THE CIVIC UNITED FRONT(CUF-Chama Cha Wananchi)
JUMUIYA YA VIJANA YA CHAMA CHA WANANCHI- CUF (JUVICUF)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUHUSU YANAYOJIRI NDANI YA CHAMA
09 Oct.2016
Waheshimiwa Waandishi wa Habari
Awali ya yote nitoe shukrani kwa vyombo vyote nchini kwa kuupasha habari umma wa watanzania kila uchao bila kuchoka pamoja na mazingira magumu ya kazi.
Pili, nianze moja kwa moja kuhusu yanayojiri ndani ya CUF kwa sasa kwa kusema JUVICUF kama Jumuiya ya Chama inaunga mkono maamuzi yote halali yaliyokwisha fanywa na mamlaka halali za Chama (BARAZA KUU LA UONGOZI)hivi karibuni ikiwemo kuwasimamisha na kuwafukuza baadhi ya wanachama akiwemo aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama Prof. Lipumba pamoja na maamuzi mengine.
Tatu, JUVICUF inasikitishwa na kikundi cha Vijana kinachojiita cha mkoa wa Dar es salaam wakati katika Katiba ya Chama CUF haina ngazi ya mkoa, kuibuka na kuongea na wanahabari wakati hawana mamlaka hayo.
Tunawasihi VIJANA wote wanachama wa CUF kuheshimu mamlaka za JUMUIYA YA VIJANA YA CHAMA na kuwa na nidhamu ambayo tumelelewa nayo ndani ya Chama chetu, kuliko kila mmoja kujiona ana ndevu kama Kambare kwa kutoa kashfa dhidi ya viongozi wa UKAWA akiwemo Mhe Mbowe na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi CUF Mhe Mtatiro tunawataka vijana hawa kuacha mara moja kutumika kukashifu watu wasio na hatia na badala wasitafute mchawi wakati wamemkumbatia.
JUVICUF inatoa wito kwa Vijana wote kuwa walinzi wa Chama dhidi ya maadui wa Chama wa ndani na nje kwani ni jukumu mama la kila mwanachama Kikatiba badala ya kushabikia ama kutumiliwa na maadui hao.
Aidha, JUVICUF inatoa wito mwingine kwa vijana wote kuheshimu uongozi halali wa Chama uliowekwa na mamlaka halali za Chama Kikatiba na si mamlaka nyingine yoyote nje ya Chama wala isiyojulikana ndani ya Katiba ya CUF.
JUVICUF pia inatumia fursa hii kuwaambia WAZANZIBAR wasiwe na hofu kabisa kwani ile haki yao iliyopokonywa ipo mbioni kurejea. CUF ni Chama cha kupigania haki hivyo abadani hakitayumbishwa na njama mbalimbali zinazoendelea za kutaka kututoa nje ya Agenda za kudai haki, CUF ni taasisi kubwa na inafahamu ktk jitihada za kudai haki hakuna 'ulelemama', hivyo wakati njama zinaendelea na jitihada za kurejesha haki Zanzibar nazo zipo pazuri na baadhi ya ushahidi jamii imeanza kuushuhudia.
JUVICUF inawaeleza maadui wa CUF na wapinga haki wote kuwa CUF ipo imara sana tofauti na wanavyojidanganya, tupo tayari kupambana nao nawao wanajua hilo, na tunawahakikishia CUF itaibuka mshindi ktk mapambano haya kwani Mungu yu pamoja na HAKI siku zote, na ndio maana CUF imekuwa mshindi mara zote yanapotokea mapambano dhidi yake na wahujumu HAKI. Hivyo hatuna wasiwasi.
Aidha JUVICUF Tunatoa wito kwa Vijana wote wa CUF nchini kutotoa ushirikiano wowote kwa prof. Lipumba ambae anatarajia kuanza ziara wiki ijayo katika mikoa ya kusini Lindi na Mtwara na Tanga katika lengo lile lile la kutaka kuongeza mpasuko ndani ya chama ili kuwapa maadui wetu wa kisiasa nafasi ya kutupiku .
Lengo walilo nalo kwa sasa dhidi ya chama chetu ni wazi kwamba wanataka kuvuruga na kukidhoofisha chama
Mwisho JUVICUF inatoa rai kwa wadau wa maendeleo, wanachama wote wa CUF mahala popote walipo kuunganisha nguvu ktk vita hii dhidi ya HAKI, kutokubali kugawanywa na wahujumu HAKI na kuwa nao makini na njama zao ovu ikiwemo kuripoti ktk mamlaka halali za Chama zinazoongozwa na KAMATI YA MUDA YA UONGOZI chini ya Julius Mtatiro, Katani A. Katani na Severine Mwijage njama zozote ovu dhidi ya Chama Chetu.
HAKI SAWA KWA WOTE
Hamidu Bobali (MB)
Mwenyekiti JUVICUF
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
- TAMKO LA UMOJA WA KLABU ZA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA JUU YA KUTEKWA KWA MWANDISHI WA HABARI WA SAUTI YA UJERUMANI ( DW ) SALMA SAID.
- CUF wamuandikia barua Mwenyekiti wa ZEC
- Sera ya kunena na Kutenda ya Wana CUF
- (no title)
- Ufungaji wa Kampeni ya uchaguzi mdogo wa Dimani.
- Salam kwa Mkururinza wa Zanzibar
No comments:
Post a Comment