Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF , Maalim Seif Sharif Hamad
Kwa Ufupi:
Maalim alihudhuria masomo ya shule ya msingi katika Shule ya Msingi Uondwe iliyoko Pemba na kisha akasoma shule ya wavulana ya Wete (Shule zote hizi za msingi amesoma katikati ya mwaka 1950 – 1957) kabla ya kujiunga na elimu ya Sekondari (Kidato cha kwanza hadi cha nne) kati ya mwaka 1958 – 1961 katika Shule ya Sekondari ya Kumbukumbu ya Mfalme George, iliyoko katika Kisiwa cha Unguja, na pia akaendelea na kidato cha tano na sita katika sekondari hii kati ya mwaka 1962 -1963.
Kwa Ufupi:
Maalim alihudhuria masomo ya shule ya msingi katika Shule ya Msingi Uondwe iliyoko Pemba na kisha akasoma shule ya wavulana ya Wete (Shule zote hizi za msingi amesoma katikati ya mwaka 1950 – 1957) kabla ya kujiunga na elimu ya Sekondari (Kidato cha kwanza hadi cha nne) kati ya mwaka 1958 – 1961 katika Shule ya Sekondari ya Kumbukumbu ya Mfalme George, iliyoko katika Kisiwa cha Unguja, na pia akaendelea na kidato cha tano na sita katika sekondari hii kati ya mwaka 1962 -1963.
Historia yake
Maalim
Seif Sharif Hamad ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Zanzibar
na pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF. Maalim Seif alizaliwa
Oktoba 22, 1943 huko Nyali, Mtambwe katika Wilaya ya Wete iliyoko
kisiwani Pemba.
Maalim alihudhuria masomo ya shule ya
msingi katika Shule ya Msingi Uondwe iliyoko Pemba na kisha akasoma
shule ya wavulana ya Wete (Shule zote hizi za msingi amesoma katikati ya
mwaka 1950 – 1957) kabla ya kujiunga na elimu ya Sekondari (Kidato cha
kwanza hadi cha nne) kati ya mwaka 1958 – 1961 katika Shule ya Sekondari
ya Kumbukumbu ya Mfalme George, iliyoko katika Kisiwa cha Unguja, na
pia akaendelea na kidato cha tano na sita katika sekondari hii kati ya
mwaka 1962 -1963.
Pamoja na kufaulu vizuri sana masomo
ya kidato cha sita, Maalim Seif hakwenda chuo kikuu kwa sababu serikali
ilimtaka afanye kazi serikalini ili kuziba nafasi za kazi zilizokuwa
wazi kutokana na kuondoka kwa wingi kwa Waingereza kurudi nchini kwao.
Maalim aliajiriwa kama mwalimu kwa miaka tisa, yaani 1964 – 1972 na
alifundisha Sekondari Fidel Castro iliyoko Pemba na Chuo cha Ualimu cha
Lumumba kilichoko Unguja.
Mwaka 1972 aliruhusiwa
kujiunga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kusomea shahada ya kwanza ya
Sayansi ya Siasa, Usimamizi wa Umma na Uhusiano wa Kimataifa, alihitimu
shahada hii mwaka 1975 akiwa mmoja wa wanafunzi waliofaulu vizuri sana
kiasi kwamba chuo kilipenda abakie kufundisha, jambo ambalo
hakukubaliana nalo.
Maalim Seif alianza kujifunza na
hata kuingia katika masuala ya uongozi mkubwa wa serikali mwaka 1975,
alipoteuliwa kuwa Msaidizi Binafsi wa Rais wa Zanzibar wakati huo (Aboud
Jumbe) ambapo aliifanya kazi hiyo hadi mwaka 1977. Mwaka 1977
akateuliwa kuwa Waziri wa Elimu wa Zanzibar na akatumika katika nafasi
hiyo hadi mwaka 1980.
Mwezi Februari 1984 akateuliwa
kuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Zanzibar (Cheo sawa na cha Waziri
Mkuu wa Tanzania, kimajukumu). Maalim Seif amekuwa Waziri Kiongozi wa
Zanzibar katika kipindi chote cha uongozi wa Rais Mwinyi kama Rais wa
Zanzibar, na mwaka 1985 alipochaguliwa Rais Idris Abdul Wakil kuongoza
Zanzibar, bado Maalim Seif aliteuliwa kuwa Waziri Kiongozi na
alishikilia wadhifa huo hadi Januari 1988 alipoondolewa katika baraza la
mawaziri na baadaye kufukuzwa ndani ya CCM. Kwa hivyo, Maalim Seif
amekuwa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar kuanzia mwaka 1977-1988.
