Headlines News :
KARIBU CUF DIASPORA NETWORK - CUF HAKI SAWA KWA WOTE...TEGEMEA KILA JIPYA NA ZURI KUTOKA KWETU...LIKE PAGE YETU KWENYE FACEBOOK
Home » » WATETEZI WA UDHALIMU HUU UNAKUJA NA EXCUSE YA KIBITI, SORAGA, PADRI etc

WATETEZI WA UDHALIMU HUU UNAKUJA NA EXCUSE YA KIBITI, SORAGA, PADRI etc

Na Ally Saleh Mbunge wa Malindi, Zanzibar 
 Kama kufumbua na kufumbua Bwana Ali Juma Suleiman ametangulia mbele ya haki. La, bora niseme ametangulizwa mbele ya haki kwa kudhulumiwa na makundi ambayo yameshafanyia udhalimu mwingi wanachama wa chama kikuu cha upinzani The Civic United Front. Marehemu Ali ameshafika na hesabu yake kwa Mola wake imeshaanza tokea jana, na wengi tunaamini amekufa shahidi kwa kuwa amedhulumiwa. Lakini pia amekufa shahidi kwa kuwa amekufa akipigani haki, usawa wa nchi jambo ambalo waliomuua hawalitaki kabisa. Hata akiwa kitandani siku moja kabla ya kufariki aliendelea kusimama katika anachokiamini na alisema kuwa “Tusikubali kabisa kuonewa.” Na amini alikuwa akikariri Wimbo wa Taifa wa CUF ambao amekuwa akiuimba kwa miaka kadhaa tokea alipoingia chama ambacho wanachama wake wamepitia madhila mengi sana.

 Marehemu Ali ameungana na wengine wengi waliouliwa kwa sababu tu ya imani zao za siasa ikiwa ni pamoja na waliokufa kimya kimya baada ya vifo kama hivi vya kupigwa toka zama za Janjawidi hadi sasa zama za Mazombie na wale ambao waliouliwa katika maandamano ya kudai haki yao katika tarehe 26 na 27 Januari 2001. Wapo kwa makundi makubwa waliokufa kwa uonge na ukiwa baada ya dhuluma za kupigwa na kuteswa na kutiwa vilema, wako ambao wamebaki na vilema vyao wakichechemea na wengine wakiugua kisaklojia kutokana na yaliowakuta na kutwisha. Yote haya ambapo, CUF imekusanya majina ya maelfu ya wahanga wa tokea Janjawidi hadi sasa Mazombie, vitendo vyengine vikifanywa mchana kweupe, na majina na ushahidi kupelekwa Serikalini ikiwa na pamoja na Bungeni, lakini hakuna lilokuwa. Jeshi la Polisi halijawahi hata siku moja angalau kujaribu kuchukua hatua na wakibanwa wanasema wanaodhulumiwa wapekele ushahid. Kesi kwa maelfu ziko kwenye madaftari ya vituo vya Polis lakini hata moja haijafanyiwa uchuguzi.

 Tumelisikia Jeshi la Polisi likikana kabisa kuwepo kwa Mazombie na kusema wao haiwajui, wala hawaamini kuwa wapo. Wananchi wamekuwa wakifanya kama ada tu kwenda vituo vya Polisi lakini wanajua kuwa Jeshi la Polisi halina uwezo wala nia ya kuwakamata watendaji hao wa maovu dhidi ya wenzao. Binafasi nimekuwa nikilishikia bango suala hilo la Mazombie na hivi karibuni niliwasilisha majina ya wanachama na wapenzi wa cuf zaidi ya 350 ambao wameripoti matukio ya kupigwa, kuteswa na madhila mengine waliofanyiwa, lakini hakuna kilichofanywa na Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba. Mwigulu alitafuta suluhu kwa kutoa kauli wakati akitaka bajeti yake ipitishwe baada ya kushika shilling, lakini hadi leo hajanitafuta kabisa na wala sifikiri atanitafuta maana ni wazi kuwepo kwa Mazombi kunaungwa mkono na CCM na kuna maslahi na chama hicho.
 Tulipopendekeza Bunge liiunde kamati ya uchunguzi kuhusu jambo hilo, kwa kweli lilrahishishwa na kutupiliwa mbali kama mzigo uso na maana, na likazimwa kabisa. Pamoja na yote yanayotokea haijawahi kabisa kutokea Serikali ya Zanzibar wala ile Serikali ya Muungano kutoa kauli yoyote ile ya kulaani vitendo vya makundi hayo, ambayo kwa vitendo wanavyofanya ni kudhihirisha kuwa nchi haina udhibiti na usalama. Basi SMZ na SMT wako radhi isemwe na ionekane hivyo. Pili Serikali hizo mbili kwa kukaa kimya na sawa na kusema wako tayari isemwe kuwa inaridhia matendo hayo yafanywe kwa raia wengine ilhali, vitendo hivyo ni vya kibaguzi na vinavyolengwa watu maalumu katika jamii kwa sababu ya imani zao za kisiasa.

