Headlines News :
KARIBU CUF DIASPORA NETWORK - CUF HAKI SAWA KWA WOTE...TEGEMEA KILA JIPYA NA ZURI KUTOKA KWETU...LIKE PAGE YETU KWENYE FACEBOOK
Home » » KAULI YA WAZIRI KIVULI WA WIZARA YA MUUNGANO NA MAZINGIRA KUHUSU UCHAGUZI WA MAREJEO ZANZIBAR

KAULI YA WAZIRI KIVULI WA WIZARA YA MUUNGANO NA MAZINGIRA KUHUSU UCHAGUZI WA MAREJEO ZANZIBAR



Kambi Rasmi ya Upinzani inasema kuwa Dk. Ali Muhammed Shein hana uhalali wa kushika nafasi hiyo kwa sababu matokeo ya Uchaguzi wa Marejeo yana kila dalili kuwa yalikuwa ni ya kupanga kitakwimu. Kwa mfano katika Jimbo la Malindi, Dk Shein alipata kura 2,334 katika Uchaguzi wa Oktoba, lakini katika Uchaguzi wa Machi 20 akapata kura 5,873 ikiwa ni ongezeko la kura 3,539. Na kwa Jimbo la Mwanakwerekwe, Dk. Shein alipata kura 4,003 Oktoba, lakini akaibuka na kura 9,5,97 hapo juzi ikiwa ni ongezeko la kura 5,594. Majimbo yote hayo Maalim Seif aliongoza kwa kura Oktoba.
KAULI YA WAZIRI KIVULI WA WIZARA YA MUUNGANO NA MAZINGIRA KUHUSU UCHAGUZI WA MAREJEO ZANZIBAR
MARCH 31, 2016
Wana Habari
Tunaelewa sote kuwa Uchaguzi wa Marudio umefanyika Zanzibar na hivi sasa kuna harakati zinazoendelea kuunda Serikali kutokana na uchaguzi ambao umekosa uhalali wa kikatiba na kisheria.
Kambi Rasmi ya Upinzani inatamka wazi kuwa haitautambua uongozi huo wa Serikali ya Zanzibar na wala haitatoa ushirikiano wowote kwayo.
Uongozi mzima wa Serikali ya Zanzibar hauna uwezo wa kikatiba na kisheria kushiriki katika suala lolote la Muungano kwa sababu umekosa ridhaa ya Wazanzibar kutokana na kufutwa uchaguzi halali tarehe 28 Oktoba 28, 2015 na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya ZEC na pia hapakuwa na uhalali wa kikatiba na kisheria kuwepo kwa Uchaguzi wa Marejeo wa Machi 20, 2015.
Ieleweke kuwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar una athari ya moja kwa moja kwa upande wa Jamhuri ya Muungano, na Kambi Rasmi ya Upinzani inapinga kwa vyovyote vile uchaguzi huo kuhusishwa na mambo ya Muungano na itapinga na kulaani kitendo chochote kitachoelekeza hivyo.
Mnasaba wa Uchaguzi huo na Muungano ni katika maeneo yafuatayo ambayo kwa hali ilivyo kwa sasa yameingia katika mashaka na mgogoro wa kikatiba:
Pamoja na mamlaka ya Zanzibar kutajwa katika Katiba yake ya 1984 lakini pia yanatajwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano Kifungu cha 4 (2) na hapana shaka Katiba ya Jamhuri ya Muungano inatambua misingi ya demokrasia na kwa hivyo kwa utawala wa sasa kuingia madarakani kwa misingi isiyo halali na kufanya teuzi zinazohusu Baraza la Mawaziri, Mahakama na Baraza la Wawakilishi kunatia katika utata Katiba ya Jamhuri ya Muungano
Wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani hatutalikubali jambo hilo la kutiwa doa na kuipuuza Katiba ya Jamhuri ya Muungano na tutafanya kila njia kuonyesha kutoridhishwa kwetu kunajisiwa kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano
Uchaguzi Mkuu wa Marejeo na unyakuaji madaraka uliofanywa huko Zanzibar unakwenda kinyume kabisa na Malengo Muhimu na Msingi wa Mwelekeo wa Shughuli za Serikali kuhusu Serikali na Watu inasemwa katika Kifungu 8 (2)
“Muundo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar, au wa chochote kati ya vvyombo vyake
na uendeshaji wa shughuli zake utatekelezwa kwa kuzingatia
umoja wa Jamhuri ya Muungano na haja ya kukuza umoja wa
kitaifa na kudumisha heshima ya Taifa”
Uchaguzi wa kihuni uliofanywa Zanzibar huawezi kabisa kuwa unaakisi kifungu hiki cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano si kwa kuzingatia umoja wa kitaifa wala si kwa kudumisha heshima ya kitaifa.
Wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani watalisimamia jambo hili kwa nguvu zote kuhakikisha kuwa Uchaguzi wa Marejeo hautasimama mbele ya macho ya sheria na katiba na tukijua kuwa kutakuwa na tishio la kutetereka umoja wa kitaifa..
Wala Wabunge wa Kambi ya Upinzani hawatakubali Tanzania ipate aibu mbeleya wananchi wake lakini pia mbele ya macho ya kimataifa ambapo jina la Tanzania limekuwa kubwa, la kuaminika na la kusifika lakini linaweza kabisa kuharibiwa na aibu hii.
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano Kifungu 54 (1) Rais wa Zanzibar anakuwa sehemu ya Baraza la Mawaziri wa Muungano, na kwa hivyo atatarajiwa kula kiapo kushika nafasi hiyo.
Kambi Rasmi ya Upinzani inasema Dk. Ali Muhammed Shein hakushinda katika taratibu zinazoendana na misingi ya demokrasia kwanza kwa kuhusika kwa kiasi kikubwa kwa nguvu za kijeshi kupitia vitisho vilivyokuwa vikionekana na kujiri hata majeshi yetu kuvaa soksi za usoni.
Dk. Shein amechaguliwa katika kipindi ambacho kamatakamata ilikuwa kubwa ambapo katika kipindi kabla ya Uchaguzi wa Oktoba zaidi ya watu 100 walikamatwa na katika kipindi cha baada ya Oktob hadi Machi 20 watu zaidi ya 150 wamekamatwa pamoja na kukamatwa na kuhojiwa viongozi wa Chama cha Wananchi CUF.
Kambi Rasmi ya Upinzani inasema kuwa Dk. Ali Muhammed Shein hana uhalali wa kushika nafasi hiyo kwa sababu matokeo ya Uchaguzi wa Marejeo yana kila dalili kuwa yalikuwa ni ya kupanga kitakwimu. Kwa mfano katika Jimbo la Malindi, Dk Shein alipata kura 2,334 katika Uchaguzi wa Oktoba, lakini katika Uchaguzi wa Machi 20 akapata kura 5,873 ikiwa ni ongezeko la kura 3,539. Na kwa Jimbo la Mwanakwerekwe, Dk. Shein alipata kura 4,003 Oktoba, lakini akaibuka na kura 9,5,97 hapo juzi ikiwa ni ongezeko la kura 5,594. Majimbo yote hayo Maalim Seif aliongoza kwa kura Oktoba.
Kwa mujibu wa majimbo ambayo Tume ilikuwa imeyatangaza mpaka Oktoba 28, 2015 ambayo yalikuwa ni 31, ZEC inaonekana imemuongezea Dk. Shein kura za chini kabisa kwa kiasi cha 61 na za juu kabisa ni 5,594 jambo ambalo halielekei, halina mantiki na haliwezekani. Maana hata majimbo yote ya Pemba, Dk. Shein amepata kura za ziada.
Kwa mujibu wa Kifungu cha 66 (1) (c) Wajumbe 5 wa Baraza la Wawakilishi huingia katika Bunge la Jamhuri ya Muungano na hushiriki katika shughuli zote za Bunge kama vile kutunga sheria na kushiriki katika Kamati mbali mbali za Bunge.
Pia kama itampendeza Rais wa Jamhuri ya Muungano ana uwezo wa Kikatiba wa kumteua yoyote mmoja wao au wote kushika nafasi ya Uwaziri katika Jamhuri ya Muungano. Katika Uchaguzi huo wa Marejeo pia alipigiwa kura Mbunge pekee aliyekuwa amebakia Shamsi Vuai Nahodha wa Jimbo la Kijitoupele.
Ushiriki wa Wajumbe hao wa Baraza la Wawakilishi utalivunjia hadhi Bunge kwa kuwa watakuwa wanatokana na uchaguzi ambao haukukidhi vigezo vya kidemokrasia na inawezekana pia wakatoka katika majimbo ambayo hata Uchaguzi wa Oktoba majimbo wanayoyashika sasa yalikuwa yamekwenda kwa upinzania na kukabidhiwa vyeti vya ushindi na ZEC.
Kambi ya Upinzani Bungeni inapinga ushiriki wa Wajumbe hao wa Baraza la Wawakilishi kwa sababu wameshiriki katika zoezi zima la kubaka demokrasia pia wanatokana na Baraza la Wawakilishi ambalo uhalali wake unakwenda kinyume na matakwa ya katiba na sheria kwa kupokea Wajumbe ambao hawakupitia mchakato unaokubalika wa kikatiba.
Kambi ya Upinzani inaonya kuwa kutakuwa na migongano kadhaa ya Kikatiba katika suala hili bila ya kuwepo na ulazima isipokuwa itatokea kwa sababu Serikali ya Jamhuri ya Muungano imeamua kuitia kwenye mbeleko Serikali ya Drk Shein ili kuendeleza ubabe wa CCM kuitawala Zanzibar kwa nguvu na kudhihirisha nia ya Serikali ya Jamhuri kutokubali kuruhusu maamuzi ya kidemokrasia huko Zanzibar.
Kambi ya Upinzani inasema wazi kuwa kubebwa kwa utawala wa Dk. Shein kutozorotesha uimara wa Muungano na kuutia mtihani mkubwa hasa kwa vile matokeo ya Uchaguzi wa Marejeo yameshindwa kujenga mazingira ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambayo ilileta utulivu na kuupa pumzi Muungano, lakini hali hii mpya inatoa fursa kwa upinzani kudai kwa nguvu zote kuwepo kwa Katiba Mpya ambayo tutaidai kwa nguvu zetu zote.
Ally Saleh (Mbunge)
Waziri Kivuli wa Muungano na Mazingira
Machi 31, 2016
0715 4300 22 / 0777 4300 22
Share this article :

No comments:

Post a Comment

 
Support : ZENJIBARZA
Copyright © 2011. ACT WAZALENDO DIASPORA NETWORK - All Rights Reserved