Headlines News :
KARIBU CUF DIASPORA NETWORK - CUF HAKI SAWA KWA WOTE...TEGEMEA KILA JIPYA NA ZURI KUTOKA KWETU...LIKE PAGE YETU KWENYE FACEBOOK
Home » , » MAHAKAMA YAIPIGA NA CHINI HOJA ZA SERIKALI DHIDI YA KESI YA CUF

MAHAKAMA YAIPIGA NA CHINI HOJA ZA SERIKALI DHIDI YA KESI YA CUF

Mahakama yatupa hoja za serikali ya kesi ya CUF


MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imekubaliana na hoja za Wakili wa Wabunge wanane wa Chama cha Wananchi CUF ambao ubunge umetenguliwa baada ya kuvuliwa uanachama, na sasa pingamizi la muda litaanza kusikilizwa Jumatatu,


Awali serikali iliwasilisha mapingamizi matatu ambapo jana iliondoa moja na kubakia mawili likiwamo la kuiomba mahakama isiingilie mhimili wa Bunge kwa kuzuia wabunge hao wasiapishwe.
Mapingamizi mawili ya serikali nayo yalitupwa na mahakama huku serikali ikiambiwa kinachofanyika siyo kuingilia mhimili wa Bunge.
Kwa mujibu wa mahakama, shauri dogo namba 479 litaanza kusikilizwa jumatatu ambalo litakuwa na mambo makuu saba likiwamo hoja ya kuzuia wabunge wanane wa CUF kuapishwa.

Jaji Lugani Mwandambo amekubali hoja za Wakili wa wabunge hao, Peter Kibatala kwamba shauri hilo limefunguliwa kwa kifungu sahihi na kwamba litaendelea kusikilizwa.

Mahakama hiyo imezitupa hoja tatu za serikali, ikiwamo kutaka chombo hicho kutupilia mbali hoja za kuzuia kuapishwa wabunge hao.Mwandambo alisema kinachofanyika kwa sasa katika kesi hiyo siyo kuingilia mahakama kama hoja ya serikali ilivyowasilisha hoja hiyo.

Chanzo cha wabunge hao kuvuliwa ubunge kimetokana na Chama cha Wananchi (CUF), chini ya Profesa Ibrahim Lipumba kuwavua uanachama.*



Zaidi soma hapa chini Tamko la Chama

TAARIFA RASMI YA CUF JUU YA MAAMUZI YALIYOTOLEWA LEO TAREHE 25/8/2017 NA MAHAKAMA KUU
Mbele ya Jaji Lugano Mwandambo leo tarehe 25/8/2017 imetoa maamuzi madogo juu ya Pingamizi lillowekwa na Mwanashera Mkuu wa Serikali katika shauri la madai namba 479/2017.
Katika mapingamiz hayo matatu , moja likuwa ni uwezo wa mahakama kulisikiliza shauri hilo. Pili, Kifungu 65CPC kilchotumika ilidaiwa kuwa sio sahihi, tatu, Hoja ya Muhimili wa Bunge kutoingiliwa.
kwa upande wa Mawakili wote wa Lipumba wameshindwa kuwasilisha maelezo ya mapingamizi yao kwa maandishi (written submission) kama ilivyopangwa ratiba hiyo tarehe 15/8/2017. kwamba tarehe 18/8/2017 walalamikiwa wenye mapingamizi (Lipumba na Wenzake, AG, NEC, BUNGE, Wakurugenzi wa Halmashauri Temeke na Ubungo) wawe wamewasilisha mapingamizi yao na kuwa-save waleta maombi/Applicant (wabunge) na Applicant wanapaswa kujibu mapingamizi hayo mpaka tarehe 21/8/2017 na AG kuwasilisha hoja zake tena tarehe 22/8/2017 na leo tarehe 25/8/2017 imepangwa kutolewa maamuzi.
Mahakama ilianza kwa kueleza historia ya shauri hilo tangu kuwasilshwa mahakamani hapo na kwamba walalamikiwa wengine hawakuweza kuwasilisha mapingamizi yao kama ilivyopangwa. aidha AG aliondoa pingamizi namba moja hapo juu kwa kutotoa maelezo ya pingamizi hilo katika hoja za maandishi walizowasilisha.
MAAMUZI YA MAHAKAMA LEO:
1. Kifungu kilichotumika ni sahihi na hivyo kulitupa pingamizi namba moja. kwa kuwa mwanasheria ameshindwa kueleza ni kifungu kipi kinastahiki kama sio hicho.
2. Kuhusu hoja ya muhimili wa bunge kutoingiliwa Mhe. Jaji ameeleza Dhana ya mgawanyo wa madaraka kwa Bunge,(Parlamentary) Mahakama (Judicial) na Serikali (Executive)
(The concept of separation of power) na kwamba mahakama haijaombwa kuingilia muhimili wa bunge bali kuna mgogoro wa uongozi kati ya CUF na wanachama wake waliokuwa na nafasi za uongozi wakiwa ni wabunge. kazi ya Bunge ni kutunga sheria na Mahakama ni Kutafsiri Sheria kwa mujibu wa katiba 107A. Mahakama haiwezi kuingilia muhimili wa bunge pale unapotekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria isipokuwa kama unakwenda nje ya mamlaka yake kwa mujibu wa sheria.
Hakuna muhimili wa dola ambao hauwezi kupingwa mahakamani. hakuna kifungu cha sheria makhsusi knachoizuia mahakama kutekeleza wajibu wake. mgawanyo wa madaraka kwa mujibu wa ibara ya 4(1) (4) cha katiba. umeelezwa vizuri. HAYA NDIO BAADHI YA SEHEMU YA NUKUU ZA MAAMUZI YALIYOTOLEWA NA MAHAKAMA.
Mahakama imepanga Jumatatu Tarehe 28 August, 2017 kusikiliza maombi Rasmi yaliyowasilishwa mahakamani hapo kuomba Zuio na kuhifadhi hali iliyopo sasa. (Temporary Injunction and to maintain Status Quo).
MWISHO;
Shauri la MSINGI NAMBA 143/2017 LIMEPANGWA KUTAJWA/KUSIKILZWA TAREHE 31/8/2017
CUF NI TAASISI IMARA, YENYE VIONGOZI MAKINI.
HAKI SAWA KWA WOTE
Imetolewa leo Tarehe 25/8/2017
Na. Kurugenzi ya Habari, Uenezi Na Mahusiano Na Umma-CUF Taifa
SALIM BIMAN
MKURUGENZI-07774141212
MBARALA MAHARAGANDE
NAIBU MKURUGENZI
0715 062577 au 0767 062 577
maharagande@gmail.com
Share this article :

No comments:

Post a Comment

 
Support : ZENJIBARZA
Copyright © 2011. ACT WAZALENDO DIASPORA NETWORK - All Rights Reserved