ALIYEKUWA MGOMBEA WA URAIS WA ZANZIBAR KATIKA UCHAGUZI WA OKTOBA 2015 KUPITIA CUF CHAMA KIKUU CHA UPINZANI ZANZIBAR SEIF SHARIF HAMAD AMEMALIZA ZIARA YAKE YA KIKAZI UINGEREZA NA KUELEKEA UBELGIJI NA UHOLANZI.
Seif Sharif Hamad aliyekuwa mgombea urais wa Zanzibar katika uchaguzi wa Oktoba 2015 amemaliza ziara yake ya kikazi ya wiki moja nchini Uingereza na kuondoka kuelekea Ubelgiji na Uholanzi.
Akiwa nchi Uingereza Hamad alikuwa na vikao na wadau mbali wa masuala ya maendeleo na demokrasi kwa nchi za Afrika. Hamad alifanya mazungumzo ramsi na kamati ya wabunge wote ya bunge la makabwela la Uingereza kuelezea hali ya kisiasa Zanzibar baada ya Uchaguzi wa Oktoba 2015 ikiwa ni pamoja na hali tete ya usalama Zanzibar, ambapo alidai wafuasi wake wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya ukatili dhidi ya binaadamu na vikosi vya ulinzi na usalama vya serikali. Hamad pia amefanya mazungunzo na sekretariat ya Jumuiya ya Umoja wa Madola kwa mazungumzo yanayofanana na yale ya kamati ya vyama vyote ya bunge la makabwela la Uingereza.
Hamad pia alifika CHATHAM HOUSE mahali ambako pana historia kubwa na Tanzania, mahali hapa Julius Nyerere aliyekuwa Rais wa Tanganyika alifika kudai uhuru wa Tanganyika aidha pia Abeid Aman Karume aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar akifuatana na viongozi wengine wa vyama vya kupigania uhuru Zanzibar kutoka ASP, ZNP, na ZPP pia aliwahi kufika CHATHAM HOUSE kudai uhuru wa Zanzibar miezi michache kabla ya Uhuru wa Disemba 10, 1963.
Hamad akiwa Chatham House pia aliongozana na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza na Ireland Dr. Asha-rose Migiro pamoja na Mwambata wa Usalama katika Ubalozi wa Uingereza kutoka Zanzibar Juma Fum Sheha. Akiwa Chatham House, Hamad alipata fursa nyengine kuelekea kubakwa kwa demokrasia Zanzibar Oktoba 2015 mbele ya balozi wa Tanzania Uingereza tofauti na malengo ya kupata Uhuru yalioasisiwa na Chatham House mwaka 1963, pia alielezea ukatili dhidi ya binadaamu kwa wafuasi wake unaofanywa na vikosi vya ulinzi vya serikali aliyoiita sio halali.
Katika kikao hicho na hasa pale Hamad alipokuwa akimwaga ugali baada ya alichokidai kumwagwa kwa mboga Zanzibar, Balozi Migiro pamoja na Mwambata wa Usalama kutoka Zanzibar Juma Fum Shema katika ubalozi wa Tanzania Uingereza hawakuonekana kuwa na furaha wakati wote wa mazungumzo na kuwa kama kile wazungu wanachosema "been in the wrong place at the wrong time" au hapa Zanzibar wanaposema hawakuwa "hadhir" muda wote wa mazungumzo, na hasa pale picha zilipokuwa zikichukuliwa na wasaidizi wa Hamad.
Hamad pamoja na ujumbe aliofuatana nao waliondoka jana Uingereza kulekea Ubelgiji na Uholanzi kwa dhamira inayofanana na ziara yake ya Uingereza.
Chanzo : Mwandishi Wetu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment