Mgombea urais wa Zanzibar
kupitia chama cha wananchi-CUF- Maalim Seif Sharrif Hamad amesisitiza kuwa anahitaji siku 100 tu kwa Zanzibar kuwa na mamlaka yake kuhusu
sera na uchimbaji wa mafuta kisiwani humo.
Maalim ametoa msimao huo wakti akiwahutubia wanachama,wapenzi na wananchi
waliohudhuria katika mkutano wa kampeni
za urais zinazoendelea visiwani Zanzibar uliofanyika Sebleni nyumba za
wazee mjini unguja ambapo
amesmea CUF haijachupia agenda ya mafuta
na sera hiyo bado iko
mikononi mwa uopande wa pili wa
muungano.
Mgombea huyo wa urais wa Zanzibar ambaye pia ni katibu mkuu
wa CUF na makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar aliwahakishia umati huo na
wananchi kwa ujumla kuwa serikali ya CUF itakuwa na mfumo mzuri wa kuhakikisha
haina shida ya soko la ajira na kusema seriklai yake itapigania kubadilisha
hali ya maisha ya wananchi.
Katika mkutano huo Maalim Seif alitumia fursa ya kuwanadi
wagombea ubunge,uwakilishi na udiwani wa chama hicho kwa majimbo ya magomeni na
amani katika hatua nyengine pamoja na kuwepo wagombea 14 wa urais bado vyama
vya CCM na CUF ndivyo vianvyonekana kuwa na mikutano mingi ya kampeni huku
badhi ya vyama vyemngine havijannza kampeni zao za urais.
No comments:
Post a Comment