Headlines News :
KARIBU CUF DIASPORA NETWORK - CUF HAKI SAWA KWA WOTE...TEGEMEA KILA JIPYA NA ZURI KUTOKA KWETU...LIKE PAGE YETU KWENYE FACEBOOK
Showing posts with label MAGAZETI. Show all posts
Showing posts with label MAGAZETI. Show all posts

MAAAMUZI YA BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA LA THE CIVIC UNITED FRONT (CUF - CHAMA CHA WANANCHI) KUHUSIANA NA HUJUMA ZA DOLA DHIDI YA CUF

Image may contain: 1 person
BARAZA Kuu la Uongozi la Taifa lilipokea, kujadili na kufanya maamuzi kuhusu ajenda moja tu iliyowasilishwa kwake na Kamati ya Utendaji ya Taifa ambayo ilikuwa ni: • Taarifa kuhusu kile kinachoitwa kuwavua uanachama Wabunge wanane (8) na Madiwani wawili (2) wa Viti Maalum kupitia CUF kilichotangazwa kufanywa na Ibrahim Lipumba na kikundi chake ikiwa ni mwendelezo wa hujuma za Dola dhidi ya Chama cha CUF. Baada ya mjadala wa kina, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa linapenda kutoa maazimio yafuatayo kuhusiana na tukio hilo na mwendelezo wa vitendo na matukio mengi ya hujuma yanayofanywa na Dola dhidi ya CUF:-

1. KUHUSU UHALALI WA BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA: Kutokana na mkanganyiko unaosababishwa na upotoshaji wa makusudi unaofanywa na Ibrahim Lipumba na kikundi chake wa kuitisha watu wa kuokota barabarani na kuwakusanya Buguruni huku akiwaita kuwa ndiyo Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF, tumeona kuna haja ya kuweka kumbukumbu sahihi ili kuepusha upotoshaji huo usiendelee. Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama huwa linaundwa kila baada ya miaka mitano kupitia Uchaguzi Mkuu wa Chama ndani ya Chama na hupata wajumbe wake kupitia uchaguzi unaofanywa na Mkutano Mkuu wa Taifa (wajumbe 25 kutoka Tanzania Bara na wajumbe 20 kutoka Zanzibar), wajumbe 14 wanaoteuliwa na Mwenyekiti kwa kushauriana na Makamu Mwenyekiti na kisha kuthibitishwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa, wajumbe wanaoingia kwa nafasi zao wakiwemo Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Chama, Wenyeviti na Makatibu wa Jumuiya za Chama na Viongozi wa Kambi za Wabunge na Wawakilishi wa Chama. Viongozi Wakuu wa kitaifa wa Chama pia ni wajumbe. Wafuatao ndiyo Wajumbe halali waliochaguliwa na Mkutano Mkuu wa Taifa uliomalizika Juni 27, 2014 hapo Ubungo Plaza, Dar es Salaam kuwa wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa (BKUT) watakaokaa madarakani kwa kipindi cha miaka mitano (2014 – 2019) hadi watakapochaguliwa wengine na Mkutano Mkuu wa Taifa kwa mujibu wa Katiba ya CUF ya mwaka 1992 (Toleo la 2014):- VIONGOZI WAKUU: 1. Mwenyekiti (alijiuzulu tarehe 5 Agosti, 2015 na kujiuzulu kwake kuthibitishwa na Mkutano Mkuu wa Taifa wa dharura tarehe 21 Agosti, 2016).

Mbunge wa Temeke akamatwa kihuni

Image result for ABDALL MTOLEA PICTURES

SITAKI KUMUONA LIPUMBA ASEMA MBUNGE WA TEMEKE

Mbunge wa Temeke kwa tiketi ya CUF, Abdallah Ally Mtolea amefunguka na kusema kwa sasa hana jambo la kumshauri Profesa Lipumba na kudai haitaji hata kumuona kwa sababu ameshapoteza ile heshima na thamani yake.

