Dar es Salaam.
Mjumbe wa Iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Humphrey Polepole amesema yupo tayari kufanya kampeni za kumpinga mgombea urais wa Chadema na Ukawa, Edward Lowassa kwa madai kuwa ana doa linalomzuia kuwania nafasi hiyo.
Mjumbe wa Iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Humphrey Polepole amesema yupo tayari kufanya kampeni za kumpinga mgombea urais wa Chadema na Ukawa, Edward Lowassa kwa madai kuwa ana doa linalomzuia kuwania nafasi hiyo.
Polepole
ameibuka kuwa maarufu tangu kumalizika kwa Bunge la Katiba, akishiriki
kwenye midahalo kadhaa kuhusu mchakato wa kuandika Katiba mpya,
akitofautiana na msimamo wa CCM wa kubadilisha Rasimu ya Katiba.
Akizungumza
na Mwananchi jana, Polepole alisema Lowassa anayeungwa mkono na vyama
vya NCCR-Mageuzi, Chadema, CUF na NLD vinavyounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa), ana tuhuma za ufisadi na ni mmoja wa makada wa CCM
walioipinga Rasimu ya Katiba.
Polepole alisema msingi
wa kuzaliwa kwa Ukawa ni kutaka Katiba mpya yenye maoni ya wananchi,
hivyo Chadema kumpokea Lowassa ni sawa na kukiuka misingi hiyo.
“Nimeshirikiana
na Ukawa na viongozi wao kama Watanzania kuhakikisha Taifa letu
linapata Katiba mpya na inayotokana na maoni ya wananchi. CCM ambao
walikuwa ndiyo wana mkakati na wenye maamuzi ya mwisho katika kukwamisha
maoni ya wananchi. Watu hao (wa CCM) hawastahili kupewa uongozi iwe
ndani ya CCM au hata ndani ya Ukawa,” alisema.
“Hawana
dhamira njema na Taifa letu, watuhumiwa mengine nitaelewa, lakini kwenye
la Katiba nilikuwepo na ninajua mchango wao wa kutukwamisha. Niliweka
maoni yangu kwamba CCM ikiwachagua hao nitapiga kampeni ya kuwakataa.
Hawakupita CCM na mmoja wapo ni Lowassa.”
Alisema amepoteza imani na Ukawa kwa kukubali kuikiuka misingi ambayo awali waliisimamia.
“Nina
haki ya kutokubaliana na msimamo wa Ukawa na ikibidi nitasimama na
kupiga kampeni ya kumkataa mgombea wao wa urais,” alisema.
Katika
Bunge la Katiba, wajumbe kutoka CCM walilazimisha kuondolewa kwa baadhi
ya mapendekezo kwenye Rasimu ya Katiba, ikiwa ni pamoja na pendekezo la
kutaka muundo wa Muungano uwe wa serikali tatu.
No comments:
Post a Comment