UPDATES KUTOKA MAHAKAMA KUU LEO TAREHE 29/6/2017
MAHAKAMA YAPANGA KUSIKILIZA PINGAMIZI LA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI:
Leo mbele ya Mheshimiwa Jaji Wilfred Dyansobera amefanya maamuzi ya kuahirisha Shauri la Msingi Miscellaneous Civil Cause No. 21/2017 kuhusu wizi wa shilingi milioni 369 fedha za Ruzuku za Chama cha CUF uliofanywa na Lipumba na genge lake wakishirikiana na Msajili wa Vyama vya siasa nchini Jaji Franscis Mutungi mpaka Tarehe 6 July, 2017. Maamuzi hayo yameelezwa mbele ya Mahakama ya wazi (Open Court) iliyofurika wana NGANGARI wakiongozwa na Wabunge 40 wa CUF na kikosi makini cha ulinzi wa Chama Blue Guards. Hatua hiyo imefikiwa baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (Senior State Attorney) Wakili Msomi SILVESTER MWAKITALE – kuiomba Mahakama kuhairisha shauri hilo ili waweze kuwapatia nakala za Pingamizi (Copy of Preliminary Objection to be saved to Applicant-(THE REGISTERED TRSTEES OF THE CIVIC UNITED FRONT (CUF-CHAMA CHA WANANCHI). Upande wa Mawakili wasomi wa CUF ukiongozwa na JUMA NASSOR, HALFANI DAIMU NA HASHIMU MZIRAY ulikuwa hauna Pingamizi na Maombi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya kuweka pingamizi hilo na kukubaliana na kuagizwa na Mahakama kuwa kesho Tarehe 30/6/2017 nakala hizo wapatiwe Mawakili wa CUF na pingamizi hilo litasikilizwa Tarehe 6 July, 2017.
Katika hatua nyingine Mahakama Kuu haikuweza kufanyia kazi Maamuzi yake iliyoyatoa awali Shauri lilipoitwa mbele ya Jaji Tarehe 21/6/2017 juu ya kuwataka kufika Mahakamani Afisa wa RITA na Thomas Malima aliyejitambulisha kama Katibu wa Bodi ya Wadhamini aliyewasilisha barua ya kutaka Kufuta kesi zote zilizopo Mahakamani hapo kuleta ushahidi na kuthibitisha nyaraka zilizowasilishwa Mahakamani za kuteuliwa kwa ‘Bodi FEKI’ ya Wadhamini na pia kutaka kuwaondoa mawakili wanaoiwakilisha Bodi Halali ya Wadhamini ya CUF pamoja na kutaka kumuingiza Wakili Mpya atakaye iwakilisha ‘Bodi FEKI’ ya Lipumba na genge lake Mhe. Makubi Makubi. Kutosikilizwa kwa suala la maombi ya kufuta kesi limetokana na uwepo wa pingamizi la Mwanasheria Mkuu wa Serikali na hivyo kuamuriwa kuwa masuala hayo yatajadiliwa baada ya pingamizi hilo kusikilizwa na kutolewa maamuzi ndipo itaangaliwa kama kuna haja ya kuendelea na maombi hayo ya kufuta kesi hizo.
Mahakama Kuu imeendelea kuwatambua Mawakili wa Bodi Halali ya Wadhamini wa CUF inayoongozwa na Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad na kuiweka pembeni barua ya ‘Bodi FEKI’ ya Genge la Lipumba kutaka kubadilisha mawakili hao kwa kumuingiza wakili wao. Leo mawakili wa Lipumba na genge lake hawakuruhusiwa kushiriki katika kesi hiyo kwa kuwa si sehemu ya walalamikiwa (Respondents). Kesi hii inawahusu Bodi ya Wadhamini-CUF dhidi ya Mutungi na Mwanasheria Mkuu wa serikali.
Wakati huohuo CUF IKIWA NI TAASISI IMARA, YENYE VIONGOZI MAKINI tayari imeshachukua hatua za kutekeleza Maazimio ya Kikao Cha Kamati ya Utendaji Taifa kilichofanyika tarehe 23/6/2017 na kuongozwa na Mwenyekiti wake Maalim Seif Sharif Hamad katika Ofisi ndogo ya Makao Makuu Vuga, Zanzibar kushughulikia kisheria kuipinga Bodi FEKI ya lipumba kwa mujibu wa Sheria ya REGISTRATION INSOLVENCY AND TRUSTEESHIP AGENCY (RITA) THE TRUSTEES INCORPORATION ACT [CAP 318-R.E 2002] AN ACT TO PROVIDE FOR THE INCORPORATION OF CERTAIN TRUSTEES.
Article 26. “Application to decide question whether a person is a member of a corporate body or as to property When any question arises as to whether a person is a member of a body corporate or as to the vesting or divesting of any property under the provisions of this Act, any person interested in such question may apply to the High Court for its opinion on such question and notice of hearing shall be given to such persons and in such manner as the court shall think fit, and any opinion given by the court on an application under this section shall be deemed to have the force of a declaratory decree.” [s. 18]
Sheria hii inaeleza wazi kuwa “…kama kuna mtu yeyote ambaye hakuridhika na maamuzi ya RITA kuteua wajumbe wa Bodi ya Wadhamini sheria inampa haki ya kufungua mashtaka Mahakama Kuu na kupinga maamuzi ya RITA. Maamuzi ya Mahakama Kuu ndiyo yatakayo zingatiwa na kufuatwa kwa kuwa na nguvu ya kisheria.”
Pamoja na hilo wahusika wote walioshiriki kufoji nyaraka watapaswa kuitwa mbele ya Mahakama Kuu na kujibu kwanini wasitiwe hatiani na Kufungwa Jela kwa makosa hayo.
HAKI SAWA KWA WOTE
SALIM BIMAN
MKURUGENZI WA HABARI, UENEZI NA MAHUSIANO NA UMMA CUF-TAIFA
ZANTEL-0777414112
VODA-0752325227
MBARALA MAHARAGANDE
NAIBU MKURUGENZI WA HABARI, UENEZI NA MAHUSIANO NA UMMA CUF-TAIFA
maharagande@gmail.com
TIGO-0715 062577
VODA-0767 062577
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
- Uchaguziwa Mwenyekiti mpya wa CUF leo
- Taarifa kwa vyombo vya habari
- Maalim Seif na Fimbo ya Mussa
- Kituko cha Sheha na dada yangu
- CUF Zanzibar Yamtaka Rais Magufuli Aondoshe Majeshi yake Zanzibar
- MAAAMUZI YA BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA LA THE CIVIC UNITED FRONT (CUF - CHAMA CHA WANANCHI) KUHUSIANA NA HUJUMA ZA DOLA DHIDI YA CUF
No comments:
Post a Comment