Mtolea amesema hayo leo alipokuwa akihojiwa na EATV na kusema yeye alikuwa ni miongoni mwa watu ambao walikuwa wanamuheshimu sana  Prof. Ibrahim Lipumba kiasi kwamba ilifika hatua hakutaka kua muongeaji sana juu ya mambo yake lakini kwa kuwa tayari ameshajivunjia heshima mwenyewe hivyo hana budi kusema.
"Mimi nilianza kuona nia mbaya ya Lipumba pale aliponikatalia kwenda kwenye ufunguzi wa kampeni zangu mwaka 2015 kwani nilimfuata lakini yeye alikataa kabisa, lakini niliposhinda ubunge nilimfuata pia na kumpa taarifa na kumuomba tuendelee kushirikiana nikiamini yeye ni mkongwe katika siasa kuna mambo mengi ya kunishauri na kuniongoza sikumtenga kabisa, ila aliposema anataka kurudi baada ya kujiuzulu mimi sikumuelewa ni nikamfuata nikimwambia mzee unataka kutuletea mgogoro" alisema Mtolea 
Mbali na hilo Mtolea anasema saizi Lipumba amefikia hatua ambayo haambiliki chochote na kusema hatamani hata kukutana naye 
Msikilize hapa akifunguka zaidi 

Kesi YA CUF DHIDI YA RITA KUUNGURUMA JULAI 10

 

Mashauri sita yaliyofunguliwa katika Mahakama Kuu na Bodi ya Wadhamini ya CUF yanatarajiwa kusikilizwa na baadhi yake kutajwa tarehe, Jumatatu ya Julai 10, 2017, baada ya leo kuahirishwa usikilizwaji wa kesi ya msingi ya wizi wa ruzuku ya chama hicho. Kufuatia mawakili upande wa mashitaka kutopewa nakala ya maombi ya pingamizi la Mwanasheria Mkuu wa Serikali. 
Wakati akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, Wakili wa CUF, Juma Nassoro amesema leo mahakama hiyo imewapatia nakala za pingamizi hilo.
Na kwamba, Jaji Wilfred Dyansobela anayesimamia mashauri hayo amesema Jumatatu ijayo mashauri yote yatasikilizwa na kutajwa tarehe ikiwemo la kupinga maamuzi ya RITA ya kusajili wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa .
Shauri lingine litakalosikilizwa siku hiyo ni la kuzuia fedha za ruzuku ya chama hicho kupewa Profesa Lipumba na wenzake.
Aidha, upande wa Lipumba kupitia Abdul Kambaya haikuridhishwa na maamuzi hayo ya mahakama ya kuahirisha usikilizwaji wa kesi hiyo ya msingi kwa madai kuwa yanachelewesha muda.
“Sisi tulikuja kwa agizo la mahakama, badala yake jaji hakutokea tukasikia juu kwa juu kuwa kesi imeahirishwa. Wanachokifanya ni kuchelewesha muda jumatatu watazikwa,” amesema.  

TAMKO LA MADIWANI WA THE CIVIC UNITED FRONT (CUF-CHAMA CHA WANANCHI) WA MKOA WA DAR ES SALAAM JUU YA KUUNGA MKONO HOTUBA NA MSIMAMO WA CHAMA ULIOTOLEWA NA KATIBU MKUU MAALIM SEIF SHARIF HAMAD TAREHE 28 JUNE 2017 KATIKA HOTEL YA PEACOCK:

