Headlines News :
KARIBU CUF DIASPORA NETWORK - CUF HAKI SAWA KWA WOTE...TEGEMEA KILA JIPYA NA ZURI KUTOKA KWETU...LIKE PAGE YETU KWENYE FACEBOOK
Showing posts with label PICHA. Show all posts
Showing posts with label PICHA. Show all posts

CUF Wanawake wawapa 'take-care' Mutungi, Lipumba


Huku wakisubiri hukumu ya kesi zao zilizoko mahakamani dhidi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, na Profesa Ibrahim Lipumba, Jukwaa la Wanawake la CUF linamuonya Jaji Mutungi kuwa pakitokezea lolote baya kwenye nchi atahusika moja kwa moja


 

NDUNGAI NI NYOKA ANETAFUNA MKIANI

SERIAKLI YA CCM INAVYOJIKANYAGA LIPUMBA NA SAKAYA SIO WANCHAMA WA CUF ni mamluki walionunuliwa na CCM kuisambaratisha CUF kwa k usaidiwa na Msajili wa vyama , BRELA na Ofisi ya Speaker kutumika kuvuruga demokrrasia na kuzuia mabadiliko ndani ya nchi

Katibu Mkuu wa Chama cha CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema kwamba hatua ya Spika kuwavua ubunge , udiwani na kuteua wengine wapya inalenga kudhoofisha kambi ya wabunge wa CUF na Ukawa. Amesema Watanzania wanapaswa wajikumbushe kwamba hata kama hicho kinachoitwa ‘kuwafukuza uanachama’ wabunge halali wa CUF kingekuwa kiko sawa, hatua kama hiyo hufuata taratibu zote za kisheria na kikanuni za Bunge kujiridhisha kwanza. “ Spika Job Ndugai anadhani Watanzania ni vichaa wamuamini kuwa alishachukua hatua ya kujiridhisha kuwa wabunge wanane wa Chama cha Wananchi (CUF) wamefukuzwa uanachama kulingana na taratibu za chama hicho na hivyo wamekosa sifa za kuendelea na Ubunge. Ndani ya siku moja?” amehoji Maalim. Ameongeza kuwa Spika amejiridhisha vipi ikiwa hata hakuwasiliana na Katibu Mkuu wa Chama ambaye kwa mujibu wa Katiba ya CUF ndiye Mtendaji Mkuu wa shughuli za chama na pia kwa nafasi hiyo ndiye katibu wa vikao vya Mkutano Mkuu wa Taifa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama? Amesema yeye kama katibu, alimuandikia Spika Ndugai barua, Jumanne, Julai 25 akimueleza kwamba hilo lililoitwa Baraza Kuu la Uongozi la CUF halikuundwa na wajumbe halali wa Baraza Kuu. “Angekuwa na nia ya kweli ya kutaka kujiridhisha si hapo ndipo pangekuwa pa kuanzia kwa kuwepo kile wanasheria wanachokiita shaka inayoweza kuingia akilini yaani ‘reasonable doubt’?’’ amehoji. Hata hivyoa amesema Spika Ndugai aliyapuuza yote hayo kwa sababu ni kinyume na mkakati wa Dola wa kuihujumu CUF na kuua demokrasia Tanzania. Hapo ndipo Spika Job Ndugai alipolifikisha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

MAAAMUZI YA BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA LA THE CIVIC UNITED FRONT (CUF - CHAMA CHA WANANCHI) KUHUSIANA NA HUJUMA ZA DOLA DHIDI YA CUF

Image may contain: 1 person
BARAZA Kuu la Uongozi la Taifa lilipokea, kujadili na kufanya maamuzi kuhusu ajenda moja tu iliyowasilishwa kwake na Kamati ya Utendaji ya Taifa ambayo ilikuwa ni: • Taarifa kuhusu kile kinachoitwa kuwavua uanachama Wabunge wanane (8) na Madiwani wawili (2) wa Viti Maalum kupitia CUF kilichotangazwa kufanywa na Ibrahim Lipumba na kikundi chake ikiwa ni mwendelezo wa hujuma za Dola dhidi ya Chama cha CUF. Baada ya mjadala wa kina, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa linapenda kutoa maazimio yafuatayo kuhusiana na tukio hilo na mwendelezo wa vitendo na matukio mengi ya hujuma yanayofanywa na Dola dhidi ya CUF:-

1. KUHUSU UHALALI WA BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA: Kutokana na mkanganyiko unaosababishwa na upotoshaji wa makusudi unaofanywa na Ibrahim Lipumba na kikundi chake wa kuitisha watu wa kuokota barabarani na kuwakusanya Buguruni huku akiwaita kuwa ndiyo Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF, tumeona kuna haja ya kuweka kumbukumbu sahihi ili kuepusha upotoshaji huo usiendelee. Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama huwa linaundwa kila baada ya miaka mitano kupitia Uchaguzi Mkuu wa Chama ndani ya Chama na hupata wajumbe wake kupitia uchaguzi unaofanywa na Mkutano Mkuu wa Taifa (wajumbe 25 kutoka Tanzania Bara na wajumbe 20 kutoka Zanzibar), wajumbe 14 wanaoteuliwa na Mwenyekiti kwa kushauriana na Makamu Mwenyekiti na kisha kuthibitishwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa, wajumbe wanaoingia kwa nafasi zao wakiwemo Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Chama, Wenyeviti na Makatibu wa Jumuiya za Chama na Viongozi wa Kambi za Wabunge na Wawakilishi wa Chama. Viongozi Wakuu wa kitaifa wa Chama pia ni wajumbe. Wafuatao ndiyo Wajumbe halali waliochaguliwa na Mkutano Mkuu wa Taifa uliomalizika Juni 27, 2014 hapo Ubungo Plaza, Dar es Salaam kuwa wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa (BKUT) watakaokaa madarakani kwa kipindi cha miaka mitano (2014 – 2019) hadi watakapochaguliwa wengine na Mkutano Mkuu wa Taifa kwa mujibu wa Katiba ya CUF ya mwaka 1992 (Toleo la 2014):- VIONGOZI WAKUU: 1. Mwenyekiti (alijiuzulu tarehe 5 Agosti, 2015 na kujiuzulu kwake kuthibitishwa na Mkutano Mkuu wa Taifa wa dharura tarehe 21 Agosti, 2016).

Mbunge wa Temeke akamatwa kihuni

Image result for ABDALL MTOLEA PICTURES

SITAKI KUMUONA LIPUMBA ASEMA MBUNGE WA TEMEKE

Mbunge wa Temeke kwa tiketi ya CUF, Abdallah Ally Mtolea amefunguka na kusema kwa sasa hana jambo la kumshauri Profesa Lipumba na kudai haitaji hata kumuona kwa sababu ameshapoteza ile heshima na thamani yake.