Tokea
Maalim Seif aondolewe katika utumishi wa uongozi wa juu wa Zanzibar
(akiwa mwanachama wa CCM), imemchukua miaka zaidi ya 22 ndipo tena
amerejea kileleni, sasa akiwa ni Makamu wa Kwanza Rais wa Zainzibar,
lakini akitokea Chama Cha Wananchi CUF.
Kisiasa, Maalim
Seif amepitia katika nafasi nyingi sana. Mwaka 1977 – 1988 alikuwa
Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM lakini pia mwaka 1977 – 1987 alikuwa ni
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM huku mwaka 1982 – 1987 akiteuliwa
kuongoza Idara ya Uchumi na Mipango ya Chama cha Mapinduzi (kitaifa).
Maalim
Seif na wenzake kadhaa walifukuzwa kutoka Chama Cha Mapinduzi mwaka
1988 baada ya kushindana kimsimamo na CCM na alikuwa mmoja wa
waanzilishi wa vuguvugu la “Kamahuru” la Zanzibar lililoungana na CCW
(Chama Cha Wananchi) ya Tanzania Bara na kuunda Chama Cha Wananchi CUF
ambapo yeye (Maalim Seif) alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa kwanza
wa CUF akihudumu katika wadhifa huo hadi mwaka 1999 alipochaguliwa kuwa
Katibu Mkuu wa CUF hadi hivi sasa.
Kimataifa, Maalim
amewahi kushikilia wadhifa mkubwa sana kimataifa kati ya mwaka 1997 -
2001, alikuwa Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa “The Unrepresented Nations
and Peoples Organization (UNPO)” (Nchi zisizowakilishwa na Mashirika ya
Watu) - Tafsiri yangu. Hii ni taasisi ambayo makao makuu yake yapo
jijini The Hague nchini Uholanzi na inahusisha mataifa zaidi ya 50
duniani na watu ambao siyo wajumbe wa Umoja wa Mataifa, yaani ambao
wakienda Umoja wa Mataifa wanakuwa na hadhi ya waangalizi tu (au
wageni).
Baadhi ya nchi mwanachama wa umoja huu ni pamoja na Taiwan, Tibet na Zanzibar. Lakini pia amewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Vyama vya Kiliberali Duniani kati ya mwaka 2002 – 2003.
Baadhi ya nchi mwanachama wa umoja huu ni pamoja na Taiwan, Tibet na Zanzibar. Lakini pia amewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Vyama vya Kiliberali Duniani kati ya mwaka 2002 – 2003.
Maalim Seif amemuoa Aweina Sinani Masoud tangu mwaka 1977 na wana watoto watatu.
Mbio za ubunge
Maalim
Seif si mgeni katika masuala ya uwakilishi na Ubunge. Yeye ni mmoja
kati ya Watanzania wachache waliobahatika kupitia nafasi zote za
kuwawakilisha wananchi kwa pande zote mbili za muungano.
Mwaka
1977 – 1982 amekuwa Mbunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, lakini pia kati ya mwaka 1977- 1980 na 1984 – 1988 amekuwa ni
Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Kwa muktadha huu anafahamu
vizuri shughuli za kibunge na kiuwakilishi na amepata kuzishiriki
vilivyo.
Mbio za urais
Maalim
Seif, “Rais wa Mioyo ya Wazanzibari” ameshiriki katika mbio za urais za
Zanzibar mara nne bila mafanikio, lakini zikiwa chaguzi ambazo hata
waangalizi wa kimataifa wamekuwa bila kupepesa macho wakisisitiza kuwa
zina walakini mkubwa.
Uchaguzi Mkuu wa Kwanza
alioshiriki ni ule wa mwaka 1995 akigombea urais wa Zanzibar kwa tiketi
ya CUF. Maalim Seif alikosa kuingia ikulu kwa sababu “ilitangazwa” kuwa
amepata asilimia 49.76 ya kura zote dhidi ya Rais Salmin Amour
“Komandoo” aliyekuwa na asilimia 50.24. Pamoja na CUF kupinga matokeo
hayo, pia Waangalizi wa kimataifa walisisitiza kuwa uchaguzi ule ulikuwa
“uchafu”.
Mwaka 2000 tena Maalim Seif alitaka kuingia
Ikulu lakini haikutokea. Ilitangazwa kuwa amepata asilimia 32.96 ya kura
zote dhidi ya asilimia 67.04 za Amani Karume wa CCM. Huu ni uchaguzi
ambao pia hata waangalizi wa kimataifa waliutaja kama moja ya chaguzi
zisizofuata kabisa misingi ya kidemokrasia huku ukandamizaji wa vyama
vya upinzani hususani CUF ukiwa wazi. Kwa mfano, waangalizi wa Jumuiya
ya Madola waliutaja uchaguzi huu kama “Shambels” (Msambaratiko) –
Tafsiri yangu.
Kwenye uchaguzi wa mwaka 2005, Maalim
Seif aliangushwa kwa mara nyingine na Rais Amani Karume wa CCM, Safari
hii Maalim akitangaziwa kupata asilimia 46.07 dhidi ya 53.18 za Karume.
CUF ilikataa matokeo haya na ikatangaza kutomtambua Karume kama Rais wa
Zanzibar. Waangalizi wa kimataifa kama Jumuiya ya Madola na Taasisi ya
Demokrasia ya Marekani ziliweka wazi kuwa uchaguzi ule haukuwa huru na
wa haki, baadhi ya maandiko yanasisitiza kuwa huwenda hii ndiyo sababu
iliyofanya Marekani (kama nchi) isitume hata balozi wake au mwakilishi
kushuhudia sherehe za kumwapisha Karume (mara ya pili).
Maalim
Seif alitupa karata ya nne ya kusaka urais wa Zanzibar mwaka 2010 mara
hii akipambana na Dk Ali Mohamed Shein ambapo pia Tume ya Taifa ya
Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) ilitangaza kuwa Dk Shein amemzidi Maalim Seif
kwa kura 4471. Ndiyo kusema kuwa Maalim Seif alipata asilimia 49.1
dhidi ya asilimia 50.1 za Shein. Uchaguzi wa mwaka huo pia ulionekana
kuwa na kasoro nyingi sana.
Kwa mwaka huu 2015 tayari
Maalim Seif Sharif Hamad amekishachukua fomu na kupitishwa na CUF kuwa
mgombea urais wa Zanzibar kwenye uchaguzi wa mwaka huu n CUF upande wa
Zanzibar inaonekana imejipanga sana kushiriki kwenye uchaguzi mwaka huu,
huwenda kuliko wakati wowote ule kama alivyowahi kuandika Ismail Jussa,
Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa chama hicho, kwenye ukurasa wake wa
“Facebook”.
Nguvu yake
Kwanza,
Maalim Seif ndiye kiongozi mwenye uzoefu mkubwa sana wa kisiasa kati ya
viongozi wa upinzani, akianza utumishi wa juu kabisa serikalini
alipokuwa kijana mdogo tu na ameendelea hadi kufikia nyadhifa za juu
kabisa. Uzoefu wake ni silaha tosha kuwa ukimpa uongozi wa nchi wala
hawezi kwenda kuanza kujifunza, tayari anajua wapi aanzie na kwa nini.
Lakini
nguvu kubwa na sifa maalum ya Maalim Seif ni kuwa Msimamo thabiti na
usioyumba. Kiongozi huyu ana misimamo yake juu ya baadhi ya masuala na
ikifika hapo hawezi kuyumba. Mathalani, hivi karibuni amekuwa na msimamo
wa dhati wa kudai mamlaka kamili ya Zanzibar, msimamo huu umekuwa
ajenda kubwa sana katika siasa za Zanzibar na ni moja ya masuala ambayo.
Lakini pia watu waliowahi kufanya naye kazi.
Katika
siasa ukiwahi kupitia kifungo cha kisiasa, kunyanyaswa moja kwa moja na
kuteswa kwa sababu ya msimamo wako kidemokrasia, jambo hili hugeuka na
kuwa ushujaa. Maalim Seif alipofukuzwa CCM mwaka 1988 alikaa muda mfupi
tu kabla ya kuanza kuwa mfungwa.
Alikamatwa mwezi Mei 1989 na kufikishwa mahakamani akishitakiwa kwa kukutwa na nyaraka za siri za serikali (mashtaka ya kupikwa). Alikaa gerezani kwa miaka mitatu (hadi mwaka 1991). Wananchi na marafiki wan chi yetu kimataifa walipoomba sana Maalim Seif na wenzake watolewe gerezani, Rais wa Zanzibar wakati huo, Salmin Amour “Komando”, aliwakebehi hadharani kuwa “wanapaswa kukaa huko huko, hawataoza kwa sababu wao siyo mapapai!”