4
Image may contain: 4 people, people sitting, table and indoor
THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF-CHAMA CHA WANANCHI)
TAMKO LA MADIWANI WA THE CIVIC UNITED FRONT (CUF-CHAMA CHA WANANCHI) WA MKOA WA DAR ES SALAAM JUU YA KUUNGA MKONO HOTUBA NA MSIMAMO WA CHAMA ULIOTOLEWA NA KATIBU MKUU MAALIM SEIF SHARIF HAMAD TAREHE 28 JUNE 2017 KATIKA HOTEL YA PEACOCK:
Tarehe 5 JULY, 2017
NDUGU WAANDISHI WA HABARI,
WAHESHIMIWA VIONGOZI WA CUF,
WAHESHIMIWA WANACHAMA WA CUF,
WAHESHIMIWA WANANCHI, MABIBI NA MABWANA,
NAOMBA NIANZE KWA KUWASALIMU KWA SALAMU ZA CHAMA CHETU HAKI SAWA KWA WOTE,
1. Awali ya yote, tuanze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kutujaalia uhai na uzima na kutuwezesha kukutana hapa asubuhi hii, kwa lengo la kutoa Tamko na msimamo wetu Rasmi juu ya sintofahamu inayoendelea ndani ya Chama chetu, na kuunga mkono Hotuba na msimamo wa Chama uliotolewa na Katibu Mkuu wetu, Maalim Seif Sharif Hamad. Tukiwa ni Madiwani wa CUF, kutoka Manispaa za Mkoa wa Dar es Salaam na kupitia kwenu ujumbe wetu uweze kuwafikia wana-CUF wenzetu, Wapenda Mabadiliko wote nchini, na Watanzania kwa Ujumla.
2. Tunapenda kuchukua fursa hii kuwashukuru nyinyi Waandishi wa Habari kwa kuhudhuria kwenu na mara zote kutukimbilia kila tunapokualikeni mbali na Changamoto mnazokabiliana nazo juu ya uhuru wa Habari na aina ya uongozi wa Serikali ya awamu ya Tano jinsi unavyoikandamiza demokrasia nchini na kutopenda kukosolewa.

ZANZIBAR STONE TOWN MEMBER OF PARLIAMENT STAND WITH GIRLS

I STAND FOR THE GIRLS ... PLEASE JOIN ME
Image result for ALLY SALEH PICTURES
By Ally Saleh
Many people have come to the defence of young girls who get into wrong side and become pregnant while still at school be it at primary level or secondary one and thus cut off from following their educational programs.
Thus means not only dreams but also hopes are dashed and buried in a grave that most of them would not be able even to trace as they grow old and lament only. But then lamenting will not be enough because their lack of education might be an obstacle to their development and end up in the poverty cycle.
Most people believe that pregnancy in young girls is never wanted but these young females are caught at a time when they are not only naïve but also at an age where foolishness is only thing they do. And on top of it both young men and those of old age with good cash flow pry on these innocent souls and and trap them.
Some feel it is cruel to blame a girl of 13 or even 16 and 17 to have willingly made a choice of entering sex life and hence with no education to protect herself from becoming pregnant but even from being passed with HIV AIDS or any other sexual transmitted diseases.
A month ago a debate ensued at the Parliament about change of the 1971 Law of Marriage Act in order to change marriage age in Tanzania and a big shout was recorded with two opposing sides arguing their cases with no results. Those who refuse lean on morality and those who want it be raised to be 18 lean of reality.
There not even consensus with the Cabinet Members as the then newly appointed Minister for Constitutional and Legal Affairs Professor Palmagamba Kabudi took a cautious approach saying the government was still synthesizing the issue while Minister for Women and Health Ummy Mwallimu skipping out of official Budget presentation notes indicated that things were moving on to effect changes.
But while the debate is still raging in the public domain with consensus being sought with activists charging time was up for the changes, the traditionalist especially those with religious inclinations have been saying this was only going to happen over their dead bodies.
The latter’s argument is that if a girl was pregnant and returned to classes after delivery will poison the others on their habits, which tends to assume that the only bad thing is to become pregnant ignoring the very act of having sex which is not committed only by the girl who becomes pregnant but many and most others around her.