Mtolea amesema hayo leo alipokuwa akihojiwa na EATV na kusema yeye alikuwa ni miongoni mwa watu ambao walikuwa wanamuheshimu sana  Prof. Ibrahim Lipumba kiasi kwamba ilifika hatua hakutaka kua muongeaji sana juu ya mambo yake lakini kwa kuwa tayari ameshajivunjia heshima mwenyewe hivyo hana budi kusema.
"Mimi nilianza kuona nia mbaya ya Lipumba pale aliponikatalia kwenda kwenye ufunguzi wa kampeni zangu mwaka 2015 kwani nilimfuata lakini yeye alikataa kabisa, lakini niliposhinda ubunge nilimfuata pia na kumpa taarifa na kumuomba tuendelee kushirikiana nikiamini yeye ni mkongwe katika siasa kuna mambo mengi ya kunishauri na kuniongoza sikumtenga kabisa, ila aliposema anataka kurudi baada ya kujiuzulu mimi sikumuelewa ni nikamfuata nikimwambia mzee unataka kutuletea mgogoro" alisema Mtolea 
Mbali na hilo Mtolea anasema saizi Lipumba amefikia hatua ambayo haambiliki chochote na kusema hatamani hata kukutana naye 
Msikilize hapa akifunguka zaidi 

Kesi YA CUF DHIDI YA RITA KUUNGURUMA JULAI 10

 

Mashauri sita yaliyofunguliwa katika Mahakama Kuu na Bodi ya Wadhamini ya CUF yanatarajiwa kusikilizwa na baadhi yake kutajwa tarehe, Jumatatu ya Julai 10, 2017, baada ya leo kuahirishwa usikilizwaji wa kesi ya msingi ya wizi wa ruzuku ya chama hicho. Kufuatia mawakili upande wa mashitaka kutopewa nakala ya maombi ya pingamizi la Mwanasheria Mkuu wa Serikali. 
Wakati akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, Wakili wa CUF, Juma Nassoro amesema leo mahakama hiyo imewapatia nakala za pingamizi hilo.
Na kwamba, Jaji Wilfred Dyansobela anayesimamia mashauri hayo amesema Jumatatu ijayo mashauri yote yatasikilizwa na kutajwa tarehe ikiwemo la kupinga maamuzi ya RITA ya kusajili wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa .
Shauri lingine litakalosikilizwa siku hiyo ni la kuzuia fedha za ruzuku ya chama hicho kupewa Profesa Lipumba na wenzake.
Aidha, upande wa Lipumba kupitia Abdul Kambaya haikuridhishwa na maamuzi hayo ya mahakama ya kuahirisha usikilizwaji wa kesi hiyo ya msingi kwa madai kuwa yanachelewesha muda.
“Sisi tulikuja kwa agizo la mahakama, badala yake jaji hakutokea tukasikia juu kwa juu kuwa kesi imeahirishwa. Wanachokifanya ni kuchelewesha muda jumatatu watazikwa,” amesema.  

TAMKO LA MADIWANI WA THE CIVIC UNITED FRONT (CUF-CHAMA CHA WANANCHI) WA MKOA WA DAR ES SALAAM JUU YA KUUNGA MKONO HOTUBA NA MSIMAMO WA CHAMA ULIOTOLEWA NA KATIBU MKUU MAALIM SEIF SHARIF HAMAD TAREHE 28 JUNE 2017 KATIKA HOTEL YA PEACOCK:

4
Image may contain: 4 people, people sitting, table and indoor
THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF-CHAMA CHA WANANCHI)
TAMKO LA MADIWANI WA THE CIVIC UNITED FRONT (CUF-CHAMA CHA WANANCHI) WA MKOA WA DAR ES SALAAM JUU YA KUUNGA MKONO HOTUBA NA MSIMAMO WA CHAMA ULIOTOLEWA NA KATIBU MKUU MAALIM SEIF SHARIF HAMAD TAREHE 28 JUNE 2017 KATIKA HOTEL YA PEACOCK:
Tarehe 5 JULY, 2017
NDUGU WAANDISHI WA HABARI,
WAHESHIMIWA VIONGOZI WA CUF,
WAHESHIMIWA WANACHAMA WA CUF,
WAHESHIMIWA WANANCHI, MABIBI NA MABWANA,
NAOMBA NIANZE KWA KUWASALIMU KWA SALAMU ZA CHAMA CHETU HAKI SAWA KWA WOTE,
1. Awali ya yote, tuanze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kutujaalia uhai na uzima na kutuwezesha kukutana hapa asubuhi hii, kwa lengo la kutoa Tamko na msimamo wetu Rasmi juu ya sintofahamu inayoendelea ndani ya Chama chetu, na kuunga mkono Hotuba na msimamo wa Chama uliotolewa na Katibu Mkuu wetu, Maalim Seif Sharif Hamad. Tukiwa ni Madiwani wa CUF, kutoka Manispaa za Mkoa wa Dar es Salaam na kupitia kwenu ujumbe wetu uweze kuwafikia wana-CUF wenzetu, Wapenda Mabadiliko wote nchini, na Watanzania kwa Ujumla.
2. Tunapenda kuchukua fursa hii kuwashukuru nyinyi Waandishi wa Habari kwa kuhudhuria kwenu na mara zote kutukimbilia kila tunapokualikeni mbali na Changamoto mnazokabiliana nazo juu ya uhuru wa Habari na aina ya uongozi wa Serikali ya awamu ya Tano jinsi unavyoikandamiza demokrasia nchini na kutopenda kukosolewa.

BASHANGE AWATULIZA WANA CUF

ZANZIBAR STONE TOWN MEMBER OF PARLIAMENT STAND WITH GIRLS

I STAND FOR THE GIRLS ... PLEASE JOIN ME
Image result for ALLY SALEH PICTURES
By Ally Saleh
Many people have come to the defence of young girls who get into wrong side and become pregnant while still at school be it at primary level or secondary one and thus cut off from following their educational programs.
Thus means not only dreams but also hopes are dashed and buried in a grave that most of them would not be able even to trace as they grow old and lament only. But then lamenting will not be enough because their lack of education might be an obstacle to their development and end up in the poverty cycle.
Most people believe that pregnancy in young girls is never wanted but these young females are caught at a time when they are not only naïve but also at an age where foolishness is only thing they do. And on top of it both young men and those of old age with good cash flow pry on these innocent souls and and trap them.
Some feel it is cruel to blame a girl of 13 or even 16 and 17 to have willingly made a choice of entering sex life and hence with no education to protect herself from becoming pregnant but even from being passed with HIV AIDS or any other sexual transmitted diseases.
A month ago a debate ensued at the Parliament about change of the 1971 Law of Marriage Act in order to change marriage age in Tanzania and a big shout was recorded with two opposing sides arguing their cases with no results. Those who refuse lean on morality and those who want it be raised to be 18 lean of reality.
There not even consensus with the Cabinet Members as the then newly appointed Minister for Constitutional and Legal Affairs Professor Palmagamba Kabudi took a cautious approach saying the government was still synthesizing the issue while Minister for Women and Health Ummy Mwallimu skipping out of official Budget presentation notes indicated that things were moving on to effect changes.
But while the debate is still raging in the public domain with consensus being sought with activists charging time was up for the changes, the traditionalist especially those with religious inclinations have been saying this was only going to happen over their dead bodies.
The latter’s argument is that if a girl was pregnant and returned to classes after delivery will poison the others on their habits, which tends to assume that the only bad thing is to become pregnant ignoring the very act of having sex which is not committed only by the girl who becomes pregnant but many and most others around her.

