TAARIFA RASMI:
Kundi la WAHUNI lililotumwa kuvamia Mkutano Mkuu wa CUF na kuuvuruga limeendelea na vikao vyake jana na leo na limefikia maazimio kuwa litavamia OFISI KUU ya CUF Buguruni ili kumrejeshea Lipumba Uenyekiti kwa kumleta ofisini kwa nguvu.
Kesho kundi hilo litakuwa nyumbani kwa Prof. Lipumba ili kukubaliana naye juu ya mpango wa namna ya kutekeleza azma hiyo. Na kwa namna ambavyo Prof. amekuwa hatabiriki huenda akakubali mpango huo kama alivyokubali kuletwa na kuvamia na kuvuruga mkutano mkuu maalum wa CUF.
Hakika, kama Lipumba atakubali kutekeleza kitendo hicho atakuwa ni Profesa wa ajabu kupata kutokea hapa duniani. Namuombea sana Lipumba ambaye ni "Alhaji" aanze kujitambua na nafsi yake imsute kwamba haya anayoyapanga na kuyatekeleza yanaidhalilisha sana familia yake, wasomi wenzake, wanasiasa wenzake na kuvunja kabisa heshima kubwa ambayo aliijenga kwa miaka 20.
Kila mmoja wetu umuombee Lipumba.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
- TAMKO LA UMOJA WA KLABU ZA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA JUU YA KUTEKWA KWA MWANDISHI WA HABARI WA SAUTI YA UJERUMANI ( DW ) SALMA SAID.
- CUF wamuandikia barua Mwenyekiti wa ZEC
- Sera ya kunena na Kutenda ya Wana CUF
- (no title)
- Ufungaji wa Kampeni ya uchaguzi mdogo wa Dimani.
- Salam kwa Mkururinza wa Zanzibar
No comments:
Post a Comment