Uchaguziwa Mwenyekiti mpya wa CUF leo


MAJINA matatu ya wanachama wanaowania nafasi ya mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) iliyoachwa wazi kufuatia kujiuzulu ghafla kwa Profesa Ibrahim Lipumba mapema Agosti mwaka jana, yametajwa
Katika majina hayo, limo la Twaha Issa Taslima, wakili wa Mahakama Kuu nchini aliyeongoza kamati ya watu watatu kushikilia uenyekiti hadi utakapofanyika mkutano mkuu maalum wa kuchagua kiongozi mpya. Anashirikiana na Abubakar Khamis Bakary na Severine Mwijage.
Majina yaliyobaki ni ya Juma Nkumbi, Mwenyekiti wa chama hicho Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, na Riziki Shahari Ngwali, Mbunge wa Viti Maalum kutokea wilayani Mafia, mkoani Pwani. Huyu pia ni kiongozi wa wabunge wa CUF.
Majina hayo yamepitishwa na Baraza Kuu la Uongozi (BKUT) lililoketi jana kujadili majina ya waombaji tisa yatakayofikishwa mbele ya mkutano mkuu maalum unaofanyika mchana huu ndani ya Hoteli ya Blue Pearl, Ubungo Plaza, Dar es Salaam.
Mkutano huo unaohudhuriwa na wajumbe 832, kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi, Shaweji Mketo, pia utamchagua makamu mwenyekiti mpya kujaza nafasi iliyoachwa tangu kabla ya uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani ambapo Juma Duni Haji aliridhiwa kujiuzulu ili kuwania umakamu wa rais akibebwa na Edward Lowassa aliyegombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Lowassa alikuwa amekihama Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho kabla kilimkata kihujuma Lowassa katika orodha ya wawaniaji urais na hivyo kuzusha malalamiko ambayo hatimaye yamekipasua chama hicho.
Baraza Kuu la CUF ambalo pia limejadili na kupitia majina wanachama 34 wanaowania za ujumbe wa baraza hilo, limewapeleka mbele ya mkutano mkuu maalum viongozi wake waandamizi Salim Abdalla Bimani na Mussa Haji Kombo wanaowania umakamu mwenyekiti.
Bimani na Kombo wamebaki baada ya wawaniaji wenzao awali, Dk. Juma Ameir Muchi na Juma Duni Haji, kujitoa mapema. Sababu za kujitoa kwao hazijaelezwa ingawa imetajwa kuwa Duni amehofia kukivuruga chama baada ya kubainika kuwepo kundi la wanachama walioazimia kumpinga mahakamani akichaguliwa.
Mketo amewaambia waandishi wa habari mapema leo kuwa Duni amejitoa ili kulinda maslahi ya chama kwa kuwa wanaomlalamikia wanatumia kifungu cha Katiba ya chama hicho kinachozuia mwanachama aliyekihama chama kugombea uongozi mpaka atimize miaka miwili.
Chama hicho kilimuidhinisha Duni kuondoka baada ya kufanya makubaliano na Chadema pamoja na NCCR-Mageuzi na National League for Democracy (NLD) ya kuwezesha ushirikiano wao chini ya mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kusimamisha mgombea mmoja kwenye uchaguzi mkuu wa taifa.
UKAWA waliendesha walifanya kampeni maridadi lakini matumaini yao ya kutwaa madaraka yalizimwa kutokana na walichoita “mbinu kali” za CCM zilizolenga kukiwezesha kubaki madarakani. Mpaka sasa Lowassa na UKAWA wanamsimamo kuwa ushindi wao ulihujumiwa.
Matokeo ya uchaguzi huo yanatarajiwa kutangazwa leo jioni.

>
…………………………………………………………………………………………………..

MAALIM SEIF AZUNGUMZA NA WATANZANIA WA BOSTON, SEHEMU YA PILI

Na Mwandishi wetu Boston

Makamo wa Kwanza Mstaafu wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, amemaliza awamu ya pili ya ziara zake za Kimataafa hapa nchini Marekani iliyoanza wiki mbili zilizopita.

Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na Wazanzibar 

Maalim Seif, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) alikamilisha ziara yake hiyo tarehe 30 Julai kwa kuzungumza na Wazanzibari kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika katika jimbo la Massachusetts.

Mgeni huyo rasmi alikaribishwa kwa risala ya Jumuiya ya Wazanzibari waishio katika jiji la Boston kulikofanyika mkutano huo, Bwana Mohammed Lali, iliyoelezea imani yao juu ya uongozi wa Maalim Seif katika mapambano ya kupigania haki sawa na demokrasia Visiwani Zanzibar.