BODI FEKI YA LIPUMBA YA GONGA MWAMBA

UPDATES KUTOKA MAHAKAMA KUU LEO TAREHE 29/6/2017



MAHAKAMA YAPANGA KUSIKILIZA PINGAMIZI LA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI:

Leo mbele ya Mheshimiwa Jaji Wilfred Dyansobera amefanya maamuzi ya kuahirisha Shauri la Msingi Miscellaneous Civil Cause No. 21/2017 kuhusu wizi wa shilingi milioni 369 fedha za Ruzuku za Chama cha CUF uliofanywa na Lipumba na genge lake wakishirikiana na Msajili wa Vyama vya siasa nchini Jaji Franscis Mutungi mpaka Tarehe 6 July, 2017. Maamuzi hayo yameelezwa mbele ya Mahakama ya wazi (Open Court) iliyofurika wana NGANGARI wakiongozwa na Wabunge 40 wa CUF na kikosi makini cha ulinzi wa Chama Blue Guards. Hatua hiyo imefikiwa baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (Senior State Attorney) Wakili Msomi SILVESTER MWAKITALE – kuiomba Mahakama kuhairisha shauri hilo ili waweze kuwapatia nakala za Pingamizi (Copy of Preliminary Objection to be saved to Applicant-(THE REGISTERED TRSTEES OF THE CIVIC UNITED FRONT (CUF-CHAMA CHA WANANCHI). Upande wa Mawakili wasomi wa CUF ukiongozwa na JUMA NASSOR, HALFANI DAIMU NA HASHIMU MZIRAY ulikuwa hauna Pingamizi na Maombi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya kuweka pingamizi hilo na kukubaliana na kuagizwa na Mahakama kuwa kesho Tarehe 30/6/2017 nakala hizo wapatiwe Mawakili wa CUF na pingamizi hilo litasikilizwa Tarehe 6 July, 2017.

Katika hatua nyingine Mahakama Kuu haikuweza kufanyia kazi Maamuzi yake iliyoyatoa awali Shauri lilipoitwa mbele ya Jaji Tarehe 21/6/2017 juu ya kuwataka kufika Mahakamani Afisa wa RITA na Thomas Malima aliyejitambulisha kama Katibu wa Bodi ya Wadhamini aliyewasilisha barua ya kutaka Kufuta kesi zote zilizopo Mahakamani hapo kuleta ushahidi na kuthibitisha nyaraka zilizowasilishwa Mahakamani za kuteuliwa kwa ‘Bodi FEKI’ ya Wadhamini na pia kutaka kuwaondoa mawakili wanaoiwakilisha Bodi Halali ya Wadhamini ya CUF pamoja na kutaka kumuingiza Wakili Mpya atakaye iwakilisha ‘Bodi FEKI’ ya Lipumba na genge lake Mhe. Makubi Makubi. Kutosikilizwa kwa suala la maombi ya kufuta kesi limetokana na uwepo wa pingamizi la Mwanasheria Mkuu wa Serikali na hivyo kuamuriwa kuwa masuala hayo yatajadiliwa baada ya pingamizi hilo kusikilizwa na kutolewa maamuzi ndipo itaangaliwa kama kuna haja ya kuendelea na maombi hayo ya kufuta kesi hizo.

Mahakama Kuu imeendelea kuwatambua Mawakili wa Bodi Halali ya Wadhamini wa CUF inayoongozwa na Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad na kuiweka pembeni barua ya ‘Bodi FEKI’ ya Genge la Lipumba kutaka kubadilisha mawakili hao kwa kumuingiza wakili wao. Leo mawakili wa Lipumba na genge lake hawakuruhusiwa kushiriki katika kesi hiyo kwa kuwa si sehemu ya walalamikiwa (Respondents). Kesi hii inawahusu Bodi ya Wadhamini-CUF dhidi ya Mutungi na Mwanasheria Mkuu wa serikali.

Wakati huohuo CUF IKIWA NI TAASISI IMARA, YENYE VIONGOZI MAKINI tayari imeshachukua hatua za kutekeleza Maazimio ya Kikao Cha Kamati ya Utendaji Taifa kilichofanyika tarehe 23/6/2017 na kuongozwa na Mwenyekiti wake Maalim Seif Sharif Hamad katika Ofisi ndogo ya Makao Makuu Vuga, Zanzibar kushughulikia kisheria kuipinga Bodi FEKI ya lipumba kwa mujibu wa Sheria ya REGISTRATION INSOLVENCY AND TRUSTEESHIP AGENCY (RITA) THE TRUSTEES INCORPORATION ACT [CAP 318-R.E 2002] AN ACT TO PROVIDE FOR THE INCORPORATION OF CERTAIN TRUSTEES.

Article 26. “Application to decide question whether a person is a member of a corporate body or as to property When any question arises as to whether a person is a member of a body corporate or as to the vesting or divesting of any property under the provisions of this Act, any person interested in such question may apply to the High Court for its opinion on such question and notice of hearing shall be given to such persons and in such manner as the court shall think fit, and any opinion given by the court on an application under this section shall be deemed to have the force of a declaratory decree.” [s. 18]

Sheria hii inaeleza wazi kuwa “…kama kuna mtu yeyote ambaye hakuridhika na maamuzi ya RITA kuteua wajumbe wa Bodi ya Wadhamini sheria inampa haki ya kufungua mashtaka Mahakama Kuu na kupinga maamuzi ya RITA. Maamuzi ya Mahakama Kuu ndiyo yatakayo zingatiwa na kufuatwa kwa kuwa na nguvu ya kisheria.”

Pamoja na hilo wahusika wote walioshiriki kufoji nyaraka watapaswa kuitwa mbele ya Mahakama Kuu na kujibu kwanini wasitiwe hatiani na Kufungwa Jela kwa makosa hayo.

HAKI SAWA KWA WOTE

SALIM BIMAN
MKURUGENZI WA HABARI, UENEZI NA MAHUSIANO NA UMMA CUF-TAIFA
ZANTEL-0777414112
VODA-0752325227

MBARALA MAHARAGANDE
NAIBU MKURUGENZI WA HABARI, UENEZI NA MAHUSIANO NA UMMA CUF-TAIFA
maharagande@gmail.com
TIGO-0715 062577
VODA-0767 062577

CHAMA CHA CUF CHAZINDUA OFISI YA WABUNGE HUKO DAR


WABUNGE WA CUF PAMOJA NA VIONGOZI WENGINE WAKIFUTURU BAADA YA UFUNGUZI WA OFSI MPYA YA WABUNGE HUKO MAGOMENI DAR



IKIWA ni takribani miezi 10 sasa kwa Chama cha Wananchi (CUF), upande wa Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif
Hamad kuvamiwa katika Ofisi Kuu za Bugurunina kundi la Profesa Ibrahim Lipumba chama hicho kimezindua ofisi mpya za chama hicho katika eneo la Mtaa wa Idrisa,
Kata ya Mzimuni, wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Image may contain: 1 person, standing

Aidha, Seif amesisitiza kuwa hatarajii kukutana na  Profesa Lipumba kwa kile alichodai kuwa hatambuliki katika chama na hana  sifa hizo kwa sasa.  Akizindua ofisi hiyo ambayo lengo kubwa ni kwa ajili ya wabunge 40 wa CUF, Seif alisema  uamuzi wa wabunge hao kumpatia ofisi ya kufanyia kazi hapo ni cha kiungwana na kinahitajika kuungwa mkono na wanachama wote.
Image may contain: 3 people, people sitting

Alisema kwa muda wa miezi 10 sasa wamekuwa wakishindwa kufanya kazi hasa upande wa Tanzania Bara
jambo ambalo limewaathiri sana hivyo kupatiwa ofisi kutamsaidia kutimiza majukumu yake vilivyo bila hofu yoyote.Maalim Seif alisema kukosa ofisi kumewaathiri sana katika baadhi ya mambo hivyo anaamini kwa sasa akifikia Dar es Salaam anamahali pa kukutana na wakurugenzi wake.
Image may contain: 1 person, eating, sitting, food and indoor

“Nimekuwa ni kija hapa nakosa sehemu ya kukutana na wakurugenzi, viongozi mbalimbali wanachama ila hiki ambacho wabunge wamefanya ni cha kuungwa mkono sijawahi kufanya kazi na wabunge wanao kipenda chama kama kipindi hiki,” alisema.


