Home »
NEWS
» SWALI: Je ni kweli baraza la madiwani halmashauri ya manispaa ya Kinondoni limevunjwa?
SWALI: Je ni kweli baraza la madiwani halmashauri ya manispaa ya Kinondoni limevunjwa?
JIBU: Ni kweli baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni limevunjwa rasmi jana tarehe 16/09/2016 na mchakato wa Uchaguzi wa Meya utaanza mara moja Jumatatu tarehe 19/09/2016 kwa Halmashauri zote mbili, Ubungo na Kinondoni. Mchakato huu utatumia wiki mbili hadi kukamilika na kupata ma mayor wapya.
SWALI: Je kuna tatizo la kiutendaji lililopelekea baraza hilo kuvunjwa?
JIBU: Hakuna tatizo lolote la kiutendaji lililosababisha kuvunjwa kwa halmashauri ya Kinondoni isipokua ni utaratibu tu wa kisheria wa wilaya mbili kutokua ndani ya halmashauri moja, kama ilivyoainishwa katika sheria ya Serikali za mitaa namba 8 ya mwaka 1982 (The Local Government (Urban Authorities) Act, 1982).
Kwa mujibu wa sheria hii, wilaya mbili haziwezi kuwa ndani ya halmashauri moja, lakini halmashauri mbili au zaidi zinaweza kuwa ndani ya wilaya moja.
Ikumbukwe kwamba wilaya ya Kinondoni ilikua na halmashauri moja ya Kinondoni. Mwanzoni mwa mwaka huu Rais Magufuli akaitangaza Ubungo kuwa wilaya mpya, lakini halmashauri ikabaki kuwa moja. Yani Mayor wa Kinondoni akawa mmoja lakini wakuu wa wilaya wawili (wa Ubungo na Kinondoni). Kisheria hii si sahihi.
Kwahiyo baada ya kupatikana wilaya mpya ya Ubungo, ilibidi baraza la madiwani Kinondoni liwe nulified, yazaliwe mabaraza mawili (la Kinondoni na Ubungo) maana halmashauri zinapaswa kuwa mbili tofauti.
Kwahiyo mchakato huu utakapokamilika, Kinondoni itakua wilaya moja yenye halmashauri moja na majimbo mawili ya uchaguzi (Kinondoni na Kawe). Maana yake ni kwamba Kinondoni itakua na Mkuu wa wilaya mmoja, Mayor mmoja na wabunge wawili.
Na Ubungo nayo itakuwa ni wilaya moja yenye halmashauri moja na majinbo mawili ya uchaguzi (Ubungo na Kibamba). Maana yake ni kwamba DC atakuwa mmoja, Mayor mmoja na wabunge wawili.
Kwa hiyo tunategemea kupata Mayor mpya wa Ubungo na Mayor mpya Kigamboni. Maana yake ni kwamba halmashauri za jiji la Dar zinaongezeka kutoka 3 zilizopo sasa na kuwa 5, ambazo ni Halmashauri ya Manispaa Kinondoni, halmashauri ya manispaa Temeke, halmashauri manispaa Ilala, na Halmashauri mpya za manispaa Ubungo na Kigamboni.
Jambo la msingi hapa ni kwamba Halmashauri mpya ya Ubungo nayo itaongozwa na UKAWA maana ndio wenye viti vingi vya udiwani. Katika baraza la Kinondoni lililovunjwa UKAWA walikua na viti vya udiwani 38 (CHADEMA 29 na CUF 9), huku CCM wakiwa na viti 15 tu.
Katika mgawanyo uliotokea inasadikiwa takribani madiwani 18 wa UKAWA watakuwa kwenye halmashauri mpya ya Ubungo, huku CCM ikihama na madiwani 7 tu. Wanaodhaniwa kubakia Kinondoni UKAWA ni 20 na CCM 8. Kwahiyo haihitaji muujiza kujua kwamba UKAWA inaenda kuongoza halmashauri zote hizi mbili.
Mayor wa Kinondoni atatoka UKAWA na wa Ubungo pia atatoka UKAWA. Hii itafanya UKAWA kuwa na mamayor wanne kati ya sita wa halmashauri zote za Dar (za manispaa na jiji).
Mayor wa jiji Dar (UKAWA)
Mayor Ilala (UKAWA)
Mayor Kinondoni (UKAWA)
Mayor Ubungo (UKAWA)
Mayor Temeke (CCM)
Mayor Kigamboni (possibly CCM)
Mchakato utakapokamilika, Kigamboni nayo itafuata utaratibu kama wa Ubungo katika kumpata Mayor na kuunda Halmashauri mpya.
Hii ni fursa kwa madiwani wa UKAWA ktk halmashauri mpya ya Ubungo na halmashauri nyingine zinazoongozwa na UKAWA kuwatumikia wananchi wao kwa ufanisi, na kuwaletea maendeleo wanayotarajia.
Kila la heri rafiki yangu Boniface Jacob Mstahiki mayor wa zamani wa manispaa ya Kinondoni ambaye unaenda kuwa Mayor mpya wa manispaa ya Ubungo maana kata yako ya Ubungo ipo wilaya mpya. Pia Niwaatakie heri madiwani wote wa UKAWA katika halmashauri ya Kinondoni, kwenye mchakato wao wa kutuletea Mayor mpya wa manispaa hiyo. Naamini atakua mtu makini na mwenye weledi katika utumishi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
- CUF wamuandikia barua Mwenyekiti wa ZEC
- TAMKO LA UMOJA WA KLABU ZA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA JUU YA KUTEKWA KWA MWANDISHI WA HABARI WA SAUTI YA UJERUMANI ( DW ) SALMA SAID.
- Sera ya kunena na Kutenda ya Wana CUF
- (no title)
- Toleo la Annur June 23
- Ufungaji wa Kampeni ya uchaguzi mdogo wa Dimani.
- Salam kwa Mkururinza wa Zanzibar
No comments:
Post a Comment