Headlines News :
KARIBU CUF DIASPORA NETWORK - CUF HAKI SAWA KWA WOTE...TEGEMEA KILA JIPYA NA ZURI KUTOKA KWETU...LIKE PAGE YETU KWENYE FACEBOOK
Showing posts with label VEDIO. Show all posts
Showing posts with label VEDIO. Show all posts

NDUNGAI NI NYOKA ANETAFUNA MKIANI

SERIAKLI YA CCM INAVYOJIKANYAGA LIPUMBA NA SAKAYA SIO WANCHAMA WA CUF ni mamluki walionunuliwa na CCM kuisambaratisha CUF kwa k usaidiwa na Msajili wa vyama , BRELA na Ofisi ya Speaker kutumika kuvuruga demokrrasia na kuzuia mabadiliko ndani ya nchi

Katibu Mkuu wa Chama cha CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema kwamba hatua ya Spika kuwavua ubunge , udiwani na kuteua wengine wapya inalenga kudhoofisha kambi ya wabunge wa CUF na Ukawa. Amesema Watanzania wanapaswa wajikumbushe kwamba hata kama hicho kinachoitwa ‘kuwafukuza uanachama’ wabunge halali wa CUF kingekuwa kiko sawa, hatua kama hiyo hufuata taratibu zote za kisheria na kikanuni za Bunge kujiridhisha kwanza. “ Spika Job Ndugai anadhani Watanzania ni vichaa wamuamini kuwa alishachukua hatua ya kujiridhisha kuwa wabunge wanane wa Chama cha Wananchi (CUF) wamefukuzwa uanachama kulingana na taratibu za chama hicho na hivyo wamekosa sifa za kuendelea na Ubunge. Ndani ya siku moja?” amehoji Maalim. Ameongeza kuwa Spika amejiridhisha vipi ikiwa hata hakuwasiliana na Katibu Mkuu wa Chama ambaye kwa mujibu wa Katiba ya CUF ndiye Mtendaji Mkuu wa shughuli za chama na pia kwa nafasi hiyo ndiye katibu wa vikao vya Mkutano Mkuu wa Taifa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama? Amesema yeye kama katibu, alimuandikia Spika Ndugai barua, Jumanne, Julai 25 akimueleza kwamba hilo lililoitwa Baraza Kuu la Uongozi la CUF halikuundwa na wajumbe halali wa Baraza Kuu. “Angekuwa na nia ya kweli ya kutaka kujiridhisha si hapo ndipo pangekuwa pa kuanzia kwa kuwepo kile wanasheria wanachokiita shaka inayoweza kuingia akilini yaani ‘reasonable doubt’?’’ amehoji. Hata hivyoa amesema Spika Ndugai aliyapuuza yote hayo kwa sababu ni kinyume na mkakati wa Dola wa kuihujumu CUF na kuua demokrasia Tanzania. Hapo ndipo Spika Job Ndugai alipolifikisha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

MAAAMUZI YA BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA LA THE CIVIC UNITED FRONT (CUF - CHAMA CHA WANANCHI) KUHUSIANA NA HUJUMA ZA DOLA DHIDI YA CUF

Image may contain: 1 person
BARAZA Kuu la Uongozi la Taifa lilipokea, kujadili na kufanya maamuzi kuhusu ajenda moja tu iliyowasilishwa kwake na Kamati ya Utendaji ya Taifa ambayo ilikuwa ni: • Taarifa kuhusu kile kinachoitwa kuwavua uanachama Wabunge wanane (8) na Madiwani wawili (2) wa Viti Maalum kupitia CUF kilichotangazwa kufanywa na Ibrahim Lipumba na kikundi chake ikiwa ni mwendelezo wa hujuma za Dola dhidi ya Chama cha CUF. Baada ya mjadala wa kina, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa linapenda kutoa maazimio yafuatayo kuhusiana na tukio hilo na mwendelezo wa vitendo na matukio mengi ya hujuma yanayofanywa na Dola dhidi ya CUF:-

1. KUHUSU UHALALI WA BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA: Kutokana na mkanganyiko unaosababishwa na upotoshaji wa makusudi unaofanywa na Ibrahim Lipumba na kikundi chake wa kuitisha watu wa kuokota barabarani na kuwakusanya Buguruni huku akiwaita kuwa ndiyo Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF, tumeona kuna haja ya kuweka kumbukumbu sahihi ili kuepusha upotoshaji huo usiendelee. Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama huwa linaundwa kila baada ya miaka mitano kupitia Uchaguzi Mkuu wa Chama ndani ya Chama na hupata wajumbe wake kupitia uchaguzi unaofanywa na Mkutano Mkuu wa Taifa (wajumbe 25 kutoka Tanzania Bara na wajumbe 20 kutoka Zanzibar), wajumbe 14 wanaoteuliwa na Mwenyekiti kwa kushauriana na Makamu Mwenyekiti na kisha kuthibitishwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa, wajumbe wanaoingia kwa nafasi zao wakiwemo Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Chama, Wenyeviti na Makatibu wa Jumuiya za Chama na Viongozi wa Kambi za Wabunge na Wawakilishi wa Chama. Viongozi Wakuu wa kitaifa wa Chama pia ni wajumbe. Wafuatao ndiyo Wajumbe halali waliochaguliwa na Mkutano Mkuu wa Taifa uliomalizika Juni 27, 2014 hapo Ubungo Plaza, Dar es Salaam kuwa wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa (BKUT) watakaokaa madarakani kwa kipindi cha miaka mitano (2014 – 2019) hadi watakapochaguliwa wengine na Mkutano Mkuu wa Taifa kwa mujibu wa Katiba ya CUF ya mwaka 1992 (Toleo la 2014):- VIONGOZI WAKUU: 1. Mwenyekiti (alijiuzulu tarehe 5 Agosti, 2015 na kujiuzulu kwake kuthibitishwa na Mkutano Mkuu wa Taifa wa dharura tarehe 21 Agosti, 2016).

Mbunge wa Temeke akamatwa kihuni

Image result for ABDALL MTOLEA PICTURES

Kesi YA CUF DHIDI YA RITA KUUNGURUMA JULAI 10

 

Mashauri sita yaliyofunguliwa katika Mahakama Kuu na Bodi ya Wadhamini ya CUF yanatarajiwa kusikilizwa na baadhi yake kutajwa tarehe, Jumatatu ya Julai 10, 2017, baada ya leo kuahirishwa usikilizwaji wa kesi ya msingi ya wizi wa ruzuku ya chama hicho. Kufuatia mawakili upande wa mashitaka kutopewa nakala ya maombi ya pingamizi la Mwanasheria Mkuu wa Serikali. 
Wakati akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, Wakili wa CUF, Juma Nassoro amesema leo mahakama hiyo imewapatia nakala za pingamizi hilo.
Na kwamba, Jaji Wilfred Dyansobela anayesimamia mashauri hayo amesema Jumatatu ijayo mashauri yote yatasikilizwa na kutajwa tarehe ikiwemo la kupinga maamuzi ya RITA ya kusajili wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa .
Shauri lingine litakalosikilizwa siku hiyo ni la kuzuia fedha za ruzuku ya chama hicho kupewa Profesa Lipumba na wenzake.
Aidha, upande wa Lipumba kupitia Abdul Kambaya haikuridhishwa na maamuzi hayo ya mahakama ya kuahirisha usikilizwaji wa kesi hiyo ya msingi kwa madai kuwa yanachelewesha muda.
“Sisi tulikuja kwa agizo la mahakama, badala yake jaji hakutokea tukasikia juu kwa juu kuwa kesi imeahirishwa. Wanachokifanya ni kuchelewesha muda jumatatu watazikwa,” amesema.  

TAMKO LA MADIWANI WA THE CIVIC UNITED FRONT (CUF-CHAMA CHA WANANCHI) WA MKOA WA DAR ES SALAAM JUU YA KUUNGA MKONO HOTUBA NA MSIMAMO WA CHAMA ULIOTOLEWA NA KATIBU MKUU MAALIM SEIF SHARIF HAMAD TAREHE 28 JUNE 2017 KATIKA HOTEL YA PEACOCK:

4
Image may contain: 4 people, people sitting, table and indoor
THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF-CHAMA CHA WANANCHI)
TAMKO LA MADIWANI WA THE CIVIC UNITED FRONT (CUF-CHAMA CHA WANANCHI) WA MKOA WA DAR ES SALAAM JUU YA KUUNGA MKONO HOTUBA NA MSIMAMO WA CHAMA ULIOTOLEWA NA KATIBU MKUU MAALIM SEIF SHARIF HAMAD TAREHE 28 JUNE 2017 KATIKA HOTEL YA PEACOCK:
Tarehe 5 JULY, 2017
NDUGU WAANDISHI WA HABARI,
WAHESHIMIWA VIONGOZI WA CUF,
WAHESHIMIWA WANACHAMA WA CUF,
WAHESHIMIWA WANANCHI, MABIBI NA MABWANA,
NAOMBA NIANZE KWA KUWASALIMU KWA SALAMU ZA CHAMA CHETU HAKI SAWA KWA WOTE,
1. Awali ya yote, tuanze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kutujaalia uhai na uzima na kutuwezesha kukutana hapa asubuhi hii, kwa lengo la kutoa Tamko na msimamo wetu Rasmi juu ya sintofahamu inayoendelea ndani ya Chama chetu, na kuunga mkono Hotuba na msimamo wa Chama uliotolewa na Katibu Mkuu wetu, Maalim Seif Sharif Hamad. Tukiwa ni Madiwani wa CUF, kutoka Manispaa za Mkoa wa Dar es Salaam na kupitia kwenu ujumbe wetu uweze kuwafikia wana-CUF wenzetu, Wapenda Mabadiliko wote nchini, na Watanzania kwa Ujumla.
2. Tunapenda kuchukua fursa hii kuwashukuru nyinyi Waandishi wa Habari kwa kuhudhuria kwenu na mara zote kutukimbilia kila tunapokualikeni mbali na Changamoto mnazokabiliana nazo juu ya uhuru wa Habari na aina ya uongozi wa Serikali ya awamu ya Tano jinsi unavyoikandamiza demokrasia nchini na kutopenda kukosolewa.

BASHANGE AWATULIZA WANA CUF

ZANZIBAR STONE TOWN MEMBER OF PARLIAMENT STAND WITH GIRLS

I STAND FOR THE GIRLS ... PLEASE JOIN ME
Image result for ALLY SALEH PICTURES
By Ally Saleh
Many people have come to the defence of young girls who get into wrong side and become pregnant while still at school be it at primary level or secondary one and thus cut off from following their educational programs.
Thus means not only dreams but also hopes are dashed and buried in a grave that most of them would not be able even to trace as they grow old and lament only. But then lamenting will not be enough because their lack of education might be an obstacle to their development and end up in the poverty cycle.
Most people believe that pregnancy in young girls is never wanted but these young females are caught at a time when they are not only naïve but also at an age where foolishness is only thing they do. And on top of it both young men and those of old age with good cash flow pry on these innocent souls and and trap them.
Some feel it is cruel to blame a girl of 13 or even 16 and 17 to have willingly made a choice of entering sex life and hence with no education to protect herself from becoming pregnant but even from being passed with HIV AIDS or any other sexual transmitted diseases.
A month ago a debate ensued at the Parliament about change of the 1971 Law of Marriage Act in order to change marriage age in Tanzania and a big shout was recorded with two opposing sides arguing their cases with no results. Those who refuse lean on morality and those who want it be raised to be 18 lean of reality.
There not even consensus with the Cabinet Members as the then newly appointed Minister for Constitutional and Legal Affairs Professor Palmagamba Kabudi took a cautious approach saying the government was still synthesizing the issue while Minister for Women and Health Ummy Mwallimu skipping out of official Budget presentation notes indicated that things were moving on to effect changes.
But while the debate is still raging in the public domain with consensus being sought with activists charging time was up for the changes, the traditionalist especially those with religious inclinations have been saying this was only going to happen over their dead bodies.
The latter’s argument is that if a girl was pregnant and returned to classes after delivery will poison the others on their habits, which tends to assume that the only bad thing is to become pregnant ignoring the very act of having sex which is not committed only by the girl who becomes pregnant but many and most others around her.

MAALIM SEIF AWAPANDISHA RITA MAHAKAMANI

RITA) MAELEZO YA JUMLA YA KATIBU MKUU WA CUF, SEIF SHARIF HAMAD, KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA WA WATANZANIA JUU YA MUENDELEZO WA HUJUMA ZINAZOFANYWA NA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI JAJI FRANCIS MUTUNGI DHIDI YA CUF KWA KUTUMIA WAKALA WA USAJILI, UFILISI NA UDHAMINI (

PEACOCK HOTEL, DAR ES SALAAM, TAREHE 28 JUNE, 2017

Ndugu zangu wahariri na waandishi wa habari,

Awali ya yote nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kutujaalia uhai na uzima na kutuwezesha kukutana leo hapa. Nitumie fursa hii pia kuwapa mkono wa Eid Mubarak Waislamu wa hapa nchini pamoja na Waislamu wengine duniani wanaoendelea na maadhimisho ya sikukuu ya Eid-el-Fitr kufuatia kukamilika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Pili, nawashukuru na nyinyi Wahariri na waandishi wa habari kwa kupokea mwaliko wetu na kuhudhuria mkutano huu. Siku zote mmetupa mashirikiano makubwa katika shughuli zetu na kuufikisha ujumbe wetu kwa umma wa Watanzania na ulimwengu kwa ujumla. Ahsanteni sana.

Ndugu Wahariri na waandishi wa habari, mtakumbuka vyema tarehe 9 Aprili, 2017 katika ukumbi wa Hotel ya Ramada Encore Dar City Centre jijini Dar es Salaam, nilitoa maelezo ya kutosha kuhusu mbinu chafu iliyopangwa kufanywa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kwa maelekezo ya Dola kupitia Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kwa lengo la kumnusuru kibaraka wao Ibrahim Haruna Lipumba kwa kuhakikisha kwamba Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini feki waliopelekwa na kibaraka Lipumba wanasajiliwa baada ya kuona Bodi halali ya CUF - Chama Cha Wananchi ni kikwazo katika kufanikisha mipango yao haramu ya kufungua akaunti mpya ya benki ili kuwezesha wizi wa ruzuku ya Chama.

Katika mkutano huo, nilifafanua pia na kueleza kwa kina hujuma zinazofanywa na dola dhidi ya CUF - Chama Cha Wananchi hasa baada ya mafanikio makubwa na ushindi wa kutosha uliopatikana Zanzibar katika uchaguzi wa Oktoba, 2015. Sitoyarejea tena hapa niliyoyaeleza siku ile.

RITA YAKUBALI KUTUMIWA KATIKA MPANGO HARAMU

Niseme tu kwamba yale tuliyoyaeleza tarehe 9 Aprili yamethibitika wiki iliopita kwa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kutekeleza alichoagizwa kufanywa ambacho ni kusajili wajumbe feki wa Bodi ya Wadhamini ya CUF. Mtaona utekelezaji umechukua muda kwa sababu inaonekana baada ya kuzieleza njama zile hadharani na nyinyi vyombo vya habari kuziandika, RITA walishtuka na kudai bado wanayafanyia kazi maombi yaliyowasilishwa na wanahitaji kujiridhisha juu ya uhalali wa vyombo vilivyofamya mabadiliko yaliyowasilishwa kwao.

Nilieleza siku ile kwamba tokea kuanza kwa njama ovu na mbinu chafu hizi, moja ya vinavyoonekana vikwazo vikubwa vinavyokwamisha kufanikiwa malengo ya wanaomtumia kibaraka Ibrahim Lipumba imekuwa ni Bodi ya Wadhamini ya THE CIVIC UNITED FRONT (CUF - Chama Cha Wananchi) ambayo imechukua hatua madhubuti za kukilinda Chama na; hususan, rasilimali zake kupitia Mahakama na taratibu nyingine za kiutawala na kisheria. Hatua hizo zilizochukuliwa na Bodi ya CUF ni kwa mujibu wa Katiba ya Chama ya mwaka 1992(Toleo la 2014) kifungu cha 98(4) ambayo nanukuu:

"98(4) - Bodi inaweza kushtaki au kushitakiwa kwa niaba ya Chama"

Aidha mamlaka hayo yamebainishwa katika Sheria ya Wadhamini (The Trustees' Incorporation Act Cap.318), kifungu cha 8(1)(b), nanukuu:

"8(1) Upon the grant of a certificate under subsection (1) of section (5), the trustee or trustees shall become a body corporate by the name described in the certificate, and shall have;-

(b) power to sue and be sued in such corporate name"

Tunazo taarifa zisizo na shaka kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA amepata shinikizo kubwa kusajili wajumbe feki wa Bodi ya Wadhamini ya CUF kwa kutumia majina yaliyowasilishwa na kibaraka Lipumba ili kuhujumu majina halali yaliyopitishwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kupitia kikao chake kilichofanyika Makao Makuu ya Chama Zanzibar, tarehe 19 Machi, 2017. Afisa Mtendaji Mkuu huyo wa RITA amenukuliwa na vyombo vya habari kukiri hivyo alipohojiwa akiwa Dodoma kama ilivyonukuliwa na gazeti la Mwananchi toleo Na.6176 la tarehe 25 Juni, 2017. Aidha katika barua aliyomwandikia Kaimu Katibu Mkuu (cheo ambacho hakipo kwenye Katiba ya CUF), amebainisha wazi wazi kuwa usajili huo wa wajumbe feki wa Bodi ya CUF umezingatia barua mbili alizoandikiwa na Msajili wa Vyama vya Siasa zenye Kumb. Na. CHA.322/362/14/23 ya tarehe 4/4/2017 na Kumb. Na. CHA.322/362/14/30 ya tarehe 11/5/2017. Wakati akihojiwa na gazeti la Mwananchi, Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Mama Emmy Hudson, amejitetea na kuweka wazi kuwa mtu mahsusi wa kutoa majibu ya kwa nini yamesajiliwa majina feki ya Bodi ya CUF ni Msajili wa Vyama vya Siasa.

Pamoja na kwamba utetezi huo haumwondoi Mama Hudson kutiwa hatiani kwa kosa la matumizi mabaya ya madaraka kutokana na kwamba anayesajili Bodi sio Msajili ya Vyama vya Siasa bali ni yeye (RITA) na sheria inamtaka kujiridhisha na nyaraka zinazowasilishwa kwake na waombaji. Suala hilo limefafanuliwa vizuri na yeye mwenyewe kupitia taarifa yake kwa umma ya tarehe 29 Machi, 2017. Katika ibara ya (3) ya taarifa hiyo Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu na Kaimu Kabidhi Wasii Mkuu wa RITA, Mama Emmy K. Hudson anasema (nanukuu):

"Tarehe 27 Machi, 2017 Wakala ulipokea maombi ya Usajili wa Bodi mpya ya Wadhamini ya CUF. Kwa mujibu wa utaratibu, maombi hayo yakipokelewa hupitia katika hatua ya uchambuzi wa taarifa zilizowasilishwa ili kujiridhisha sababu za mabadiliko hayo, na kuangalia iwapo taratibu zilifuatwa katika upatikanaji wa wadhamini hao kwa kuzingatia maamuzi ya mkutano uliohusika kupitisha mabadiliko hayo, hii ni kwa mujibu wa kifungu 17(a). Hatua hii bado haijakamilika."

Maelezo hayo yamenukuliwa kutoka kwenye Sheria ya Wadhamini (The Trustees' Incorporation Act Cap. 318), kifungu cha 17(a) kinachotamka ifuatavyo:

"17 - No changes of the names of a person who is or who were trustee or trustees of a body corporate  or organization incorporated under this Act shall be authorised by the Registrar-General unless he is satisfied that-

a) There were held a lawful meeting of the body corporate or organization for the purpose of electing a person or persons as trustees of such a body corpotate or organization."

Ndugu Wahariri na waandishi wa habari, kwa sababu ya kutaka uelewa fasaha wa hujuma iliyofanywa na RITA akishirikiana na Msajili wa Vyama vya Siasa na kibaraka wake Lipumba kuhusiana na Bodi ya Wadhamini ya The Civic United Front (CUF - Chama Cha Wananchi), naomba kutoa maelezo ufafanuzi.

Bodi ya Wadhamini ya CUF ilisajiliwa mwaka 1993 kwa kufuata taratibu zote za kisheria (Sheria ya Vyama vya Siasa, Sura 258 na The Trustees' Incorporation Act Cap. 318) na kupatiwa hati ya usajili Na. ADG/T.1/1127. Sheria ya Wadhamini (The Trustees' Incorporation Act Cap. 318) kifungu cha 8(1a) kinasema Bodi iliyosajiliwa ni endelevu isipokuwa kama imefutwa. Hapa nanukuu:

"8(1). Upon the grant of a certificate under subsection (1) of section (5) the trustee or trustees shall become a body corporate by the name described in the certificate, and shall have;-

(a) perpetual succession and common seal"

CUF - Chama Cha Wananchi kimeendelea kuheshimu na kutekeleza  matakwa ya sheria hiyo kwa kuweka sawa kumbukumbu za Bodi yake na kufanya mabadiliko kila ilipobidi kwa mujibu wa Katiba ya Chama kifungu 98(1) na kuwalipia wadhamini ada ya kila mwaka (return of trustees) ambayo kwa sasa ni Tshs. 50,000/=. Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya CUF walifanyiwa mabadiliko madogo mara ya mwisho mwaka 2012 na imeendelea kulipiwa ada ya wadhamini ya kila mwaka hadi tarehe 24 Mei, 2017 kwa mujibu wa kumbukumbu ya stakabadhi ya malipo iliyotolewa na RITA tarehe 24 Mei, 2016 yenye Na.105888047. Kwa mantiki hiyo mabadiliko mengine ya wajumbe wa Bodi yalipaswa kufanya mwaka huu wa 2017.

CUF kupitia Baraza Kuu la Uongozi la Taifa lililochaguliwa kihalali kupitia Mkutano Mkuu wa Taifa wa mwezi Juni mwaka 2014 na kwa kufuata masharti mapya ya Katiba ya 1992 (Toleo la 2014) ilifanya mabadiliko machache ya wajumbe wa Bodi ya Wadhamini tarehe 19 Machi, 2017 na kuyawasilisha kupitia barua ya Katibu Mkuu Kumb. Na. CUF/HQ/AKM/003/RT/001 ya tarehe 24 Machi, 2017 kwa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA). Aidha pamoja na barua hiyo Fomu T.I.4 (Notification) na T.I.5 (Return of Trustees) na malipo ya Tshs. 100,000/= yalifanywa na kupatiwa stakabadhi mbili; Na.14995169 (Notification) na Na.14995170 (Return of Trustees) zote za tarehe 27 Machi, 2017.

Kuthibitisha kupokelewa kwa mabadiliko hayo, Msimamizi wa Wadhamini RITA alikiri kwa barua Kumb. Na.ADG/T.1/1127/29 ya tarehe 31 Machi, 2017 aliyomwandikia Katibu Mkuu wa CUF - Chama Cha Wananchi. Katika barua hiyo, Msimamizi wa Wadhamini alimjulisha Katibu Mkuu kuwa pindi taratibu zitakapokamilika atamtaarifu. Mpaka ninapozungumza nanyi hapa, Katibu Mkuu hajataarifiwa chochote, jambo ambalo linakinyima Chama chetu hata haki ya kukata rufaa kwa Waziri kwa mujibu wa sheria ya Wadhamini (The Trustees'  Incorporation Act Cap. 318), kifungu cha (27) kama kilivyonukuliwa hapa:

"27. Appeals
Any person aggrieved by the refusal of the Administrator-General to grant a certificate of incorporation or to approve a change of name, or by any conditions or directions inserted in any certificate of incorporation, or by the revocation of the incorporation of any body corporate may within twenty-one days after the notification of such refusal, conditions or directions or revocation, as the case may be, appeal to the Minister responsible for legal affairs and the Minister may make such order as the circumstances may require and except as aforesaid no appeal shall lie against any such refusal, conditions or directions or revocation."

Hata hivyo, mara baada ya kuwasilisha mabadiliko hayo, kibaraka Ibrahim Lipumba naye akatakiwa na Msajili haraka aandae majina yake na kuyafikisha RITA na kwamba Ofisi ya Msajili itatoa maelekezo kwa RITA nini wafanye. Ni dhahiri barua mbili za Msajili wa Vyama vya Siasa za tarehe 4/4/2017 yenye Kumb. Na. CHA.322/362/14/23 na tarehe 11/5/2017 yenye Kumb. Na. CHA.322/362/14/30 zilizonukuliwa na RITA katika barua ya kuitambua Bodi feki ya kibaraka Lipumba zinahusika na maelekezo hayo.

Lakini pamoja na maelekezo kutoka kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, RITA si kwamba amefanya kitu ambacho hakifahamu.  Mwezi Novemba, 2016 baada ya Bodi kumfungulia kesi Msajili wa Vyama vya Siasa (Shauri Na. 23/2016 ambalo liko Mahakama ya Rufaa), Msajili wa Vyama vya Siasa katika hatua za kutaka kujinusuru na mkono wa sheria aliwasiliana na RITA kupitia barua Kumb. Na. HA.322/362/14/30 ya tarehe 14 Novemba, 2016 akiomba kusaidiwa kughushi kumbukumbu za Bodi ya CUF ili ionekane Bodi imepita muda wake na hailipii ada zake tangu mwaka 2010.

Msajili wa Vyama vya Siasa akiwa Jaji wa Mahakama Kuu alifanya hivyo akijua fika kuwa anachomshawishi RITA kufanya ni kosa la jinai na ikizingatiwa kuwa mwezi Oktoba, 2016 alikamilisha uhakiki wa utekelezaji wa masharti ya usajili kwa vyama vya siasa vyote nchini, ambapo alivifuta vyama kadhaa visivyokidhi masharti hayo na CUF - Chama Cha Wananchi hakikuwa miongoni mwa vyama visivyokidhi masharti. Barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa Kumb. Na. HA.322/362/01/21 ya tarehe 24 Oktoba, 2016 kwa makatibu wakuu wa vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu ni ushahidi wa zoezi hilo la uhakiki.

Baada ya kupata taarifa hizo za muendelezo wa hujuma za Msajili wa Vyama vya Siasa kupitia RITA, Katibu Mkuu wa CUF aliandika barua Kumb. Na.  CUF/HQ/BRT/005/016/12 ya tarehe 10 Oktoba, 2016 kuitahadharisha RITA juu ya mipango hiyo iliyokuwa ikiratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa. Barua hiyo ya Katibu Mkuu iliambatanishwa na nyaraka za kughushi za Msajili wa Vyama vya Siasa na mfuasi wa kibaraka Lipumba anayeitwa Thomas Malima akijitambulisha kama Katibu wa Bodi zilizopelekwa Bank ya NMB Ilala katika harakati za kutaka kuiba fedha za ruzuku ya Chama.

Jambo la ajabu RITA licha ya kuwa na jopo kubwa la wanasheria, ilikubali ombi la Msajili wa Vyama vya Siasa na kwa barua Kumb. Na. ADG/T.1/1127/16 ya tarehe 15 Novemba, 2016 iliyosainiwa na Afisa wake anayeitwa Gilbert P. Bubelwa iliwasilisha nyaraka za kughushi zilizoambatanishwa kwenye hati ya kiapo ya Mwanasheria Mkuu wa serikali kupinga kufunguliwa kwa shauri dhidi ya Msajili wa Vyama vya Siasa. Jambo la kushangaza wameghushi mpaka sahihi ya kibaraka Lipumba licha ya kwamba ni mshirika wao.

Ndugu wahariri na waandishi wa habari, baada ya kugundua kuwa Chama kinazo nakala halisi na stakabadhi za malipo hadi mwaka 2016 na kwa hivyo nyaraka zao za kughushi haziwezi kuwasaidia, ndipo wakaja na njama hii ya pili ya kusajili Bodi feki kwa malengo makuu manne yafuatayo:-

1) Kufuta kesi zote zilizofunguliwa na ambazo zinawaelemea licha ya kutumia nguvu kubwa ya dola.

2) Kufungua akaunti mpya ya benki ili kumwezesha kibaraka Lipumba kupata ruzuku.

3) Bodi hiyo kuwezesha udhibiti wa Ofisi za Makao Makuu, Zanzibar.

4) Kumwondoa madarakani Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad na hivyo kufanikisha njama za kuwapokonya haki yao Wazanzibari kwa maamuzi yao ya tarehe 25 Oktoba, 2015.

Baada ya kupata taarifa za uhakika juu ya njama hizo ovu, na kupata stakabadhi ya malipo ya kibaraka Lipumba ya mabadiliko ya wajumbe wa Bodi yenye Na. 14995179 ya tarehe 27 Machi, 2017 iliyotolewa na RITA, Katibu Mkuu wa CUF alimwandikia tena barua RITA yenye Kumb. Na. CUF/HQ/AKM/003/017/01 ya tarehe 28 Machi, 2017 kumtahadharisha juu ya njama hizo kama alivyokuwa amefanya awali mwezo Novemba, 2016.

Aidha, Katibu wa Bodi halali ya Wadhamini, Mhe. Joran Bashange alikwenda RITA na kukutana na wanasheria Gilbert P. Bubelwa na Mwakatobe na kuwaeleza juu ya njama hizo ovu lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kuikabili hali hiyo. Jambo hilo linadhihirisha wazi kuwa njama, hujuma na mipango yote ya kuihujumu CUF ni ya dola. Kwa hali ilivyo ya utawala wa serikali ya awamu ya tano haingii akilini kama mtumishi yeyote wa umma anaweza kuwa na ujasiri wa kufanya makosa makubwa ya kijinai wazi wazi namna hii. Watawala wanafanya hivyo kwa kujidanganya kuwa wataweza kuidhibiti CUF na hivyo khofu yao ya madai ya Wazanzibari juu ya haki yao ya ushindi ulioporwa katika uchaguzi wa tarehe 25 Oktoba, 2015 itakuwa imetoweka. Aidha wanadhani kuwa Watanzania wanaoiamini CUF kama taasisi imara ya kuwaletea mabadiliko ya kweli watasambaratika.

Ndugu wahariri na waandishi wa habari, taarifa za kusajiliwa Bodi feki ya kibaraka Lipumba kwa shinikizo la dola kupitia Msajili wa vyama vya Siasa na RITA zilipatikana tarehe 20 Juni, 2017 ambapo mawakili wa Chama walitaarifiwa kwa njia ya simu na karani wa Mahakama kuwa Shauri Na. 21/2017 mbele ya Jaji Wilfred Dyansobera, dhidi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali lililokuwa limepangwa tarehe 3 Agosti, 2017 ghafla limerudishwa nyuma hadi Jumatano ya tarehe 21 Juni, 2017 (hakuna summons zilizotolewa). Aidha Jumanne, tarehe 20 Juni, 2017 wafuasi wa kibaraka Lipumba walianza kuandika kupitia mitandao ya kijamii wakihamasishana kukusanyika Ofisi Kuu Buguruni tarehe 21/6/2017 wakitangaza kwamba mambo yote yamekwisha. Baadaye CUF - Chama Cha Wananchi kikapata taarifa za uhakika kuwa RITA imesajili Bodi feki ya Lipumba, na kwamba tayari imekwishamtaarifu Jumamosi ya tarehe 17 Juni, 2017 na kwamba wanakwenda kufuta kesi zote ili pia Msajili aweze kuanza kuwapatia ruzuku.

Jumatano, tarehe 21 Juni, 2017 siku ambayo kesi ilipangwa kusikilizwa Afisa mwandamizi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Bw. Sisty L. Nyahoza alifika Mahakama Kuu ya Tanzania Dar es salaam na kufanya mazungumzo ya siri na uongozi wa Mahakama. Wakati mazungumzo hayo yanaendelea ilikuwa ikitangazwa kuwa mashauri yote mbele ya jaji Wilfred Dyansobera, yataanza kusikilizwa saa 4.00 asubuhi hivyo wenye mashauri waendelee kusubiri.

Jumatano hiyo ya tarehe 21 Juni, 2017 saa 3.20 za asubuhi (muda mfupi kabla ya shauri kuitwa) ndipo mawakili wetu  walipopatiwa barua mbili zilizosainiwa na mfuasi wa kibaraka Lipumba anayeitwa Thomas Malima akijitambulisha kuwa eti ni Katibu wa Bodi. Barua aliandikiwa Msajili wa Mahakama Kuu na kunakiliwa kwa Jaji Wilfred Dyansobera.

Ø Ya kwanza ikimtaarifu kuondolewa kwa mawakili wetu wasomi Juma Nassor, Daimu Halfani na Hashim Mziray na eti kumuajiri wakili msomi Makubi Kunju Makubi.

Ø Ya pili ikiomba kufutwa kwa Shauri Na. 21/2017 linalomkabili Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi la wizi wa fedha ya ruzuku ya Chama takriban Tshs.369 milioni. (Thomas Malima ambaye aliomba ajumuishwe kama mlalamikiwa "RESPONDENT" kwenye shauri hilo ghafla amejigeuza kuwa mlalamikaji na anawasilisha barua mahakamani kufuta kesi).

Kupitia muhtasari wa kugushi wa kilichoitwa kikao cha Bodi feki ya kibaraka Lipumba, kilichoketi Jumamosi tarehe 17 Juni, 2017 na kuhudhuriwa na wajumbe Jumatano tarehe 21 Juni, 2017 lakini barua kupelekwa kwa Msajili wa Mahakama Jumatatu tarehe 19 Juni, 2017, azimio la Bodi feki ni kufuta kesi zote zilizofunguliwa dhidi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, kibaraka Lipumba na wafuasi wake. Ni wazi nyaraka hizo zote ni za kughushi.

Ndugu Wahariri na waandishi wa habari, Chama chetu kimepatwa na mshtuko mkubwa sana, kuona taasisi kubwa na nyeti yenye dhamana kubwa katika nchi inaweza kufanya vitendo vya ovyo vya kughushi nyaraka kama hivyo. RITA ni taasisi inayobeba maisha ya watu ya kila siku. Licha ya kusajili Bodi za Wadhamini, inasajili vizazi na vifo, ndoa, talaka na inatunza WOSIA kwa ajili ya mirathi. Katika mazingira ya kujihusisha na vitendo vya ovyo, vilivyokosa maadili ya utumishi wa umma na vya kijinai kama hivi, itaaminikaje kwa wananchi na taasisi nyingine? RITA wameacha kuongozwa na weledi katika kutekeleza majukumu yao badala yake wamesukumwa na utashi binafsi wa kifisadi na hujuma dhidi ya taasisi ya CUF. Ukiipitia barua ya RITA kwa kibaraka Lipumba unajiuliza maswali kama imetoka kweli kwenye taasisi hiyo iliyosheheni wasomi na wanasheria waliobobea. RITA imedhihirisha kuwa sio chombo cha kutenda haki na kusimamia misingi yake. Yumkini ndiyo sababu Jaji Wilfred Dyansobera ameamua Mtendaji wa RITA afike mahakamani kutoa ushahidi.

Ni aibu kubwa maana pamoja na kupokea majina feki ya kibaraka Lipumba tuliamini angetimiza ahadi aliyokuwa ameitoa kwenye taarifa yake mwenyewe kwa umma kwamba atafanya uchambuzi na kujiridhisha kama yalivyo matakwa ya sheria na si kushirikiana na mhalifu Francis Mutungi ambaye RITA wanafahamu wazi kuwa ni mlalamikiwa kwenye kesi na amekwisha waingiza kwenye mgogoro na Mahakama kufuatia nyaraka za kughushi alozoambatanisha pamoja na hati ya kiapo kwenye shauri Na. 23/2016.

Katibu Mkuu ameandika barua tatu kati ya 31 Machi na 6 Juni, 2017 akiomba kukutana na Kabidhi Wasii Mkuu wa RITA, bila ya mafanikio yoyote. Katibu Mkuu ndiye mtunza kumbukumbu zote za wajumbe wa vikao vyote vya kitaifa na jinsi wanavyopatikana. Kitendo cha RITA kukataa kumpa nafasi Katibu Mkuu kukutana naye wakati akifanya hivyo kwa kibaraka Lipumba kunadhihirisha kuwa alichokifanya hakikuwa cha bahati mbaya bali alidhamiria. Ni dhahiri RITA wamejiunga na Jaji Francis Mutungi sio tu kuivuruga CUF bali kuzizamisha ndoto za Wazanzibari juu ya haki yao ya maamuzi waliyoyafanya Oktoba 25, 2015 kwa lengo la kuididimiza demokrasia nchini.

HATUA TUTAKAZOCHUKUA:

Baada ya kupata taarifa hizi kupitia Mahakama Kuu tarehe 21 Juni, 2017, Kamati ya Utendaji ya Taifa ilikutana mjini Zanzibar tarehe 22 Juni, 2017 na kuazimia yafuatayo:

1. Kufungua kesi dhidi ya RITA kwa kukiuka taratibu za Sheria ya Wadhamini (The Trustees' Incorporation Act Cap. 318) kama nilivyonukuu vifungu mbali mbali hapo juu, kwa kutojiridhisha juu ya uhalali wa majina ya Bodi ya Wadhamini ya CUF yaliyofikishwa kwake na iwapo yamefanywa na kikao halali cha Chama chenye mamlaka hayo kwa mujibu wa Katiba ya Chama.

2. Kuwasilisha maombi mbele ya Mahakama Kuu kuitaka isimamishe kesi nyengine zote tulizozifungua kuhusiana na kadhia hii hadi hapo shauri linalohusu uhalali wa maamuzi ya RITA litakapoamuliwa.

Ni imani yangu na imani ya CUF kikiwa ni chama chenye wanachama wapatao milioni mbili na mamilioni ya wafuasi hapa nchini kwamba Mahakama Kuu zitaona umuhimu wa kulitendea haki suala hili ili kuiepusha nchi yetu na mgogoro usio na sababu zaidi ya malengo ya muda mfupi ya baadhi ya watu wanaodhani kwamba kwa kuihujumu CUF watafanikiwa.

Asanteni sana kwa kunisikiliza.

HAKI SAWA KWA WOTE

Seif Sharif Hamad,
Katibu Mkuuu,
Chama Cha Wananchi (CUF),
28 Juni 2017, Dar Es Salaam


CHAMA CHA CUF CHAZINDUA OFISI YA WABUNGE HUKO DAR


WABUNGE WA CUF PAMOJA NA VIONGOZI WENGINE WAKIFUTURU BAADA YA UFUNGUZI WA OFSI MPYA YA WABUNGE HUKO MAGOMENI DAR



IKIWA ni takribani miezi 10 sasa kwa Chama cha Wananchi (CUF), upande wa Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif
Hamad kuvamiwa katika Ofisi Kuu za Bugurunina kundi la Profesa Ibrahim Lipumba chama hicho kimezindua ofisi mpya za chama hicho katika eneo la Mtaa wa Idrisa,
Kata ya Mzimuni, wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Image may contain: 1 person, standing

Aidha, Seif amesisitiza kuwa hatarajii kukutana na  Profesa Lipumba kwa kile alichodai kuwa hatambuliki katika chama na hana  sifa hizo kwa sasa.  Akizindua ofisi hiyo ambayo lengo kubwa ni kwa ajili ya wabunge 40 wa CUF, Seif alisema  uamuzi wa wabunge hao kumpatia ofisi ya kufanyia kazi hapo ni cha kiungwana na kinahitajika kuungwa mkono na wanachama wote.
Image may contain: 3 people, people sitting

Alisema kwa muda wa miezi 10 sasa wamekuwa wakishindwa kufanya kazi hasa upande wa Tanzania Bara
jambo ambalo limewaathiri sana hivyo kupatiwa ofisi kutamsaidia kutimiza majukumu yake vilivyo bila hofu yoyote.Maalim Seif alisema kukosa ofisi kumewaathiri sana katika baadhi ya mambo hivyo anaamini kwa sasa akifikia Dar es Salaam anamahali pa kukutana na wakurugenzi wake.
Image may contain: 1 person, eating, sitting, food and indoor

“Nimekuwa ni kija hapa nakosa sehemu ya kukutana na wakurugenzi, viongozi mbalimbali wanachama ila hiki ambacho wabunge wamefanya ni cha kuungwa mkono sijawahi kufanya kazi na wabunge wanao kipenda chama kama kipindi hiki,” alisema.


Katibu huyo alisema atahakikisha kuwa anaanza kazi haraka iwezekanavyo kwa kukutana na wakurugenzi wake ili waweze kutekeleza majukumu ya chama.
Image may contain: 1 person, sitting and food

“Hakuna shaka kuwa hu u unaoitwa mgogoro umeturudisha nyuma sana hivyo naamini wakati wa kufanyakazi umerejea na hawa wabaya wetu hawata ambulia kitu kwani CUF ni  chama imara hakitikisiki,” alisema.
Maalim Seif alisema jitihada zinazofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kukimaliza chama ni kubwa lakini hawataweza kufikia lengo hilo kutokana na misingi ya chama hicho.
Image may contain: 3 people, people sitting
Alisema kwa sasaa atafanya kazi katika ofisi hiyo ambayo amepewa na wabunge hadi hapo muafaka wa ofisi kuu Buguruni utakapopatikana huku akisisitiza kuwa haki haipotei ila inachelewa.Katibu huyo alisema anaimani na   mahakama kuwa ita wapatia haki stahiki hivyo kuwataka wanachama kuendelea kuwa na subira.

Image may contain: 1 person, sitting and eating
Aidha, alisema kupitia mgogoro huo hadi sasa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini inashikilia zaidi ya sh. bilioni 1.2 ambazo ni ruzuku ya chamahicho.Maalim Seif alisema fedha hizo ni pamoja na zile ambazo ofisi ya msajili ilimpatia Lipumba hivyo waamini mgogoro ukiisha wata pata haki yao.

Kwa upande mwingine Katibu huyo alisema hana mpango wa kukutana naLipumba kuhusu mgogoro unaondelea ndani ya chama hicho kwa kile alichodai kuwa si kiongozi wala mwanachama wa chama hicho.Alisema CUF haimtambui Lipumba kwa sifa yoyote tofauti na kumfukuza uanachama hivyo yeye hawezi kukukutana na mtu  kamahuyo.
Image may contain: 1 person, sitting

Maalim Seif alisema pamoja na kuwa hawamtambui Lipumba kama kiongozi au mwanachama ila akiomba msamaha wapo tayari kumsamehe.
Akizungumza baada ya kuzinduliwa ofisi hizo Mbunge wa Viti Maalum na Kiongozi wa Wabunge wa CUF bungeni, Riziki Ngwali alisema wamelazimika kufungua ofisi nyingine ili wapate mahali pa kukutana wakiwa nje ya Bunge.
Image may contain: 1 person, standing

Ngwali alisema kupitia ofisi hiyo wataweza kujadiliana
mambo mbalimbali yanayo wahusu wabunge na wananchi na kuja na ufumbuzi.
Kwa upande wake Mbunge wa Temeke CUF, Abdallah Mtolea alisema katika ofisi hiyo wanatarajia kuajiri wataalam mbalimbali ambao watasaidia kufanya tafiti na kupitia tarifa mbalimbali za Bunge ili kuwarahisishia katika uchangiaji bungeni.


Alisema katika ofisi hizo wameingia mkataba wa kulipa sh. milioni 18 kwa mwaka ambazo zitatolewa na wabunge wenyewe kwa maslahi ya chama chao.

MBUNGE WA STONE TOWN ALI SALEH AWASOMESHA SHERIA BUNGENI

MSAJILI ANAPOSUTWA NA WANACUF

KIKAO KATI YA UJUMBE WA CUF NA KAMISHNA SIRRO


                   
                    CUF KUWASULHISHA POLISI NA MAJAMBAZI .

Image may contain: 5 people, people standing
Imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Taifa, Mhe. Julius S. Mtatiro Tumemaliza kikao na Kamishna Sirro (Mimi nikiambatana na Wakurugenzi wa kitaifa na Wajumbe wa Baraza Kuu wa CUF) ;
Kamishna Sirro ana roho ya kipekee sana ni Ofisa wa Polisi wa mfano, ametupokea na ametupatia ushirikiano mkubwa sana.


1. Tumempa barua rasmi na ushahidi wa matukio yote ya jinai ambayo chama kimetendewa tangu Agosti mwaka 2016 huku wafanya matukio hayo mabaya wakilindwa.
2. Tumezungumza kwa kina juu ya tukio la Uvamizi wa Vina Hotel na kutaka hatua zichukuliwe haraka.
3. Kamishna Sirro amesikitishwa sana kusikia kuwa viongozi wa chama wameitwa Magomeni ili wapatanishwe na wavamizi/majambazi/mungiki/mazombi. Sirro amekataa utaratibu huo na anasema kuwa makosa ya jinai hupelekwa mahakamani, hayasuluhishwi na Polisi.
4. Tumemkumbushia Kamishna matukio 13 ya jinai ambayo yametendwa na Lipumba na genge lake dhidi ya chama yakiwemo kuteka, kupiga, kuchoma visu, kuvamia n.k. tumemwambia kuwa katika matukio yote hayo, Lipumba na genge lake wameendelea kulindwa.
5. Tumemweleza Kamishna kuwa sisi tumeendelea kuwataka wanachama wawe watulivu ili tuone hatua za POLISI na kwamba hatua zisipochukuliwa, sisi tutachukua hatua.
6. Tumemkumbusha Kamishna Sirro kuwa sisi (chama) ni wengi kuliko Lipumba na Genge lake na kwamba wingi wetu ni silaha kubwa sana na kwamba tunao uwezo wa kuwasambaratisha mara 100 ikiwa tunataka. Lakini sisi bado ni wastahimilivu, tunataka kuona hatua zinachukuliwa na POLISI
7. Kamishna Sirro ameahidi kuwa anachukua hatua, ameelekeza mapungufu yetu, amekubali baadhi ya mapungufu yao na kutoa maelezo baadhi ya mambo muhimu. Hatuwezi kumhukumu Sirro kwa sasa, ila tutamhukumu tukishaona hakuna hatua zinazochukuliwa.
Na Julius Matatiro.

MAZUNGUMZO YA WAANDISHI WA HABARI NA KATIBU MKUU.

HOTUBA YA KATIBU MKUU WA THE CIVIC UNITED FRONT (CUF - CHAMA CHA WANANCHI), MAALIM SEIF SHARIF HAMAD KATIKA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI KUZUNGUMZIA HUJUMA ZA DOLA KWA KUMTUMIA KIBARAKA IBRAHIM LIPUMBA DHIDI YA CUF NA MWELEKEO WA HARAKATI ZETU RAMADA ENCORE DAR

CITY CENTRE – 09 APRILI, 2017 Ndugu zangu Wahariri na Waandishi wa Habari, Awali ya yote, nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kutujaalia uhai na uzima na kutuwezesha kukutana hapa asubuhi hii kwa lengo la kufichua njama na mbinu chafu za Dola kwa kumtumia kibaraka Ibrahim Lipumba dhidi ya chama chetu, THE CIVIC UNITED FRONT (CUF – Chama Cha Wananchi), baada ya kuishiwa na mikakati ya kisiasa ya kukisaidia Chama Cha Mapinduzi ambacho sasa kinaelekea kwenye kukata roho. Nitayaeleza hayo kwa kina muda mfupi ujao. Pili, nawashukuru na nyinyi Wahariri na Waandishi wa Habari kwa kuupokea mwaliko wetu na kuhudhuria mkutano huu. Siku zote mmetupa mashirikiano makubwa katika kuhudhuria shughuli zetu na kuufikisha ujumbe wetu kwa Watanzania na kwa ulimwengu kwa jumla. Kwa hayo yote, nasema Ahsanteni sana. KWA NINI TUMEWAITA LEO?

 Kwa takriban wiki moja sasa nimekuwa na ziara ya kuimarisha Chama kisiwani Unguja baada ya kumaliza ziara kama hiyo kisiwani Pemba. Hata hivyo, nimeamua kukatisha ziara hiyo kwa siku ya leo ili kuja kuzungumza nanyi, na kupitia kwenu kuzungumza na Watanzania na jumuiya ya kimataifa kwa ujumla, kutokana na hali tuliyofikia, ambapo tusipochukua hatua za tahadhari kama Watanzania, inaweza ikaiingiza nchi yetu katika mgogoro mkubwa sana kuwahi kushuhudiwa katika historia yetu. Si siri tena sasa kwamba kile kinachoitwa ‘mgogoro wa uongozi’ ndani ya CUF si chochote bali ni hujuma zilizopangwa na zinazoendeshwa na Dola kupitia njama ovu na mbinu chafu kwa lengo la kuua Upinzani makini hapa nchini ikiwa ni sehemu ya kile kinachoonekana ni mkakati mpana wa kunyamazisha kila sauti inayothubutu kuwakosoa watawala. Nataka ifahamike kwamba lengo la njama ovu na mbinu chafu hizi siyo CUF; lengo ni Upinzani na hasa UKAWA na lengo pana zaidi ni kuua demokrasia Tanzania kwa kuhujumu na kuziua taasisi zote zinazoonekana kuwa ni nguzo za demokrasia yetu. CUF ni taasisi moja tu katika mapambano ya Dola dhidi ya taasisi za kidemokrasia zinazoonekana kuwaamsha Watanzania na ambazo zinaonekana kama kikwazo kikubwa dhidi ya watawala walioingia madarakani mwaka 2015 na ambao wana hofu kubwa ya kuendelea kubakia madarakani kutokana na mwamko mkubwa ulioonyeshwa na Watanzania kuanzia kwenye uchaguzi mkuu wa 2015. Ndiyo maana hujuma hizi zimeelekezwa kwa Bunge, vyama vya siasa, taasisi na jumuiya za kijamii na kiraia hususan zile zinazosimamia Haki za Binadamu na uhuru wa kujieleza, watumiaji wa mitandao ya kijamii hasa wakosoaji wa watawala, wasanii hasa wale wanaotumia vipaji vyao kukosoa watawala na kuwazindua Watanzania, vyombo vya habari na waandishi wa habari na sasa inaonekana hata kwa wanasiasa wa ndani ya Chama Cha Mapinduzi wanaoonekana kuwa na uthubutu wa kusimamia wanachokiamini na kutofautiana na watawala walioingia madarakani 2015. Kuthibitisha ninayoyasema, tuangalie mtiririko wa utekelezaji wa njama ovu na mbinu chafu hizi za kutaka kuua demokrasia kwa kunyamazisha taasisi zote zinazothubutu kutoa mawazo tofauti na yale ya watawala walioingia madarakani 2015.

Tumeshuhudia mambo mengi lakini hapa nitataja mifano kumi (10):- 1. Kupiga marufuku mikutano ya hadhara na maandamano ya vyama vya siasa nchi nzima. 2. Kuzuia matangazo ya moja kwa moja (live broadcasting) ya mikutano ya Bunge ili kuwaziba macho na masikio Watanzania wasisikie mijadala ya Bunge na kuona jinsi Serikali inavyowajibika na kuwajibishwa na Wabunge ambao ndiyo wawakilishi wa wananchi waliochaguliwa kwa lengo la kuwasemea wananchi kutoka katika majimbo yao. 3. Kufinya bajeti ya shughuli za Bunge na hasa Kamati za Bunge ili zisiweze kufanya kazi ya kuisimamia Serikali, kuchunguza mapungufu ya viongozi na watendaji wa Serikali na ili zishindwe kufuatilia ahadi za watawala walizozitoa kwenye kampeni na kupitia mipango ya bajeti. 4. Kuwakamata, kuwabughudhi, kuwalaza ndani na kuwafungulia mashtaka Wabunge wa Upinzani hasa wale wanaoonekana kuwa mwiba mkali kwa watawala ili kuwatisha na kuwanyamazisha wasifanye kazi yao ya kuwakosoa watawala. 5.

 Kuzipa Mahakama maagizo hadharani ya jinsi ya kuamua kesi na hata kufikia kusema hadharani kwamba Serikali itawapa fedha wanazozihitaji kwa uendeshaji wa Mahakama ikiwa na Mahakama nazo zitaihakikishia Serikali kupata mapato kiasi fulani kupitia hukumu za faini na fidia. 6. Kuwakamata, kuwaweka ndani na kuwafungulia mashtaka watumiaji wa mitandao ya kijamii, wengi wao wakiwa ni vijana, wanaoandika maoni yao kuwakosoa watawala kwa kutumia Sheria ya Makosa ya Mtandao (Cybercrimes Act), sheria ambayo tokea awali ilipingwa kwa kuwa ni sheria kandamizi. 7. Kuwatisha waandishi wa habari na vyombo vya habari hadharani na kufikia hatua ya kuyafungia magazeti yanayoongoza kwa kuandika habari zinazokosoa watawala na kuwakamata na kuwashtaki wahariri na waandishi wa habari. Tumeshuhudia watawala wakivamia vituo vya radio wakiwa na walinzi na kutoa vitisho kwa wafanyakazi wa radio hizo kwa sababu tu radio hizo zilikataa kurusha vipindi vyao. 8. Kuwatisha na kuwakamata wasanii hasa wale wanaotumia vipaji vyao katika kuwakosoa watawala na kuwazindua Watanzania juu ya mwenendo wa Serikali. 9. Kuzitisha Jumuiya za kiraia zinazojishughulisha na masuala ya haki za binadamu, sheria na utawala bora kwa lengo la kuzinyamazisha ili zisitimize wajibu wao kwa jamii. Mfano wa karibuni kabisa ukiwa ni wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) ambapo Waziri alifikia hatua ya kutishia kukifuta iwapo wanasheria wangetumia uhuru wao kuchagua mtu asiyetakiwa na Dola kuwa Rais wao.