Katibu huyo alisema atahakikisha kuwa anaanza kazi haraka iwezekanavyo kwa kukutana na wakurugenzi wake ili waweze kutekeleza majukumu ya chama.
Image may contain: 1 person, sitting and food

“Hakuna shaka kuwa hu u unaoitwa mgogoro umeturudisha nyuma sana hivyo naamini wakati wa kufanyakazi umerejea na hawa wabaya wetu hawata ambulia kitu kwani CUF ni  chama imara hakitikisiki,” alisema.
Maalim Seif alisema jitihada zinazofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kukimaliza chama ni kubwa lakini hawataweza kufikia lengo hilo kutokana na misingi ya chama hicho.
Image may contain: 3 people, people sitting
Alisema kwa sasaa atafanya kazi katika ofisi hiyo ambayo amepewa na wabunge hadi hapo muafaka wa ofisi kuu Buguruni utakapopatikana huku akisisitiza kuwa haki haipotei ila inachelewa.Katibu huyo alisema anaimani na   mahakama kuwa ita wapatia haki stahiki hivyo kuwataka wanachama kuendelea kuwa na subira.

Image may contain: 1 person, sitting and eating
Aidha, alisema kupitia mgogoro huo hadi sasa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini inashikilia zaidi ya sh. bilioni 1.2 ambazo ni ruzuku ya chamahicho.Maalim Seif alisema fedha hizo ni pamoja na zile ambazo ofisi ya msajili ilimpatia Lipumba hivyo waamini mgogoro ukiisha wata pata haki yao.

Kwa upande mwingine Katibu huyo alisema hana mpango wa kukutana naLipumba kuhusu mgogoro unaondelea ndani ya chama hicho kwa kile alichodai kuwa si kiongozi wala mwanachama wa chama hicho.Alisema CUF haimtambui Lipumba kwa sifa yoyote tofauti na kumfukuza uanachama hivyo yeye hawezi kukukutana na mtu  kamahuyo.
Image may contain: 1 person, sitting

Maalim Seif alisema pamoja na kuwa hawamtambui Lipumba kama kiongozi au mwanachama ila akiomba msamaha wapo tayari kumsamehe.
Akizungumza baada ya kuzinduliwa ofisi hizo Mbunge wa Viti Maalum na Kiongozi wa Wabunge wa CUF bungeni, Riziki Ngwali alisema wamelazimika kufungua ofisi nyingine ili wapate mahali pa kukutana wakiwa nje ya Bunge.
Image may contain: 1 person, standing

Ngwali alisema kupitia ofisi hiyo wataweza kujadiliana
mambo mbalimbali yanayo wahusu wabunge na wananchi na kuja na ufumbuzi.
Kwa upande wake Mbunge wa Temeke CUF, Abdallah Mtolea alisema katika ofisi hiyo wanatarajia kuajiri wataalam mbalimbali ambao watasaidia kufanya tafiti na kupitia tarifa mbalimbali za Bunge ili kuwarahisishia katika uchangiaji bungeni.


Alisema katika ofisi hizo wameingia mkataba wa kulipa sh. milioni 18 kwa mwaka ambazo zitatolewa na wabunge wenyewe kwa maslahi ya chama chao.

KATIBU MKUU WA CU ATEMEBELEA MKOA WA DAR KUKAGUA UHAI WA CHAMA


MAALIM SEIF SHARIF HAMAD APOKELEWA JIJINI DAR ES SALAAM NA MANAIBU MEYA NA WABUNGE:Image may contain: 6 people, people standing
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, leo ameanza ziara rasmi ya siku tatu katika wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuwatembelea Wazee wa CUF, kuwafariji Wagonjwa na wafiwa mbalimbali.
Ziara hiyo iliyoanza majira ya saa 5 kamili asubuhi katika Kata ya Upanga ambapo alikwenda kumjulia hali mjane wa Marehemu Imamu Mohamed Ali Abeid, baadae alikwenda kumjulia hali Mzee Mawanja (Vingunguti), Mzee Hussein Kutopa, Mratibu CUF (Kata ya Vingunguti), Sheikh Juma, Bibi Hidaya, Hamad Tafiko na Mzee Mfaume (Kata ya Gongolamboto). Wengine waliotembelewa na Katibu Mkuu ni pamoja na Mzee Kombo Faki, Yusuf Musa na Mzee Hamisi (Kata ya Majohe).
Akiwasalimu wananchi wengi waliojitokeza kwa furaha kubwa kumuona Kiongozi wao katika maeneo mbalimbali aliyofika, Maalim Seif amewahakikishia kuwa CUF ni Taasisi Imara na kamwe haiwezi kuyumbishwa na mtu yeyote yule, na kwamba itazishinda changamoto zote zilizojitokeza muda si mrefu. Amewataka vijana kujiandaa kwenda kuchukua ofisi yao ya Buguruni wakati wowote kuanzia sasa.


Katika msafara huo Katibu Mkuu aliambatana na Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe. Musa Kafana, Naibu Meya wa Ilala Mhe. Omari Kumbilamoto, Mhe. Abdallah Mtolea (MB-Temeke, na Naibu Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa), Mhe. Shaweji Mketo (Naibu Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Uchaguzi), Mhe. Mbarala Maharagande (Naibu Mkurugenzi wa Habari), Mhe. Bakari Shingo (Mwenyekiti wa Wilaya ya Ilala), Mhe. Salma Mwassa (MB - V/Maalum), pamoja na viongozi wengine mbalimbali wa Jumuiya za Chama na Walinzi (Blue Guards).
Mheshimiwa Maalim Seif ataanza ziara rasmi ya ukaguzi wa uhai na shughuli za Chama katika Mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara kwa ratiba itakayotolewa hivi karibuni.
Haki Sawa Kwa Wote
Mbarala Maharagande,
Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mawasiliano na Umma - CUF
1/5/2017

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU ZIARA YA KATIBU MKUU WA THE CIVIC UNITED FRONT (CUF-Chama Cha Wananchi) KATIKA WILAYA ZA KISIWA CHA UNGUJA ILIOANZA TAREHE 1

Image may contain: 2 people, hat and outdoor

April, 1 2017 Katibu Mkuu wa The Civic United Front (CUF-Chama Cha Wananchi), Maalim Seif Sharif Hamad, ataanza ziara ya kichama ya siku tisa katika Wilaya saba za Mikoa mitatu ya kisiwa cha Unguja.
Ziara hiyo itaanza Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja ambapo Maalim Seif Sharif Hamad atafanya ziara maalum ya kutwa nzima katika kisiwa cha Tumbatu na baadae, siku zinazofuata, kuendelea na ratiba ya ziara yake katika maeneo mengine ya kisiwa cha Unguja.
Katika ziara ya kisiwa cha Tumbatu Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad amepanga kutembelea maeneo mbali mbali ya kisiwa hicho hasa yale yaliyoathiriwa kwa kuchomwa moto na makundi ya vijana maharamia wanaojulikana kama mazombi.
Kama ilivyo kawaida yake katika ziara za aina hii, Maalim Seif Sharif Hamad, amepanga pia kuwatembelea na kuwafariji wananchi wa kisiwa hicho waliopata athari kutokana na kadhia za matukio ya uvunjwaji wa haki za binadamu hasa wale waliopata athari kufuatia kuvamiwa, kupigwa na kujeruhiwa na makundi hayo. Kwa upande mwengine Maalim Seif Sharif Hamad atawajulia hali na kutoa pole kwa wagonjwa na kuwafariji wafiwa.
Sambamba na ratiba yake hiyo, Maalim Seif Sharif Hamad atafanya shughuli mbali mbali za uimarishaji Chama katika kisiwa cha Tumbatu kwa kuweka mawe ya msingi, kufungua matawi na majengo mapya ya Chama, kuzindua waratibu wa Chama na kukabidhi kadi kwa wanachama wapya wa chama katika maeneo mbali mbali ya kisiwa hicho.