Alikamatwa mwezi Mei 1989 na kufikishwa mahakamani akishitakiwa kwa kukutwa na nyaraka za siri za serikali (mashtaka ya kupikwa). Alikaa gerezani kwa miaka mitatu (hadi mwaka 1991). Wananchi na marafiki wan chi yetu kimataifa walipoomba sana Maalim Seif na wenzake watolewe gerezani, Rais wa Zanzibar wakati huo, Salmin Amour “Komando”, aliwakebehi hadharani kuwa “wanapaswa kukaa huko huko, hawataoza kwa sababu wao siyo mapapai!”
Lakini
pia mwaka 2000 alikamatwa tea na kupewa mashtaka ya kumshambulia askari
polisi na kumyang’anya bunduki (kosa la kubambikizia pia). Shitaka hili
lilitupwa na mahakama mwaka 2003. Maalim Seif ni mmoja wa viongozi
wakubwa sana wa kisiasa hapa Tanzania ambaye amewahi kukaa gerezani muda
mrefu sana. Jambo hili ni umadhubutu muhimu kwa mtu anayetaka kuongoza
nchi. Kama ameweza kukaa gerezani kwa ajili ya demokrasia na akatoka
akaendelea kuipigania, inamjenga katika sifa ya uvumilivu na kutokata
tamaa.
Udhaifu wake
Kwanza,
Maalim Seif amekuwa na uungwana uliopita kiasi katika mazingira ambayo
Zanzibar inahitaji kufanya maamuzi magumu. Uungwana huu kisiasa unaweza
kuwa na shida siku za mbele. Hivi karibuni, Mzee anayeheshimika sana
Zanzibar na mtu wa karibu na Maalim Seif alitangaza hadharani kuwa mwaka
2010 “yeye Mzee Moyo ndiye alitumwa kwenda kumuomba Maalim Seif
ayakubali matokeo ya uchaguzi”. Ndiyo kusema kuwa matokeo yale yalikuwa
yamechakachuliwa na ilimpasa Maalim Seif ayakubali ili kuiepusha
Zanzibar kuingia kwenye shari. Pamoja na mzee Moyo kurudia kauli hii
mara kadhaa, Si Maalim Seif au CUF vimewahi kukanusha.
Kama
hiyo hali ni ya kweli basi, tutegemee tena mwaka huu CCM itakuja na
mpango huo huo wa kupora ushindi Zanzibar na kutegemea uungwana na
huruma ya Maalim Seif. Hakika ifikie wakati Maalim Seif awaachie
Wazanzibari wenyewe waamue hatma yao ikiwa wataendelea kufanyiwa ujanja
kwenye masanduku ya kura. Uungwana wa namna hii unazika haki za
kidemokrasia za wapiga kura na si jambo linalopaswa kujirudia tena na
tena kwa kiongozi mkubwa.
Tulipokuwa katika Bunge
Maalum la Katiba na nadhani waliokuwa wakifuatilia matangazo ya bunge
hilo kupitia kwenye luninga walikuwa wakisikia kwa uwazi kabisa wajumbe
wa BMK ambao ni viongozi wakubwa wa CCM kutoka Zanzibar wakitamka
waziwazi kuwa hawawezi kuuachia Urais wa Zanzibar kwenye masanduku ya
kura. Hii ina maana kuwa CCM itaendelea kupora ushindi wa kidemokrasia
wa Wazanzibari kwa kutumia uungwana na busara za Maalim Seif. Jambo hili
likiendelea litahesabiwa tena kama udhaifu mkubwa sana.
Nini kimefanya apitishwe
Jambo
la kwanza lililofanya CUF impitishe kugombea urais ni kwa sababu yeye
ni Mhimili wa siasa za Zanzibar kitaifa na kimataifa. Huwezi kutaja
mustakabali wa Zanzibar na Wazanzibari bila kumtaja kiongozi huyu,
amehusika katika sehemu kubwa za mabadiliko kadhaa tangu alipokuwa ndani
ya CCM na hata alipohamia upinzani. Hali hii nadhani imeivutia CUF na
kuona kuna haja ya kuendelea kumpa nafasi.
Lakini
sababu ya pili nadhani ni kwa sababu amegombea Urais mara nne zilizopita
huku ndiye pekee akionekana bado ana mvuto na ukubalikaji mkubwa zaidi
kuliko mwanachama mwingine wa CUF. Hadi sasa CUF haina mgombea mwenye
sifa, uwezo, uzoefu na umaarufu au umashuhuri kama wa Maalim Seif.
Nadhani chama hicho kimempitisha kikitegemea kwamba yeye peke yake kwa
sasa ndiye anaweza kuaminiwa sana na wananchi kiasi cha kuweza kupigiwa
kura na kupata ushindi.