hapo, watawala wamewatisha Mawakili kwa kuwapa maagizo Polisi hadharani kwamba Mawakili watakaowatetea au watakaowaombea dhamana watuhumiwa wa aina fulani basi na wao wawekwe ndani. 10. Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kujipa mamlaka wasiyokuwa nayo kisheria ya kuita watu Polisi, kutoa amri wakamatwe na kuwekwa ndan, jambo ambalo limelalamikiwa hata na Mkurugenzi mstaafu wa Makosa ya Jinai, Mhe. Adadi Rajabu kwamba ni kinyume na sharia. Hatua hizi za ukandamizaji wa demokrasia zimeharibu kabisa taswira ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndani na nje ya nchi, taswira ambayo ilijengwa kwa miaka mingi na waasisi wa Taifa letu. Leo hii tumefikia hadi vyombo vya habari vya kimataifa vinavyoheshimika vinaiandika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama nchi inayoshuhudia kutekwa nyara na kupotea kwa raia wake wanaojulikana kwa kukosoa watawala waliopo. Jumuiya za Kimataifa zimeanza kuinyooshea kidole Tanzania kwa ukiukwaji na uvunjwaji wa haki za binadamu. Ripoti ya kila mwaka ya Shirika la Kutetea Haki za Binadamu Duniani (Amnesty International) ya mwaka 2016 imeitaja Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zinazokandamiza haki za binadamu kwa kiasi kikubwa katika Afrika Mashariki. HUJUMA DHIDI YA CUF Ndugu zangu Wahariri na Waandishi wa Habari, Njama na hujuma hizi za Dola dhidi ya taasisi za kidemokrassia hazikuviacha vyama vya siasa vilivyo makini. Niligusia hapo awali matamko ya watawala ya kuzuia maandamano na mikutano ya hadhara ya kisiasa, baadhi ya Wabunge wa Jamhuri ya Muungano kukamatwa na kufunguliwa mashtaka ya kubambikiziwa na wengine kufungwa, viongozi wengi wa vyama vya siasa kutakiwa kuripoti Polisi, kutishwa, kukamatwa na kuwekwa ndani, wengine wamefunguliwa kesi na wengine bila hata kufunguliwa kesi. Kwa upande mwengine, kama nilivyotangulia kusema hapo awali, katika njama za kudhoofisha upinzani imara na hatimaye kuua kabisa demokrasia nchini, Chama Cha Wananchi – CUF kimepandikiziwa kile kinachoitwa ‘mgogoro wa uongozi’ kwa kumtumia kibaraka Ibrahim Haruna Lipumba. Wengi mnaweza kujiuliza kwa nini iwe CUF? Sababu kubwa ni kwamba CUF imekuwa ni taasisi imara isiyoyumba katika kuifikia dhamira na malengo iliyojiwekea.

Tokea mwaka 1992 pale mfumo wa vyama vingi vya siasa uliporuhusiwa tena katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, CUF kimejipambanua na kimeonyesha uwezo wa kujipanga katika kuwatumikia wananchi na wananchi kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wakakikubali na kukiunga mkono. Kwa upande wa Zanzibar, kila mtu anajua kwamba asilimia kubwa sana inayopita zaidi ya nusu ya Wazanzibari wanakiunga mkono. Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ulikuwa ni kilele cha mafanikio na ushahidi wa wazi wa kuithibitishia dunia kuwa CUF ndio chaguo la wananchi wa Zanzibar. Matokeo haya hayakuwaridhisha watawala hata kidogo. Licha ya kutumia nguvu kubwa ikiwemo ile ya kijeshi na kwa kumtumia Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, kuiminya demokrasia isikuchukue mkondo wake kwa kuyapindua maamuzi halali ya wananchi wa Zanzibar, bado wananchi wa Zanzibar wanaendelea kuungana na kuwakataa vibaraka waliowekwa madarakani kwa nguvu. Khofu hii ndio iliyojengeka katika mioyo ya watawala. Wanatishwa na kivuli chao kila uchao. Kwa misingi hii, ndio mpango wa kumtumia kibaraka Ibrahim Haruna Lipumba ulipopangwa na kufuatiwa na njama na hujuma chafu mbali mbali zinazofanywa dhidi ya CUF.

zinaonyesha kuwa njama hizi zilianza mara baada ya kibaraka Ibrahim Haruna Lipumba kukaribishwa Ikulu mapema mwaka jana. Sikusudii kurudia tena kwa urefu mtiririko wa matukio yaliyoanzia wakati huo lakini kwa ufupi niseme nyote mnakumbuka sinema ya Lipumba, iliyoanza mara baada ya ziara yake ya Ikulu. Kwanza alitumiwa kutushawishi kushiriki uchaguzi haramu wa marudio wa Machi 20, mwaka jana huku akinambia mimi kuwa nikubali kwani angalau nitaweza kuendelea kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, kisha akadai ametengua barua yake ya kujiuzulu, akavamia Mkutano Mkuu wa Taifa wa Chama na kuuvuruga huku akilindwa na Polisi, na hatimaye akatumiwa Msajili wa Vyama vya Siasa ambaye alijipa mamlaka asiyokuwa nayo eti kubatilisha maamuzi halali ya vikao halali vya Chama na kulazimisha Lipumba atambuliwe kuwa Mwenyekiti. Baada ya hapo, sinema ikaendelea kwa kuvamia Ofisi Kuu ya Chama Dar es Salaam kwa msaada wa Polisi, kutangaza eti kawatengua viongozi halali wa Chama wakati yeye akiwa si mwanachama tena baada ya kufukuzwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama, na hatimaye kiroja cha mwisho kuokota watu barabarani na kuwapachika jina la eti ni wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa na kufanya maamuzi aliyoyaita ya Chama.

 Tokea Jaji Francis Mutungi, Msajili wa Vyama vya Siasa kujipa mamlaka asiyokuwa nayo ya kutangaza kumtambua kibaraka Ibrahim Lipumba eti kuwa Mwenyekiti wa CUF hadi hivi sasa kuna hujuma zilizoambatana na mbinu chafu zilizofanywa dhidi ya CUF na nyengine zinaendelea kufanyika. Baadhi ya hujuma hizo ni pamoja na:- 1. Kwa kutumia vyombo vya dola kumzuia Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad, kufanya shughuli zake za kisiasa kwa upande wa Tanzania Bara na huku vyombo hivyo hivyo vikimlinda kwa nguvu kubwa kibaraka Ibrahim Haruna Lipumba kukihujumu chama. 2. Kwa mashirikiano na vyombo vya dola, kibaraka Ibrahim Haruna Lipumba ameteka na kuvamia kwa nguvu ofisi za Chama za Wilaya mbali mbali nchini chini ya ulinzi wa vyombo vya dola. 3. Wizi wa fedha za ruzuku za chama kiasi cha TSh. 369 milioni uliofanikishwa kwa mashirikiano ya pamoja kati ya Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi, Hazina, Lipumba na Benki ya NMB. 4. Njama za kujaribu kumuengua Katibu Mkuu wa CUF kama zilivyobainishwa katika mawasiliano ya siri kati ya Msajili wa Vyama vya Siasa na kibaraka Ibrahim Haruna Lipumba. 5. Bunge kupokea wagombea feki waliopitishwa na Baraza Kuu feki la watu wasio wajumbe ambao waliokotwa barabarani na kumchagua Mohamed Habib Mnyaa kama mwakilishi wa CUF katika Bunge la Afrika Mashariki, mtu ambaye si tu kuwa hakupitishwa na Chama, wala jina lake kuwasilishwa katika Ofisi za Katibu wa Bunge na Katibu Mkuu wa Chama kama ambavyo Kanuni za Bunge zinataka, lakini pia mtu huyu si mwanachama wa Chama Cha Wananchi – CUF kwani alikwishafukuzwa uanachama na tawi lake la Mkanyageni, kisiwani Pemba.

