinyume na sheria) uwatese "kinyama" uwadhalilishe utu wao kisha uwaachie warudi makwao wakiwa wahoi bin taaban!! kutokana na mateso walioyapata kutoka kwenye vyombo vinavyotegemewa kusimamia sheria za nchi yetu, kulinda raia na mali zao (bila ya ubaguzi wa aina yoyote). ni aibu na fedheha kubwa, unapoona jeshi la polisi na vyombo vya dola, vinawaaminisha raia kuwa vinapambana na uhalifu, huku wao wakiongoza, au wakifanya zaidi ya uhalifu (MATESO YA KINYAMA) dhidi ya Raia wasio na "HATIA"” Amebainisha Mahinda.
Kwa upande wa Kamanda mkuu wa Mkoa wa Pwani mara alipopigiwa simu leo na muandishi wa habari hizi majira ya saa kumi na moja jioni amesema hayupo tayari kuongelea suala hilo na hana taarifa kwani uongozi wa Jeshi la Polisi haujampa taarifa yoyote.

Kamanda huyo aliyeonekana hayupo tayari kuzungumza lolote, na kusema anafuatilia tuuhuma hizo licha ya kudai kuwa waandishi wengi wa habari leo wamempigia kutaka kujua ukweli wa tuhuma hizo.

HABARI ZILIZOJIRI LEO


Topics :
 
Support : ZENJIBARZA
Copyright © 2011. ACT WAZALENDO DIASPORA NETWORK - All Rights Reserved