Akijibu risala hiyo, Mwanasiasa huyo alielezea shukrani zake za dhati kwa imani ya Wazanzibari juu uongozi wake na kuwahakikishia kuwa haki yao itapatikana.

CUF KUENDELEA KUIGOMEA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR.

Na Mwandishi wetu Boston

Maalim Seif awsili Boston kwaajili ya mkutano wa hadhara
Makamo wa Kwanza Mstaafu wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, walipowasili uwanja wa ndege wa Logan uliopo Mjini Boston

Maalim Seif Sharif Hamadi akipata picha ya pamoja na wenyeji wa mji huo

Katibu Mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad, akipata picha ya pamoja na Wazanzibar waishio jijini hapa, ili kujianda na  mkutano wa hadhara uliofanyika leo July 30, MAHALI: 42 Charles St Boston
MA 02122. 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad, amesisitiza kuwa Chama chake kitaendelea kuigomea Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Dkt Ali Mohammed Shein.

Maalim Seif Sharif Hamad 

Maalim Seif alitoa sisitizo hilo hapo jana alipokuwa akizungumza na Wazanzibari waishio nchini Marekani kwenye mkutano uliofanyika katika jiji la Boston.

"Tutaendelea kuigomea Serikali, na wala hatushirikiani nayo kwa jambo lolote", alisema Maalim Seif na kuongeza kuwa hatua hiyo tayari imeanza kuiathiri Serikali ya Zanzibar.

Maalim Seif aliwasili jijini Boston jana akitokea jijini Philadelphia ambako alihudhuria Mkutano Mkuu wa Chama Cha Democrats, uliomalizika Alkhamis iliyopita kwa kumpitisha rasmi Bi Hillary Clinton kuwa Mgombea Urais wa Marekani kwa tiketi ya Chama hicho. Uchaguzi Mkuu wa Marekani unatarajiwa kufanyika mapema mwezi Novemba mwaka huu.

Alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege, Maalim Seif anayefuatana na Msaidizi wake Bwana Issa Kheri Hussein, alilakiwa na halaiki ya Wazanzibari wakiongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazanzibari Bwana Sharif Idris pamoja na wanaharakati mbalimbali wa Demokrasia.


Akiwa Philladelphia, Mwanasiasa huyo mkongwe alipata nafasi ya kuhudhuria kwenye Kongamano la Kimataifa juu ya Uongozi Bora ambapo alipata nafasi ya kuonana na viongozi kutoka sehemu mbali mbali duniani wakiwemo Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Bwana Raila Odinga, Rais Mstaafu wa Zambia Bwana Rupia Banda, Waziri Mkuu wa zamani wa Guinea Bwana Cellou Dalein Diallo, Waziri Mkuu wa Denmark Bwana Lars Løkke Rasmussen na wengineo.

Maalim Seif na ujumbe anaofuatana nao, anaondoka leo nchini Marekani kuelekea London baada ya ziara iliyochukua muda wa wiki moja.

THE CIVIC UNITED FRONT* *(CUF- Chama Cha Wananchi)


Image result for nassor mazrui pictures

*21 JULAI, 2016*

*TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI*

Ndugu zangu waandishi wa Habari,


Awali ya yote naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia uhai na uzima wa afya na tukaweza kukutana hapa asubuhi hii ya leo. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu pia kwa kuijaalia nchi yetu kuendelea kubaki katika hali ya amani, na kuwajaalia wananchi wa nchi yetu kuendelea kubakia katika hali ya stahamala na uvumilivu mkubwa, licha ya kuwepo kwa matendo mengi ya makusudi wanayotendewa ili yawapelekee kusababisha uvunjifu wa amani na kuondoa utulivu uliopo.


Pili, nichukue fursa hii kukushukuruni nyinyi waandishi wa habari kwa kuitikia wito wetu na kuja kutusikiliza. Naamini mtatusikiliza kwa makini, hususan kutokana na uzito wa suala tulilowaitia na kwa kuzingatia hali ya nchi yetu, tunawaomba muwafikishie wananchi yale ambayo tutawaeleza.