Ndugu zangu Wahiriri na Waandishi wa Habari, Uchafu huu wote uliofanywa kwa mashirikiano makubwa na Dola (kupitia mamlaka za umma kama Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa, Polisi, Hazina, na hivi karibuni Ofisi ya Bunge) unaonekana bado haujafikia lengo kuu ambalo ni kuisambaratisha CUF. Tunaelezwa kuwa lengo kuu hasa ni Maalim Seif Sharif Hamad ambaye anaonekana kuwa mwiba mkali kwa CCM, dhambi yake kuu ikiwa ni kushinda kwa asilimia kubwa uchaguzi mkuu wa Urais wa Zanzibar mwaka 2015, na pia kule kubakia kwake kuwa nguzo kuu ya CUF katika kuuendeleza umoja wa wapinzani (UKAWA) ambao unahatarisha nafasi ya CCM katika siasa za Tanzania. Haya tuliarifiwa mapema na tuliyatolea taarifa kwa Watanzania ili wayajue na yamethibitishwa na matamko ya kipuuzi ya kibaraka Ibrahim Haruna Lipumba aliyoyatoa wiki iliopita. NJAMA ZA KUITUMIA RITA KUHITIMISHA MPANGO WAO: Baada ya kuona hawajafanikiwa na CUF imesimama imara kujilinda kupitia hatua za kisheria, sasa Dola imeamua kukamilisha mpango wake mchafu kwa kutumia Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA).


Tokea kuanza kwa njama ovu na mbinu chafu hizi, moja ya vinavyoonekana vikwazo vikubwa vinavyokwamisha kufanikiwa malengo yake imekuwa ni Bodi ya Wadhamini ya The Civic United Front (CUF – Chama Cha Wananchi) ambayo imechukua hatua madhubuti za kukilinda Chama kupitia Mahakama na taratibu nyingine za kiutawala na kisheria. Sasa njama mpya zinazofanywa ni kukiondosha hiki kinachoonekana kuwa ni kikwazo kwao. Tunazo taarifa zisizo na shaka kuwa, kuna shindikizo kubwa la kumtaka Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA kusajili wajumbe feki wa Bodi ya Wadhamini ya CUF kwa kutumia majina yaliyowasilishwa na kibaraka Ibrahim Haruna Lipumba ili kuhujumu majina halali yaliyowasilishwa na kikao halali cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kilichofanyika makao makuu ya Chama, mjini Zanzibar tarehe 19 Machi, 2017. Nitoe maelezo mafupi kuhusiana na hili ili lieleweke vizuri. Kimsingi, Bodi ya Wadhamini ya CUF ilikwisha sajiliwa tokea 1993, kwa kufuata taratibu zote zilizoelekezwa na Sheria ya Wadhamini (The Trustees’ Incorporation Act – Cap 318) na Hati ya Usajili tunayo. Kinachofanyika kila baada ya kipindi fulani ni kuweka sawa kumbukumbu za bodi hiyo kwa kuwalipia wadhamini na kuingiza kwenye kumbukumbu mabadiliko ya wajumbe kadiri yanavyofanyika kwa mujibu wa Katiba ya CUF. CUF, kupitia Baraza Kuu la Uongozi la Taifa lililochaguliwa kihalali katika Mkutano Mkuu wa Taifa wa mwaka 2014, na kwa kufuata masharti ya Ibara ya 98 ya Katiba ya CUF ya mwaka 1992 (Toleo la 2014) imefanya mabadiliko machache ya wajumbe wa Bodi ya Wadhamini na kuyawasilisha RITA, ambapo yalipokelewa na kupatiwa stakbadhi ya malipo yake.

Hata hivyo, mara baada ya kuwasilisha mabadiliko hayo machache, kibaraka Ibrahim Haruna Lipumba na yeye akatakiwa haraka aandae majina yake na kuyafikisha RITA huku akihakikishiwa kwamba RITA itapewa maelekezo ya nini cha kufanya. Lengo la njama hizi ni kumuwezesha kibaraka Lipumba kuwa na ‘Bodi ya Wadhamini’ ambayo itatumika, kwanza, kufuta kesi zote zinazomkabili yeye na genge lake na Msajili wa Vyama Vya Siasa ambaye yuko katikati kwenye hujuma hizi zote. Lengo la pili ni kufungua akaunti mpya ya benki na kuwezesha kupatikana kwa fedha za ruzuku za Chama na mwisho Bodi hiyo mpya kudhibiti Ofisi za Makao Makuu ya Chama zilizopo Mtendeni, Zanzibar na kumuondoa Katibu Mkuu wa Chama. Kufikia hatua hiyo watawala wanadhani watakuwa wamejiridhisha kuwa wameweza kuidhibiti CUF na khofu yao kwa CUF itakuwa imeondoka. Wanavyojidanganya ni kwamba madai ya Wazanzibari juu ya haki yao ya ushindi ulioporwa katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015 yatakuwa yameishia hapo na hatua zote zilizofanyika zitakuwa zimekwamishwa. Na mwisho, wanajiaminisha kwamba kufikia hapo Watanzania walioiamini CUF kama taasisi imara ya kuwaletea mabadiliko ya kweli watasambaratika.

 Tunajua kwamba Msajili amekuwa akiwasiliana na RITA kutia shinikizo wajumbe feki ndiyo wasajiliwe. Ni wazi Msajili ana maslahi ya ziada katika hili kwa sababu anahitaji RITA isajili wajumbe feki wa Bodi watakaokwenda kumfutia kesi zinazomkabili zilizofunguliwa na Bodi halali ya Wadhamini wa Chama. Tunayasubiri maamuzi ya RITA tuone kama na wao watageuka kama Msajili wa Vyama vya Siasa na kukubali kutumika katika kusajili wajumbe feki wa Bodi ya Wadhamini. UJUMBE WETU NA MWELEKEO WETU: CUF ni taasisi imara na imepita katika misukosuko mingi tokea kuasisiwa kwake. Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, tumevuka salama kote huko tulikotoka. Nawaambia watawala walio nyuma ya hujuma hizi kwamba kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na msukosuko huu wa kumtumia kibaraka wenu Ibrahim Haruna Lipumba nao tutauvuka salama na tutaushinda. Katika majaribu tunayoyapitia ya kutaka kuiua demokrasia kwa kuzikandamiza na kuziua taasisi za kidemokrasia Tanzania tokea 2015, nimetiwa moyo sana na ujasiri unaooneshwa na Watanzania katika kukabiliana na njama hizo na kuwapelekea ujumbe wa wazi watawala, tena pasina woga, kwamba zile zama za watawala kusema peke yao, kuwatisha na kuwanyamazisha Watanzania na kutaka matakwa ya mtu mmoja tu ndiyo yasimame, zimeshapita na hazitarudi tena.

Huu ni wakati wa wapenda demokrasia wote na wapenda amani ya Tanzania kusimama pamoja na kuilinda demokrasia yetu na kuzilinda taasisi zetu zinazoisimamisha demokrasia yetu. Kinachotafutwa hapa siyo CUF; kinachotafutwa hapa ni kuua taasisi zetu zinazosimamisha demokrasia yetu moja baada ya nyengine. Tukiruhusu kufanikiwa kwa hili, hatutaweza kuzuia mengine. If we don’t hang together, we will be hanged separately! Tusiposimama pamoja, tutamalizwa mmoja mmoja. Tusitoe mwanya huo! Binafsi nimetumia umri wangu wote kupigania demokrasia na haki za binadamu Zanzibar na Tanzania kwa ujumla na wananchi ni mashahidi wa hilo. Nimepatishwa tabu na misukosuko mingi na kupangiwa uovu mwingi huku wale walio nyuma ya mipango hiyo wakidhani wataweza kunitisha au kunikatisha tamaa. Wengi walionipangia njama hizo wameondoka na mimi wameniwacha pale pale


. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunilinda na kunipa uthabiti wa kukabiliana na yote yaliyonikuta. Moja kubwa linalonitia nguvu wakati wote ni imani yangu kwa Mwenyezi Mungu na, pili ni imani isiyotetereka wanayoionyesha wananchi kwangu. Nilichukua ahadi inayofanana na kiapo kwa wananchi walioniamini kuwa nitawatumikia katika uhai wangu wote. Na hapa tulipofikia hakuna tena cha kunitisha wala kunikatisha tamaa. USHINDI WETU UKO KARIBU, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Baada ya maelezo hayo, nihitimishe hotuba yangu kwa ujumbe mfupi ambao ndiyo lengo hasa la mkutano wetu huu leo hapa. Nawaambia watawala walio nyuma ya njama na hujuma hizi chafu dhidi ya CUF kuwa msitulazimishe kutusukuma kwenye ukuta. Tumevumilia kiasi cha kutosha, sasa basi! Nawahakikishia kwamba tutailinda CUF kwa gharama yoyote ile. Na nyinyi mlio nyuma ya hujuma hizi mtabeba dhamana ya mnayoyaandaa. Natoa wito kwa Wazanzibari na Watanzania wote wanaoiunga mkono CUF na wapenda demokrasia ya kweli kusimama imara kulinda haki yetu; ni wakati wa kulinda demokrasia ya kweli katika nchi yetu. Ahsanteni sana kwa kunisikiliza.

Maalim Seif asema hamtambui Lipumba

Maalim Seif asema wananuna mimi kuitwa Rais wa Zanzibar

Kinana amuanika Magufuli kuwa hasemezeki wala hashaurki

\

Alichozungumza Maalim Seif juu ya Lipumba

HABARI ZILIZOJIRI LEO


Topics :
 
Support : ZENJIBARZA
Copyright © 2011. ACT WAZALENDO DIASPORA NETWORK - All Rights Reserved