Katika ziara ya kisiwa cha Tumbatu Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad amepanga kutembelea maeneo mbali mbali ya kisiwa hicho hasa yale yaliyoathiriwa kwa kuchomwa moto na makundi ya vijana maharamia wanaojulikana kama mazombi.
Kama ilivyo kawaida yake katika ziara za aina hii, Maalim Seif Sharif Hamad, amepanga pia kuwatembelea na kuwafariji wananchi wa kisiwa hicho waliopata athari kutokana na kadhia za matukio ya uvunjwaji wa haki za binadamu hasa wale waliopata athari kufuatia kuvamiwa, kupigwa na kujeruhiwa na makundi hayo. Kwa upande mwengine Maalim Seif Sharif Hamad atawajulia hali na kutoa pole kwa wagonjwa na kuwafariji wafiwa.
Sambamba na ratiba yake hiyo, Maalim Seif Sharif Hamad atafanya shughuli mbali mbali za uimarishaji Chama katika kisiwa cha Tumbatu kwa kuweka mawe ya msingi, kufungua matawi na majengo mapya ya Chama, kuzindua waratibu wa Chama na kukabidhi kadi kwa wanachama wapya wa chama katika maeneo mbali mbali ya kisiwa hicho.
Baada ya kukamilika kwa ziara katika kisiwa cha Tumbatu, Maalim Seif Sharif Hamad ataendelea na ziara yake katika Mikoa na Wilaya nyengine za Unguja kwa ratiba ifuatayo:
Siku ya Jumapili, tarehe 2 Aprili, 2017 Katibu Mkuu atafanya ziara Wilaya ya Kaskazini ‘A’
Siku ya Jumatatu, tarehe 3 Aprili, 2017 ziara itafanyika Wilaya ya Kaskazini ‘B’
Siku ya Jumanne, tarehe 4 Aprili, 2017 Katibu Mkuu atafanya ziara Wilaya ya Kusini Unguja.
Siku ya Jumatano, tarehe 5 Aprili, 2017, Maalim Seif Sharif Hamad atafanya ziara katika Wilaya ya kati. Kuanza ziara yake kwa siku hiyo, Maalim Seif Sharif Hamad atafanya ziara maalum katika kisiwa cha Uzi na Jumamosi tarehe 8 Aprili, 2017 ataendelea na ziara yake katika maeneo mengine ya Wilaya hiyo.
Jumapili tarehe 9 Aprili, 2017, Katibu Mkuu ataendelea na ziara yake katika Wilaya ya Mjini, na Jumatatu tarehe 10 Aprili, 2017 ziara itafanyika Wilaya ya Magharibi ‘B’ kabla ya kuhitimisha ziara yake kwa kutembelea Wilaya ya Magharibi ‘A’ siku ya Jumanne tarehe 11 Aprili, 2017.
Imetolewa na:
Hisham Abdukadir
Afisa Habari na Mawasiliano
The Civic United Front
CUF-Chama Cha Wananchi
Makao Makuu-Zanzibar

Zanzibar Kumekucha kwenye Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Dimani.

Lowassa atamba kwa kura nyingi alizopewa na Wazanzibari , Kwnye uchaguzi wa jimbo la Dimani.
Lowassa ambaye alikuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chadema, katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 anashiriki uzinduzi wa kampeni hizo sambamba na Maalim ambaye pia alikuwa mgombea Urais Visiwani Zanizbar kupitia CUF.
Wakati Lowassa na Maalim Seif wakizindua kampeni hizo leo, vigogo wengine kutoka vyama washirika wa Ukawa wanatarajia kupanda jukwaa katika siku zingine za kampeni ikiwemo Januari 21 mwaka huu ambayo ndiyo siku ya mwisho ya kampeni.
Tayari Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimezindua kampeni yake siku nne zilizopita ambapo Abdurahman Kinana, Katibu Mkuu wa chama hicho akiambatana na viongozi wengine wa chama hicho na jumuiya zake walihutubia.
Miongoni mwa waliohudhuria uzinduzi wa CCM ni Shaka Hamdu, Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM).
Kwa mujibu wa Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema – Zanzibar viongozi mbalimbali wa Chadema taifa akiwemo Mwenyekiti, Freeman Mbowe na Tundu Lissu ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, watashiriki kampeni za Dimani kwa nyakati tofauti.
Salim Bimani, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma wa CUF amenukuliwa akisema “Patakuwa hapatoshi hapa Skuli ya Fuoni, Lowassa anakubalika sana hapa na pia atapata nafasi ya kuwashukuru Wazanzibar kwa kura nyingi walizompigia katika uchaguzi wa 2015.”
Mbali na viongozi wa Chadema kuwa katika ratiba ya kushiriki uchaguzi mdogo wa Dimani pia inatarajiwa kuwa James Mbatia, Mbunge wa Jimbo la Vunjo na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi anatarajiwa kutua Visiwani Zanzibar pia.
Itakumbukwa kuwa uchaguzi huo mdogo utafanyika tarehe 22 Januari, 2017 kufuatia kufariki dunia kwa Hafidh Ally Tahir aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo kabla ya kufariki dunia 11 Novemba, 2016 mkoani Dodoma.