Tumewaita leo hii ili kuzungumzia kwa kina kuhusiana na kauli za Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Ernest Mangu, na kutoa msimamo wetu juu ya mipango na mikakati ya Jeshi la Polisi dhidi ya vyama vya upinzani, hususan Chama Cha Wananchi CUF.


Juzi, Jumapili tarehe 17 Julai, 2016 wakati akihojiwa na Tido Mhando katika kituo cha televisheni cha Azzam TV na kukaririwa na magazeti kadhaa, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Ernest Mangu, amenukuliwa akisema kwamba wakati wowote kuanzia sasa, Jeshi la Polisi litamkamata na kumshitaki Katibu Mkuu wa CUF - Chama Cha Wananchi Maalim Seif Sharif Hamad kwa kuwachochea wafuasi wake ili waichukie serikali iliyopo madarakani.

Mkutano wa Hadhara, Mgeni Rasmi, Maalim Seif Sharif Hamad

 

Zanzibar Welfare Association UK

Sunday, 10 July 2016 from 16:00 to 19:00 (BST)
Barking, United Kingdom


Mkutano wa Maalim Seif Leo Washington DC


Taaswir a mbali mbali za Maalim Seif alipokua akihutubia katika kutano ulioandaliwa na (CSIS) jijini Washington DC

Katibu Mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad  akiongea jambo kujadili matokeo  ya uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015  kwenye mkutano ulioandaliwa na Centre for Strategic and International Studies (CSIS) siku ya Jumatatu June 13, 2016 ndani ya jengo  la (CSIS) liliopo Rhode Island Ave, NW jijini Washington DC. (Picha zote kwa hisani na 

Katibu Mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad, akielezea hali halisi ya siasa za Zanzibar, katikati akiwa na Mkurugenzi wa CSIS  Afica Bi Jennifer G. Cooke, pamoja na aliekua balozi wa Marekani nchini Tanzania Mark Green, ambae sasa hivi ni  President, International Republican Institute

Aliekua balozi wa Marekani nchini Tanzania Mark Green, ambae sasa hivi ni  President, International Republican Institute, akionge siasa za Zanzibar.<iframe width="640" height="420" src="https://www.youtube.com/embed/mCbaYd3PzTM" frameborder="0" allowfullscreen></iframe>

Gazeti la Annur

Gazeti lako la ANNUUR Toleo ya 1203

c

Nakala ya Annur July 10-16

 DONDOO MUHIMU
1 'Mfungwa' asimulia mateso rumande
- Shukrani zikufikie ‘Afande Dada mmoja’
- Amnusuru mtuhumiwa kuoza mkono
- Mtuhumiwa wa ugaidi amsilimisha


2 Makundi haya mithili ya Anti-Balaka Vs Seleka…
- Tunataka kuipeleka wapi Zanzibar?
- Kampeni bado, watu wanapigwa risasi
- Kutakalika au Bububu waanze kuhajiri?
3 ‘Mauwaji ya Al-Shabaab’ tena Kenya…
- Tujifunze kutoka Shambulio la Kimeta
- Akitujia fasiki na habari, tuchunguze
- Huu ndio uadilifu na ndio salama ya nchi
4 Ramadhani inaondoka
- Tukumbuke kutoa Zakatul-Fitri
5 Sheikh maarufu afariki kisiwani Pemba
6 Dk. Bilali ashukuru Waislamu kwa kuombea Taifa amani
- Mwinyi awashutua wanaopalilia farka

https://www.scribd.com/doc/271230477/ANNUUR-1185-pdf

ZEC yatangaza majimbo 4 mapya


Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salim Jecha akito taarifa kwa vyombo vya Habari kuhusiana na mabadiliko ya Mipaka na Idadi ya majimbo katika hoteli ya Grand Palace Zanzibar.