Nini kingeweza kumwangusha
Jambo
moja ambalo lingemkwamisha Maalim Seif kuwa mgombea urais wa CUF upande
wa Zanzibar ni ikiwa yeye mwenyewe angeamua kupumzika au kutogombea.
Kwa hali ya kisiasa ya Zanzibar ilivyo “chanya” kwake, sikutegemea kuwa
angeliweza kutopitishwa, na labda sana angetokea mwanachama mwingine wa
CUF mwenye sifa, uwezo na vigezo kwa upande wa Zanzibar, ambaye hadi
sasa sijamuona.
Mpango B kama asingepita
Mipango kama mitatu hivi inaweza kufuatwa na Maalim Seif ikiwa asingepitishwa kugombea urais;
Mpango
wa kwanza ni Kuendelea na wadhifa wake wa kiserikali aliona sasa hivi
pamoja na kuendelea na uongozi wa CUF ambao unapaswa kukamilika mwaka
2019. CUF bado inamhitaji kiongozi huyu na nadhani bado serikali ya
Zanzibar inamhitaji zaidi kiutumishi.
Lakini jambo la
pili ni uimarishaji wa maridhiano na utangamano wa Wazanzibari.
Ikumbukwe kuwa Maalim Seif ni mmoja wa waasisi wawili wa Maridhiano ya sasa yanayoifanya Zanzibar iwe kwenye utulivu na amani ya sasa. Naamini kuwa angekuwa na jukumu la kujipanga kuanza kusimamia masuala ya utangamano wa Wazanzibari kwa vitendo, ikiwemo kuanzisha taasisi maalumu ambazo zingeendelea kufanya naye kazi kwa lengo la kuimarisha mustakabali wa Zanzibar.
Ikumbukwe kuwa Maalim Seif ni mmoja wa waasisi wawili wa Maridhiano ya sasa yanayoifanya Zanzibar iwe kwenye utulivu na amani ya sasa. Naamini kuwa angekuwa na jukumu la kujipanga kuanza kusimamia masuala ya utangamano wa Wazanzibari kwa vitendo, ikiwemo kuanzisha taasisi maalumu ambazo zingeendelea kufanya naye kazi kwa lengo la kuimarisha mustakabali wa Zanzibar.
Lakini lingine ambalo nadhani
ni ajenda yake ya kudumu ni kupigania Zanzibar yenye mamlaka kamili.
Ajenda hii naamini ingeendelea kuwa mikononi mwa Maalim Seif na
wanachama wake kwa sababu imekuwa na “mashiko makubwa” na kwa
wazanzibari wanaweza kuona kuwa inahitaji kuendelezwa na walioianzisha
akiwemo yeye mwenyewe. Namuona akiipigania ajenda hii hata ikiwa
atachaguliwa kuingia Ikulu.
Hitimisho
Vijana
ambao hawakuwahi kufanya kazi na Maalim Seif wamekosa kujifunza uongozi
thabiti kutoka kwa mtu ambaye anajua uongozi unafanywaje. Maalim Seif
ni Mwalimu wa Siasa na Uongozi na anajua muda gani afanye nini ili
kuendelea kuweka utulivu mahali anapoongoza.
Nakumbuka
wakati anatangaza kumtambua tena Rais Karume, vikao vya chama vilitoa
baraka za jambo hilo lakini vikiwa na hofu kubwa ya nini kitakachotokea.
Maalim Seif aliihimili hali ile, akamtambua Karume, akatengeneza
maridhiano na Wazanzibari wakamuelewa. Ni nadra sana kwa dunia ya sasa
kupata viongozi wanaokubalika, kuheshimika na kuaminiwa na wafuasi wao,
kama ilivyo kwa Maalim Seif.
Maalim Seif si mtu wa
mambo makuu sana, mara nyingi utamkuta yumo mitaani kabisa akiwatembelea
wagonjwa huku na kule, wazee na watu wasiojiweza. Staili yake ya
uongozi ni ya kuamini kuwa watu wa chini wanahitaji msaada na faraja
kubwa ya uongozi. Namna anavyosimamia ajenda muhimu ndani ya Zanzibar
huku misimamo yake ikiwa wazi ni karata muhimu kwake kuzidi kuaminiwa na
huwenda kukabidhiwa dola.
Mimi namtakia kila le heri kiongozi huyu, katika safari yake ya kurejesha hadhi ya Zanzibar na Wazanzibari wote kwa ujumla.
Chanzo: Mwananchi
Chanzo: Mwananchi
No comments:
Post a Comment