WAZANZIBARI WANAYE RAIS WAO WA MOYONI

VIONGOZI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameishiwa hoja. Wanapojitokeza mbele ya umma wa Wazanzibari na Watanzania, na kokote waendako, hawawezi kuzungumza kwa ujasiri na uchangamfu kile hasa kilichotokea kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 wa Zanzibar.
Yeyote miongoni mwao akitaka kusema, atalitafuta la kusema, na akilipata, atalisema katika lugha ya kulazimisha aaminike. Atajibaraguza tu. Ni kwa sababu kubwa moja – wanajua kwa uhakika wanaiongoza Zanzibar kwa mabavu.
Wanaongoza kwa mabavu maana hawana ridhaa ya wananchi kupitia uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba 2015. Wananchi wa Zanzibar wangekuwa wametoa ridhaa kwa uongozi wa CCM, isingekuwepo sababu ya kulazimishwa kumridhia Dk. Ali Mohamed Shein.
Pale rais wa jamhuri, Dk. John Magufuli alipotoa matamshi ya kuwataka wamtii Dk. Shein kwa kusema “ndiye rais wa Zanzibar na hakuna wa kumuondoa mpaka uchaguzi mwingine ufike mwaka 2020,” alikuwa analazimisha wananchi wamkubali kiongozi wasiyemchagua.
Alifanya hivyo, tena katika lugha ya kusononesha wananchi, kwa kujua huyo anayetaka wananchi wamridhie hawakumchagua. Labda rais alijuilishwa na wasaidizi wake wa kiusalama kwamba Zanzibar kungali na upinzani mkali kwa umma kumkubali Dk. Shein, na hiyo imetokana na ukweli kuwa hakuwa chaguo lao kupitia uchaguzi ule.
Hata pale alipoamua kumuita Jecha Salim Jecha, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), na kumpongeza na kumtakia tuzo kwa alichosema “amefanya kazi yake vizuri kwa asilimia zote,” alijua anajitoa kimasomaso katika dhana ile ya ‘funika kombe mwanaharamu apite.’
Tuseme itokee Dk. Shein amemtunuku tuzo Jecha, kama alivyosikia rai ya Rais Magufuli kwenye mkutano wa hadhara Septemba mwaka jana, ninaamini Jecha ataendelea kuumia moyo.
Mtumishi mstaafu huyu serikalini anayefahamika kuwa kada wa CCM, anaumia moyo kwa sababu anajua alikanyaga haki. Mwenyewe alikiri mbele ya makamishna wa Tume kuwa alilazimika kufuta uchaguzi ili “kukiokoa Chama cha Mapinduzi.” Kumbe alikistiri chama chao.
Jecha alitangulia kuomba msamaha makamishna hao akiwepo makamu mwenyekiti Jaji Abdulhakim Ameir Issa, alipokutana nao mara ya kwanza Novemba mosi 2015, tangu alipoutangazia umma tarehe 28 Oktoba 2015, kuwa “nimeufuta uchaguzi na matokeo yake yote na utaitishwa uchaguzi mpya baadaye.”
Jecha alitoa tangazo hilo siku ambayo kisheria alitakiwa kutangaza matokeo ya urais ambayo yalishakuwa tayari. Kura zote zilishahesabiwa vituoni na kuidhinishwa na watendaji wa Tume, sehemu kubwa ya kura zilishahakikiwa.
Wakati huo Jecha akitangazia akiwa mafichoni, baada ya kutelekeza kazi aliyoahidi kuifanya kwa kisheria, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi walishakabidhiwa hati za ushindi.
CCM ilikuwa imeangushwa na umma. Badala yake, kwa mara nyingine, Chama cha Wananchi (CUF) ndicho kilipewa ridhaa. Yaliyofanyika baada ya kufutwa uchaguzi, yanabakia haramu kisheria.
Ina maana ule ulioitwa “uchaguzi wa marudio” uliofanyika 20 Machi 2016, kisheria ulikuwa na mpaka leo hii, batili. Na huu ndio uchaguzi ambao CCM kilitangazwa mshindi.
Rais anajua Jecha haishi kwa raha. Anahofu. Anakijua anachohofia. Sasa ni kwa nini aishi kwa hofu kama hakutenda lolote baya? Jecha ataishi kwenye kwapa za dola hadi lini?
Binafsi ninamuonea huruma kwa namna anavyoishi katika utaratibu wa kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa; na wafanyao hivyo wakiwa ni viongozi wa CCM, chama kilekile kilichomteua kugombea ubunge mwaka 2010.
Wiki iliyopita, akasikilikana kiongozi mwingine wa ngazi ya juu wa CCM akiendelea kuthibitisha walivyoishiwa hoja. Uovu wa kuhujumu maamuzi ya wananchi wa Zanzibar unawaandama kisawasawa.
Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana, katibu mkuu wa chama hicho, kwenye jukwaa la kampeni ya uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Dimani, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja, alisema, “Hakuna nchi yoyote yenye ubavu wa kumtangaza Maalim Seif Shariff Hamad kuwa rais Zanzibar.”
Alisema wapinzani wamekosa la kufanya na wamebakia kudanganya wananchi kuwa kuna rais mwingine atakayetangazwa. “Nawaambia acheni kudanganywa, hakuna rais mwingine atakayetangazwa badala ya Dk. Shein hadi mwaka 2020.”
Anaibua maswali. Ni kwanini hasa Kanali Kinana aseme hivyo leo? Hivi amemsikia nani akiwaambia watu Maalim Seif atatangazwa rais na nchi fulani? Tangu lini kiongozi akatangazwa na nchi? Je kwa kauli yake hiyo anamaanisha CCM inatapatapa?
Huko ni kutapatapa. Uongozi uliojiweka madarakani kama hauna hofu yoyote, ya nini watu wazima kupiga mayowe wakati unashika serikali?
Upo huogopi yeyote na chochote, si unaendesha mambo yako kwa rah
a; yanakusumbuaje maneno ya mitaani? Viongozi wa CCM kwani wanahofia kitu gani? Haoni kanali kuwa huko ni kule kujitekenya wakacheka wenyewe?
Labda watu wamesahau hulka ya Kanali Kinana anapoandamwa na wakati mgumu kisiasa. Huhangaika na hatimaye kujitengenezea kivuli. Akitupa kombora, anakiona kivuli chake.
Ndiye huyuhuyu ambaye Septemba 2015, alijitokeza hadharani na kuandika makala kwenye jarida la Hill, akisema upinzani unaoongozwa na Edward Lowassa na wenzake hauwezi kuruhusiwa kushika dola.
Alisema Tanzania haiwezi kuachiwa kuwa makazi ya makundi ya Waislam wenye misimamo mikali kama kundi la Uamsho lililojipatia umaarufu mkubwa Zanzibar kwa kutaka Muungano wa maridhiano.
Kanali Kinana kuitaja Zanzibar si kwa bahati mbaya; anaijua ni nchi ambayo Uislam sio tu dini inayotawala imani za Wazanzibari karibu wote, bali kwa kweli ndio staili ya maisha hata kwa wasioifuata. Hawafuati mpangilio wa ibada zake, bali wanapenda utamaduni wa Kiislam.
Lakini pia, anajua Zanzibar ndiko serikali ya CCM imekuwa ikipata shida kubwa kuhimili nguvu ya maoni ya wananchi wake waliothibitisha pasina shaka kuwa hawawezi tena kuishi chini ya utawala wa CCM.
Ndio maana makala yake ilijibiwa na wengi wakiwemo waandishi wa kizungu. Majibu yakawa kwamba kiukweli, utawala wa CCM unaendesha serikali kwa mfumo wa kuchochea migawanyiko na Uislam ukitumika kama kivuli.
Aliiandika makala baada ya kujionea muamko mkubwa wa wananchi kisiasa na kiukombozi. Anajua kilichomsibu (marehemu) Samuel Sitta alipokwenda kushawishi katiba mpya. Sheria ilichanwa akishuhudia.
Akiwa kwenye ziara aliyofuatana na Nape Nnauye, aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Kanali Kinana alisema kwa hali aliyoiona, atalazimika kuhamia Zanzibar wakati wa uchaguzi ili kukisaidia chama chake. Alibaini ugumu wa CCM kushinda uchaguzi Zanzibar.
Ripoti zinasema wakati wa ziara yake, mara kadhaa alishangazwa kuwaona watu walewale kila mkutano aliohutubia. Alipouliza, wasaidizi wake walimwambia, “kama si hivyo katibu, huku hutapata watu wa kukusikiliza.”
Makundi ya watu huhamishwa huku na kule kujaza mikutano ya CCM. Ni tofauti na CUF ambako wananchi huchangishana fedha kugharamia usafiri ili kufika kwenye mikutano ya hadhara kote Unguja na Pemba.
Pita mitaani Zanzibar, wananchi wanasema “tunae rais wetu wa moyoni.”
Maoni: 0774/0713 226 248
Chanzo: MwanHalisi

Jumuiya ya vijana CUF (JUVICUF) wilaya ya Kaskazini A Unguja leo tarehe 22/10/2016, imefanya Kongamano lao katika Viwanja vya hoteli ya Silver sand,Pwani mchangani Wilaya ya Kaskazini A Unguja.