Ndugu Waandishi Tume ya Uchaguzi inapenda kutoa taarifa kuwa imekamilisha kazi yake ya uchunguzi wa Idadi, Mipaka na Majina ya majimbo ya Uchaguzi. Tume imeongeza idadi ya majimbo manne ya uchaguzi ya Wawakilishi na kufanya jumla majimbo yote kuwa 54 badala ya 50 yalokuwa ya awali.
Baada ya maelezo hayo, sasa naomba niwatangazie majimbo ya uchaguzi yatakayotumika katika uchaguzi wa mwaka 2015. Soma zaidi hapa: –

Gazeti la Annur Ijumaa ya Tar 2 Julai


 Tembelea link hii hapa chini kupata nakala kamili ya toleo la Annur-1183

Toleo la Annur June 23


Toleo la Annur Ijumaa iliyopita
DONDOO MUHIMU
1 Waislamu Mbeya wavunja rekodi
- Tamasha lakusanya watu 700
- Ni mfano wa Jihad ya mali, nafsi

2 Elimisheni-Totonji
- Wapeni wake zenu amani, furaha
- Imarisheni ndoa na familia zenu
- Msihangaishwe na propaganda

3 Sumaye amesahau mauaji ya Wazanzibari mwaka 2001?
4 Kuukaribisha mwezi wa Ramadhani - Tahariri
5 Mufti Simba: Taifa limepoteza kiongozi muhimu
6 Bunge la Ulaya lawatetea wakazi Gaza
- Waweka saini kuondolewa mzingiro
7 Jinamizi la kutoroka wanajeshi Israel
- Wahalifu watumika kuziba pengo
8 Mafundisho ya Qur’an
9 Kwa mwendu huu....
CUF kuingia Ikulu, labda ngamia apenye kwenye tundu la sindano
10 Ukristo umenyauka Ulaya
- Maelfu wanakimbilia Uislamu
- Wengi ni wasomi, Wanawake
- Kanisa la Venice lageuzwa Msikiti
11 Propaganda za udini shuleni Tanzania-7
- Profesa Ibrahim Noor Shariff
12 Yaliomo ndani ya Ramadhani kwa mja
Na Ben Rijal
13 Fiqh ya Funga
14 Funga na uhakika wa misaada ya kijamii
15 Ulaji usiofaa unavyokwamisha funga ya Ramadhani kuleta siha
16 Dunia tunayoishi ndani ya Quran-1

Ingia katika link hii hapa chini kupata nakala nzima ya gazeti la Annur kwa sura ya PDF

https://www.scribd.com/doc/269445456/ANNUUR-1182-pdf

ANNUUR 1182.pdf by annurtanzania

Gazeti la Annur June 14

Patana nakala yako ya Annur kila Ijumaa
 DONDOO MUHIMU

1 Guantanamo Dar!
- Aljazeera Ukerewe yazima uzushi wa ‘Jihad John’-3
- Waalikeni Polisi, 'Task Force' Misikitini wajione!
- Mwenzao alisilimu baada ya kutesa Guantanamo
- OCD Nansio ajionea. Sasa ahimiza ‘Doria ya Nafsi’


2 Tafrani Segerea
- Ustadh Salum Ally alala juu ya mti
- Amtaka Mwanasheria Mkuu Zanzibar
- Sheikh Farid aitwa kuepusha balaa

3 Vitabu hivi vichomwe moto
- Kwa nini Wizara inaruhusu kutukanwa WaislamU

4 ‘Ushindi lazima’ Zanzibar Woga ukizidi huzaa ujasiri
- Usanii wa vitambulisho upo wazi

5 Karibu Ramadhani
6 Serikali ina nia mbaya-Wakili
- Ni juu ya akina Sheikh Mselem
- Mgomo wapamba moto Segerea

https://www.scribd.com/doc/268524336/ANNUUR-1181-pdf

ANNUUR 1181.pdf by annurtanzania

HABARI ZILIZOJIRI LEO


Topics :
 
Support : ZENJIBARZA
Copyright © 2011. ACT WAZALENDO DIASPORA NETWORK - All Rights Reserved