Katibu
Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amesema
anakusudia kuifanya Zanzibar kuwa visiwa vya fursa za biashara na ajira
kwa wananchi.
Maalim Seif ambaye tayari Chama chake kimeshamteua rasmi kuwa mgombea wa nafasi ya Urais wa Zanzibar kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015, ameeleza hayo katika viwanja vya Kibandamaiti, wakati akihutubia mkutano wa hadhara ulioandaliwa na chama hicho kwa ajili ya mapokezi ya mgombea huyo.
Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba (kulia), akimtambulisha rasmi mgombea wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, kwa wananchi wa Zanzibar. |
Maalim Seif ambaye tayari Chama chake kimeshamteua rasmi kuwa mgombea wa nafasi ya Urais wa Zanzibar kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015, ameeleza hayo katika viwanja vya Kibandamaiti, wakati akihutubia mkutano wa hadhara ulioandaliwa na chama hicho kwa ajili ya mapokezi ya mgombea huyo.
Amesema
Zanzibar inazo fursa nyingi za kuweza kunyanyua kipato cha wananchi, na
kwamba ataweka kipaumbele katika kuziibua na kuziendeleza fursa hizo.
Maalim
Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amesema katika
kujenga mazingira bora ya uwekezaji, ataisimamia ipasavyo Mamlaka ya
vitega uchumi, ili kuondosha vizingiti vinavyokwamisha uwekezaji nchini.
Amefahamisha
kuwa wapo wafanyabiashara wengi wa ndani na nje ya nchi wenye nia ya
kuwekeza miradi mikubwa ya kiuchumi, lakini wamekuwa wakipata usumbufu,
jambo ambalo ameahidi kulishughulikia muda mfupi baada ya kuingia
madarakani.
Sambamba
na hilo, Maalim Seif amesema iwapo atachaguliwa kuiongoza Zanzibar,
atahakikisha kuwa Zanzibar inakuwa na shirika lake la ndege ndani ya
kipindi cha mwaka mmoja, ili kurahisisha shughuli za kibiashara ikiwemo
Utalii.
Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na wananchi. |
Amesema
hatua hiyo itakwenda sambamba na uboreshaji wa huduma za viwanja vya
ndege, ambavyo vitaweza kutoa huduma bora kitaifa na kimataifa.
Aidha
amesema chini ya uongozi wake iwapo atapata ridhaa ya kuongoza nchi
baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015, ataitangaza Zanzibar kuwa bandari
huru, sambamba na kujenga bandari mpya itakayotoa huduma bora kwa
mwambao wa Afrika Mashariki.
Katika
hatua nyengine Maalim Seif amesema anakusudia kuongeza viwango vya
mishahara kwa wafanyakazi wote, pamoja na kuzingatia maslahi ya wastaafu
na wazee wasiojiweza.
Akizungumzia
kuhusu mafuta, Maalim Seif amesema anakusudia kuanzisha Wizara ya
Mafuta na Gesi ili kurahisisha uchimbaji wa nishati hiyo, itakayoondosha
hali ya umasikini katika visiwa vya Zanzibar.
Maalim
Seif pia alizungumzia hali ya amani na utulivu nchini, na kueleza kuwa
amani ya kweli itapatikana iwapo vyombo vinavyohusika vitatoa haki kwa
wananchi wote.
Mapema
akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti wa CUF Taifa Prof. Ibrahim
Haruna Lipumba, amesema Baraza Kuu la Uongozi la CUF limeshawika
kumuidhinisha Maalim Seif kuwa mgombea Urais wa Zanzibar, kutokana na
uwezo na nia ya dhati ya kuwatumikia wazanzibari.
Amesema
viongozi waliopo madarakani wana dhamana na wajibu mkubwa wa
kuhakikisha kuwa uchaguzi mkuu ujao unafanyika katika hali ya amani,
sambamba na kuheshimu maamuzi ya wananchi katika uchaguzi huo.
Chanzo: Haki na Umma
No comments:
Post a Comment