Jumuiya ya vijana CUF (JUVICUF) wilaya ya Kaskazini A Unguja leo tarehe 22/10/2016, imefanya Kongamano lao katika Viwanja vya hoteli ya  Silver sand,Pwani mchangani  Wilaya ya Kaskazini A Unguja.

Kongamano hilo limelenga katika kujitathmin Zanzibar tulipotoka tulipo na tunapoelekea pamoja na mustakbali wa jumuiya za vijana na jinsi ya kufanya kazi kisayansi.

Katika kongamano hilo lililokutanisha wajumbe wa kamati tendaji za Wilaya za kisiwani Unguja za jumuiya ya vijana wa CUF (JUVICUF),pia viongozi waandamizi wa chama cha wananchi CUF na jumuiya walihudhuria katika kongamano hilo miongoni mwa viongozi hao ni;

Mh.Nassor Ahmed Mazrui (Naibu katibu mkuu CUF Zanzibar),
Mh.Juma Duni Haji (Makamo M/kiti mstaafu CUF),
Mh Salim Biman (mkurugenzi wa habari na uenezi CUF),
Mh. Khalifa ( Mbunge wa jimbo la Mtambwe na M/kiti wa chama wilaya ya Wete),
Mh.Faki Suleiman (Makamo M/kiti JUVICUF Taifa),
Mh.Mahmoud Ali Mahinda (Katibu Mtendaji JUVICUF Taifa),
Mh.Issa Kheir Hussein ( katibu wa Katibu mkuu),
Wajumbe wa baraza kuu chama cha wananchi CUF,
Wawakilishi, wabunge wa chama na
Wajumbe wa kamati tendaji JUVICUF taifa.

Pamoja na mengi katika kongamano hilo Mh. Mazrui amesisitiza kuwaambia vijana kwamba "vijana ondoeni hofu  maana tuliwaahidi kama ikitokea tutashindwa kuipata haki ya Wazanzibar tutawaambia vijana muitafute wenyewe ila musijali bado hatujashindwa na wala hakuna dalili za kushindwa katika hili, haki yenu itapatikana muda sio mrefu"

pia akawasihi vijana kwa kusema " vijana chama kinawategemea hivyo hamupaswi kutetereka kwamaana kama mutatetereka na chama kitatetereka hivyo munapaswa kuwa imara muda wote".

Kuhusu suala la mgogoro iliotengenezwa na *wahafidhina* Mh Mazrui alisema " CUF nichama imara na kitaendea kuwa imara na CUF ndio iliokuza jina la Lipumba na ifahamike ikiwa Lipumba amekianzisha yeye chama cha CUF basi ataweza kukivuruga lakin kama CUF ndio imemtengeneza yeye basi yeye ndio atakae vurugika"

Na mwisho kabisa akawaambia yakwamba  ikiwa CCM wanasema Maalim ni Simba mzee basi niajabu kuona Simba mzee kumpita Paka jike kwa kura zaidi ya elfu ishirini na tano (25,000)".

Nae mh Juma Duni Haji amesema kwa mzalendo yoyote hawez kukubali kununulika " mzalendo hawezi kurud nyuma wala kukubali kutiwa bei,mimi hapa nimeteswa na kufungwa lakin bado naamin katika ukombozi kwasababu *I HAVE  A MISSION* na siwezi kukubali kurudi nyuma mpaka malengo ya ukombozi yakamilike."

Mwisho nae babu Duni amewaambia vijana ya kwamba " Vijana musijali,kuhusu haki yenu ya 25,october kwamaana kijungu kipo jikoni kinapwaga na sio kijungu cha mawe bali nicha maboga,hivyo vijana muwe tayari kuyapokea mamlaka yenu kamili"

Naye Katibu mtendaji wa JUVICUF taifa Mh Mahinda amesema " Hakuna wakumzuia Maalim Seif kuzungumza na Wazanzibari,na waumin wenzake akiwa msikitini, na siku watakapo jaribu kumkamata au kumdhalilisha kiongozi huyo basi katu Vijana wa CUF na Wanzanzibar wazalendo hatutokubali nandio itakua mwanzo wa fujo katika nchi hii" alimalizia kwa kusema "tumechoka na hatuwezi kukubali tena kuwa maridhia"

Mwisho Mh.Salim Biman alifunga kwa nasaha nyingi kwa vijana pamoja nakuwataka vijana kuwatayar kuyapokea mamlaka kamili baada ya kazi kubwa walioifanya.
Pia aliwapongeza zaidi vijana wa JUVICUF wilaya ya Kaskazini A kwakuonesha mfano kwa kufanya jambo kubwa la kuwakutanisha vijana kwalengo la kujenga

Abeid Kh Bakar
N/M/Habari na Uenezi
JUVICUF - Taifa

Jecha ni wa Kushtakiwa sio wa Kupongezwa

Image result for picha ya jecha na Magufuli
CHAMA cha Wananchi (CUF) kimetoa tamko la kumshangaa Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli kwa kutaka Jecha Salim Jecha, Mwenyekiti wa tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), atunukiwe tuzo kwa utendaji uliotukuka,.Chama hicho kimesema kwamba mshangao uliopo unahusu kitendo cha rais Magufuli kumsifia Jecha ambaye anajulikana dunia nzima kuwa amevuruga uchaguzi mkuu wa Zanzibar.
“Ni jambo la kushangaza Rais anamsifia hadharani Jecha kuwa amefanya kazi nzuri asilimia 100 wakati waangalizi wa ndani na nje wa uchaguzi walijiridhisha kuwa uchaguzi ulikuwa huru, wa haki na uliofanyika kwa amani,” amesema Julius Mtatiro, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya CUF.
Mtatiro ametoa taarifa hiyo kwenye mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika ofisi za makao makuu ya chama hicho, Buguruni, jijini Dar es Salaam.
Hatua hiyo ni majibu ya chama hicho kwa kauli alizotoa Rais Magufuli katika hotuba zake mbili alipokuwa katika ziara ya kushukuru wananchi wa Zanzibar. Alifanya mikutano Gombani ya Kale, Chake Chake Pemba Ijumaa na Kibandamaiti, mjini Zanzibar jana.
Katika mikutano yake alimsifia Jecha kuwa alifanya kazi kwa ufanisi na jana alipokuwa uwanja wa Demokrasia Kibandamaiti, alipendekeza apewe tuzo na Rais wa Zanzibar.
Mtatiro katika kauli yake amesema kwamba Jecha alipofuta uchaguzi mkuu wa 25 Oktoba 2015 alijifanyia tu bila ya kuwa na mamlaka yoyote ya kisheria ya kufanya hivyo.
Kwa kufuta uchaguzi, katika siku aliyotarajiwa kutangaza matokeo ya mwisho ya kura za urais, Jecha alivunja sheria na kusababisha tafrani hivyo kukibeba Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia kilichoitwa “uchaguzi wa marudio” uliofanyika 20 Machi 2016.
Ni katika uchaguzi huo wa marudio, Jecha alimtangaza Dk. Ali Mohamed Shein kuwa mshindi, utangazaji uliofanyika siku hiyohiyo ya uchaguzi. Tofauti na ilivyokuwa Oktoba 2015 ambako kwa siku nne Jecha alishindwa kutangaza ushindi wa CUF kilichomsimamisha katibu mkuu wake, Maalim Seif Shariff Hamad.
“Ni jambo lisilokubalika hata kidogo kujisifia ushindi wa kupora katika uchaguzi kutokana na kupendelewa na Tume ya Uchaguzi ikishirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama,” amesema Mtatiro katika tamko lake.
Mapema kabala ya mkutano wa Mtatiro na waandishi wa habari kulitokea tafrani kati ya walinzi wa CUF na walioaminika wafuasi wa Mwenyekiti aliyejiuzulu na baadae kusimamishwa uanachama Prof. Ibrahim Lipumba waliotaka kulazimisha kuingia ndani ya makao makuu Buguluni.