 Pia ni sawa na Serikali hiyo kukiri kuwa vyama vingi haviko katika haki na mizania yake na kwamba kuwa CUF ni kosa, ni kupotea na hakuwezi kukubalika na ndio maana ya adabu, mateso, vipigo na dhulma zote. Kwamba kijana mwenye nguvu zake na aliyeshiba maziwa ya mama yake wa CCM ana haki ya kumfanya lolote lile mwana CUF na hakuna litakalokuwa. Hadhi waliopewa Mazombi naweza kusema kuwa ni sawa na kundi la mgambo ambalo linaweza kufanya litakavyo na hakuna viwavyo. NI ishara kuwa lipo juu ya sheria. Nchi imefanya bidii zote kuzima vitendo vilivyokuwa vikifanywa Kibiti lakini kwa upande wa Zanzibar hakuna lilofanywa na zaidi wanakingwa na hata kukataa ( denial) kuwa kundi au makundi hayo yapo. Viongozi wa CUF kwa muda wote wamekuwa wakiwaambia wanachama wao wasichokozeke na wala wasirudishe mapigo wanayopigwa na huku wakijua kuwa wanachama wao wanajeruhiwa, wanatiwa vilema na kama hivyo wanauawa.


 Jeshi la Polisi, Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Muungano wamekuwa wakiwachukulia poa wanachama wa CUF na hivyo kuwapa kichwa Mazombi kuwa wanachofanya kina baraka zote zao na hakuna litakalokuwa. Maziko ya kiongozi Ali Juma Suleiman akisindikizwa na umati ambao haujawahi kutokea na ulimpeleka safari yake kwa miguu hadi makaburini, ni ishara kuwa CUF wanao watu wa kurudisha mapigo na hata kulipa kisasa na kama si hivyo basi angalau kusimama kusema kuwania sasa basi. Tusiombee yule aonewaye kufika siku ya kusema palipofika basi, na siioni siku hiyo kuwa iko mbali tena. Naamini Mazombi hata kama wanaungwa mkono kama wanavyopewa nguvu, sioni kuwa ni wengi kuzidi ummawa CUF uliochoka na dhulma zao. Watu wamekuwa wakionewa toka 1992 kuliporudishwa vyama vingi kwa maana ya wapenzi wa mabadiliko na tokea ilipoanzishwa CUF 1995. Mashtaka ya kubuni ili watu wawekwe selo au jela ni kwa maelfu mengi Ieleweke tu wanaochoka kuonewa wakijetetea basi Jeshi la Polisi ambalo haliwezi kuchukua hatua na Serikali ya Zanzibar na ile ya Muungano wanao nyamazia kimya, wasije kugeuza lawama kwa walioonewa angalau wakinyanyua mkono kujikinga au kurudisha kofi kwa kofi. Tuombe tusifike huko lakini kutanzwa kukizidi lolote laweza kuwa.
Share this article :

No comments:

Post a Comment

 
Support : ZENJIBARZA
Copyright © 2011. ACT WAZALENDO DIASPORA NETWORK - All Rights Reserved