Mtatiro mwenyekiti CUF

Image result for julius Mtatiro pictures
JULIUS Mtatiro, mwanasiasa machachari na mchambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii nchini,  ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya muda ya uongozi ndani ya Chama cha Wananchi (CUF),Mtatiro aliyewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bara, ataongoza kamati inayojumuisha Ahmed Katani na Severina Mwijage ambao ni wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa (BKUT).
Katani ni Mbunge wa jimbo la Tandahimba, mkoani Mtwara wakati Severina alikuwa mjumbe wa kamati kama hiyo ilipoteuliwa Agosti mwaka jana mara baada ya Profesa Ibrahim Lipumba kujiuzulu uenyekiti kwa barua ya 5 Agosti.
Uteuzi huo uliotangazwa leo na Nassor Ahmed Mazrui, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar,  umefanywa na Baraza Kuu lililofanya kikao cha siku moja jana mjini Zanzibar.
Kikao cha baraza kuu ambacho kikatiba, kimekasimiwa madaraka ya Mkutano Mkuu wa Taifa, kimefanyika katika hatua ya kukabiliana na hali ya hewa iliyochafuka baada ya kundi la wanachama “walioasi” kuvamia mkutano mkuu maalum uliofanyika 21 Agosti jijini Dar es Salaam ukiwa na agenda ya kuchagua mwenyekiti mpya.Mkutano huo pia ulikuwa utumike kumchagua makamu mwenyekiti kutokana na Juma Duni Haji naye kujiuzulu Agosti mwaka jana, yeye akiwa ameidhinishwa na chama ili kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi mkuu wa rais Oktoba mwaka jana.
“Kwa kuzingatia kwamba kutokamilika kwa Mkutano Mkuu Maalum wa Taifa, kulisababisha kushindwa kufanyika kwa uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Chama, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limetumia uwezo liliopewa na Katiba ya Chama, Ibara ya 101 na 118, kuunda Kamati ya Uongozi ambayo itakuwa ikifanya kazi za Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti hadi hapo uchaguzi wa kujaza nafasi hizo utakapofanyika,” imesema taarifa ya Mazrui.
Baraza pia limemteua Joram Bashange kukaimu nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Bara na Mbarala Maharagande kuwa Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma hadi hapo nafasi hizo zitakapojazwa rasmi kwa mujibu wa masharti ya Katiba ya Chama hicho.
Bashange ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Fedha wa chama, anashika kwa muda nafasi aliyokuwepo Magdalena Sakaya, Mbunge wa Kaliua, mkoani Tabora ambaye ni mmoja wa viongozi 11 wa juu akiwemo Prof. Lipumba, ambao uanachama wao umesimamishwa na Baraza Kuu hilo.Naye Maharagande anachukua nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Abdul Kambaya ambaye yumo katika orodha ya viongozi waliosimamishwa uanachama kufuatia tuhuma za kuongoza vurugu zilizosababisha kuvunjika kwa mkutano mkuu maalum.
Viongozi wengine waliosimamishwa mpaka watakapofika kujielezambele ya Baraza Kuu, ni Ashura Mustapha, Omar Mhina, Thomas Malima, Kapasha M. Kapasha, Mohamed Habib Mnyaa, Haroub Shamis na Mussa Haji Kombo.Ashura ni mjumbe wa Baraza Kuu na mwanamama aliyewahi kuwa Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano ya Umma CUF wakati Mnyaa na Kombo, walikuwa wabunge kipindi cha 2010/2015; Mnyaa akiwakilisha jimbo la Mkanyageni na Kombo jimbo la Chake Chake, kisiwani Pemba.
Taarifa ya Mazrui imesema hatua ya kuadhibu viongozi hao imetokana na kuthibitika kuwa waliongoza vurugu ambazo chama kinaamini zilipangwa makusudi kwa nia ya kukihujumu.
Viongozi hao wametajwa kuwa walishirikiana na maadui wa chama walio ndani na nje na kwamba walikaidi hata walipotakiwa kurekebisha mwenendo wao “huo mbaya dhidi ya chama.”

Sera ya kunena na Kutenda ya Wana CUF

AHSANTE MHE. DIWANI  OMAR KUMBI LA MOTO AHSANTE, MHE. MBUNGE WA JIMBO LA KINONDONI KWA KUSHIRIKI KAMA MGENI  RASMI AHSANTE WANANCHI WA VINGUNGUTI  KWA KUCHAGUA MAENDELEO AHSANTE VIONGOZI WA CUF KATA VINGUNGUTI KWA KUTANGAZA SERA INAYO TEKELEZEKA

Mhe. Omary Kumbilamoto Diwani wa Kata ya Vingunguti Leo Amekeleza  Ahadi ya Chama Cha Wananchi Cuf kwa Wapiga kura wa Kata ya Vingunguti. Ikumbukwe Wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu october 2015 Chama cha CUF  kupitia Mgombea wake iliwaahidi wananchi Wakikichagua Chama cha CUF Tutahakikisha Vingunguti Wanakua na Gari ya Wagonjwa ya Kata husika Leo yametimia.





Mheshimiwa Kumbi la Moto akwia ndani ya gari alilolikabidhi kwa wana VIngunguti.




Picha ya Chini Mheshimiwa Omar Kubi la Moto akikabidhi jezi kwa timu ya Vijana wA Vingunguti.

Mheshimiwa Kumbi la moto anasema michezo inahitaji kusaidiwa kwa vijana wetu.


MAALIM SEIF AZUNGUMZA NA WATANZANIA WA BOSTON, SEHEMU YA PILI

Na Mwandishi wetu Boston

Makamo wa Kwanza Mstaafu wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, amemaliza awamu ya pili ya ziara zake za Kimataafa hapa nchini Marekani iliyoanza wiki mbili zilizopita.

Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na Wazanzibar 

Maalim Seif, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) alikamilisha ziara yake hiyo tarehe 30 Julai kwa kuzungumza na Wazanzibari kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika katika jimbo la Massachusetts.

Mgeni huyo rasmi alikaribishwa kwa risala ya Jumuiya ya Wazanzibari waishio katika jiji la Boston kulikofanyika mkutano huo, Bwana Mohammed Lali, iliyoelezea imani yao juu ya uongozi wa Maalim Seif katika mapambano ya kupigania haki sawa na demokrasia Visiwani Zanzibar.

Akijibu risala hiyo, Mwanasiasa huyo alielezea shukrani zake za dhati kwa imani ya Wazanzibari juu uongozi wake na kuwahakikishia kuwa haki yao itapatikana.

HABARI ZILIZOJIRI LEO


Topics :
 
Support : ZENJIBARZA
Copyright © 2011. ACT WAZALENDO DIASPORA NETWORK - All Rights Reserved